singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,536
UCHAGUZI wa Marudio ulifanyika Zanzibar jana, ambapo watu wengi walionekana vituoni kuanzia saa 1:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni, wakitumia haki yao ya kidemokrasia kupiga kura.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (ZEC), Jecha Salum Jecha, uchaguzi huo uliendeshwa kwa usalama na amani. Tunapongeza wananchi hao kujitokeza kwa wingi kupiga kura kuchagua Rais wa Zanzibar, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na madiwani.
Wagombea urais katika uchaguzi huo wa jana ni Dk Ali Mohamed Shein wa CCM, Seif Sharif Hamad wa CUF, Juma Ali Khatib wa TADEA, Khamis Iddi Lilla wa ACT Wazalendo, Hamad Rashid Mohamed wa ADC na Said Soud Said wa AFP.
Wengine ni Ali Khatib Ali wa CCK, Mohamed Masoud Rashid wa CHAUMMA, Abdalla Kombo Khamis wa DP, Kassim Bakari Ali wa Jahazi Asilia, Tabu Mussa Juma wa Demokrasia Makini, Seif Ali Iddi wa NRA, Issa Mohamed Zonga wa SAU na Hafidh Hassan Suleiman wa TLP.
Pia, tunapongeza wakazi wa Jimbo la Kijitoupele kisiwani Unguja, kwa kupiga kura kuchagua mbunge wao, baada ya uchaguzi wa Oktoba mwaka jana kutofanyika, kutokana na vifaa vya kupigia kura kuchelewa kufika katika maeneo mbalimbali ya jimbo hilo.
Vifaa vyote muhimu vinavyohusika na kazi ya kupigia kura, vilikuwepo katika vituo vya kupigia kura katika visiwa hivyo vya Pemba na Unguja. Kwa upande wa Kisiwa cha Pemba, Ofisa Mdhamini wa ZEC Kisiwani Pemba, Ali Mohamed Dadi alifafanua kuwa vifaa vingi vilikuwa vimesambazwa katika jumla ya vituo 463 vya kupiga kura Pemba, ambapo kituo cha Mkoani kilikuwa na vituo 117, Chake Chake vituo 122, Micheweni vituo 91 na Wete vituo 133.
Jambo lingine linalostahili pongezi ni utulivu wa hali ya juu, uliokuwepo katika vituo vingi vya kupiga kura. Hata wananchi wengi na waangalizi wa kimataifa, walisifia hali hiyo.
Kundi lingine linalostahili kupongezwa ni Jeshi la Polisi na vyombo vingine vya ulinzi na usalama, vilivyoweza kuimarisha ulinzi katika kipindi chote cha maandalizi ya uchaguzi huo wa marudio na upigaji kura. Tuna imani utulivu huo, utaendelea wakati wote wa kuhesabu kura, kujumlisha kura na utangazaji wa matokeo.
Kwa ujumla, Wazanzibari wanastahili pongezi kubwa kufanikisha uchaguzi huo wa marudio. Uchaguzi huo wa marudio, ulifanyika jana baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana, kufutwa na Mwenyekiti huyo wa Tume, Jecha.
Jecha alitangaza kuwa kwa uwezo alionao, uchaguzi huo wa mwaka jana na matokeo yake yote yamefutwa na kwamba kulikuwa na haja ya kurudia uchaguzi huo. Alisema aliamua kufuta uchaguzi huo, kwa kuwa alikuwa ameridhika mwenyewe kama Mwenyekiti kuwa uchaguzi huo, haukuwa wa haki na kulikuwa na ukiukwaji mkubwa wa sheria na taratibu za uchaguzi.