Hongera zangu kwa mkuu wa mkoa wa Geita

besaro

Member
Nov 9, 2015
52
40
Leo ningependa kutoa pongezi za dhati kwa mkuu wa mkoa wa geita engineer Gabriel kwa mambo anayoyafanya

Ukiangalia mkoa wa geita ni kama kitovu cha biashara ya madini ya dhahabu hapa Tanzania zaidi ya 75% inatoka hapa mbali na migodi mikubwa ya ggm bali kuna migodi midogo mingi sana. Kwa hivi biashara ya madini imeshamiri sana

Mbali na madini lakini pia hali ya hewa bado ni nzuri kwa mazao mengi ya chakula kama mahindi, mpunga, viazi, mhogo, n.k

Lakini ukija kuangalia maendeleo ya mkoa bado yalikuwa chini sana huwezi hata ukafananisha na kahama ambayo ni wilaya. Mambo mengi yalikuwa chini sana

Lakini naona mabadiliko makubwa yanafanyika kwa sasa chini ya mkuu wa mkoa mpya eng. Gabriel mfano kwa sasa naona ameweka taa za barabarani , ujenzi wa soko la kisasa, maboresho ya barabara za mitaa, huduma za hospitali

Mbali na hilo huyu rc ni mtu wa watu sana utamkuta mda mwingine kajichanganya na watu kwenye kahawa kuzipata changamoto zao na yeye sio mtu wa maneno mengi au wa kujionesha au weka mtu mtu masaa 48, yeye ni maendeleo tu


Hongera sana hata kama kuna watu wanakukatisha tamaa ila wewe songa mbele tu manake hawakosekani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hongera zake RC na Wadau wote, nimepita huko karibuni Kuna mabadiliko.Tuwape moyo viongozi wanaojitoa kutumikia jamii kwa dhati.Hana siasa za fitina nimchapa kazi hodari sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hata Ruangwa/Namungo mambo ni fire kwa sasa hata OKWI analijua hilo.
 
Back
Top Bottom