Hongera wasanii maarufu wa CCM

Hongera wasanii maarufu wa CCM

Karimama

Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
13
Reaction score
4
Habari kwamba wasanii maarufu wa Bongo wamemfanyia 'semnd-off' JK na kumualika pia mgombea urais wa CCM, JP Magufuli, inaamsha hisia za huzuni kubwa kwangu na pia kwa wengine wenye mtazamo mpana.

Kwa tathimini ya chini kabisa, juu ya maandalizi ya 'send-off' ile, ni lazima wasanii hao walitumia si chini ya sh. milioni 250 kwa ajili ya maandalizi ya vitu vyote vilivyogharimu shuhuli ile iliyoandaliwa ghafla mno.

Kiasi hicho, ambacho ni kikubwa mno kwa mapato ya wasanii wanaolialia kila siku kwa ukata, kinatokana na gharama za kukodi ukumbi, chakula, mapambo na hata jukwaa achilia mbali ile picha waliyomkabidhi JK.

Wajuaji hawaamini kuwa gharama zile zilitolewa na wasanii wenyewe, kwa sababu kumshaanza kuwepo malalamiko toka baadhi ya wasanii kutolipwa fedha walizoahidiwa na waandaaji halisi wa shughuli ile. Fedha za malipo ya kutumbuiza.

Lakini tukubaliane kuwa hafla ile iliandaliwa na wasanii kwa fedha za mifukoni mwao kama wanavytoaka tuaamini. Ila wakati tukiamini hayo, tujiulize pia hivi kufanya seherehe ya mamia ya mamilioni ya fedha kama ile kuna tija mno kuliko maisha ya wasanii wenzao?

Nakumbuka:

Mikaka michache iliyopita, msanii maarufu wa maigizo, mzee Small Ngamba alifariki dunia kutokana na maradhi ya kupooza huku akilalamika kuwa hana pesa za matibabu.

Kabla ya hapo, Sajuki, msanii mwingine wa Bongo Movie, naye alifariki kwa ugonjwa wa kansa ya damu baada ya kukosa matibabu kwa wakati. Naye ilikuwa hiyo, alikosa pesa za matibabu mpaka pale Zitto Kabwe alipopitisha kwa mbinde michango kwa ajili ya matibabu yake.

Inakumbukwa pia mzee Kipara na mzee Pwagu, wasanii maarufu zaidi wa nchi hii, nao pia walikufa vifo vibaya vya maradhi kwa kukosa fedha za matibabu kwa maradhi ambayo pengine yasingesababisha umauti wao iwapo wangepeta fedha za matibabu.

Wasanii hao wote, Mungu awaweke mahali pema, mara kadhaa walizungumzia hali ya maradhi yao na kuomba msaada wa fedha kwa wasanii wenzao lakini hawakupata msaada uliostahiki.

Ndorooobo nyie!

Kwa mazingira hayo, iwapo kweli wasanii maarufu wa CCM walichangia shughuli ile, basi watakuwa 'mandorooobo' wasiojielewa wala kutafakari mustakabali wa 'maisha yao ya kuigiza' ambayo pindi yanapokuja matatizo ya kiasili kama maradhi huanza kutapata.

Lakini kwa vile inajulikana fedha zile si zao, ni vyema wafahamu kuwa walichofanya usiku ule kimewanufaisha zaidi wale waliopewa tenda ya kuwakusanya wao na kisha kuwatumia kama mambumbumbu wanaoweza kutumiwa kukampeni kwa ujira wa ubwabwa na juisi ya usiku mmoja.

Hela walitoa ccm wakawadanganya watanzania kuwa wasanii wametoa wasanii hiyo ni propaganda ya siasa.
 
Ndoroboooooooooooooooooooooo

Hahahahahahhahahahahahahahah

"send off " ya Mr President hahahahahaha
 
Acheni kujifanya mnajua vizuri mifuko ya watu
 
Kama kuna kipindi kikwete kachanganyikiwa ni hiki..Alishawahi kuwaambianwenzie ndani ya CCM kuwa wajiandae kisaikolojia kuwa wapinzani sasa mbona anataharuki? Hakuna jinsi Magufuli atashinda uchaguzi ujao..hakuna
 
Na hapa bila kupepesa macho walionufaika ni Clouds chini ya Ruge lazima walipiga ''Over Budget'' chenchi wakaweka kimiani then hao vilaza wakaingia ukumbuni kupiga picha,kula wali na soda.
 
Mnalialia nini nyie wapuuzi. Mnataka watu waache kufanya mambo yao kwa uhuru kisa siasa zenu uchwara? Hivi angefanyiwa mgombea wa UKAWA mngelialia hivi? Mnataka kujifanya wajuaji hata kwa vitu visivyo wahusu. Hafla ilikuwa ya Mh JK na wasanii full stop. Mkitaka waalikwa mnaowataka nyie andaeni ya kwenu ili mridhike na nafsi zenu. Kama nimeamua kutumia hadi senti yangu ya mwisho ili kumuaga Mh. JK na kuungana na MH Magufuli wewe kinakuuma nini? Kwani kuna siku nilishakuja kwako kukuomba msaada, au nililala na njaa nikaja kuomba chakula kwako?
 
Kama kuna kipindi kikwete kachanganyikiwa ni hiki..Alishawahi kuwaambianwenzie ndani ya CCM kuwa wajiandae kisaikolojia kuwa wapinzani sasa mbona anataharuki? Hakuna jinsi Magufuli atashinda uchaguzi ujao..hakuna
I guess wewe na wenzako ndio mmechanganyikiwa ndio maana mnaanzisha mada za jambo lisilowahusu. Kama ile hafla haina madhara kwenu kwa nini msikae kimya. Hizi mada mnaanzisha kila dakika ni za nini kama siyo kupanick?
 
Mnalialia nini nyie wapuuzi. Mnataka watu waache kufanya mambo yao kwa uhuru kisa siasa zenu uchwara? Hivi angefanyiwa mgombea wa UKAWA mngelialia hivi? Mnataka kujifanya wajuaji hata kwa vitu visivyo wahusu. Hafla ilikuwa ya Mh JK na wasanii full stop. Mkitaka waalikwa mnaowataka nyie andaeni ya kwenu ili mridhike na nafsi zenu. Kama nimeamua kutumia hadi senti yangu ya mwisho ili kumuaga Mh. JK na kuungana na MH Magufuli wewe kinakuuma nini? Kwani kuna siku nilishakuja kwako kukuomba msaada, au nililala na njaa nikaja kuomba chakula kwako?

Mbona povu jingi? Zingatia hoja sio kutoa povu tu. Ulikosa ubwabwa nini kwenye 'send-off' yenu?
 
Mbona povu jingi? Zingatia hoja sio kutoa povu tu. Ulikosa ubwabwa nini kwenye 'send-off' yenu?

Ningekosa ubwabwa ungeshaona nimekimbilia kutoa mada za kijinga kama hii ya kwenu.
 
Ningekosa ubwabwa ungeshaona nimekimbilia kutoa mada za kijinga kama hii ya kwenu.

Kwa hiyo ulipata ubwabwa? Ndio maana unatoa hoja za kuvimbilwa! Hivi ni kweli kabisa kwa akili yako unaamini Rais alistahiki kufanyiwa 'send-off' ile? Kwa lipi kubwa alilowafanyia wasanii? Ile 'studio hewa' waliyoiteka kina Runge au? Halafu kweli kwa akili zako 'nyingi' kiasi hicho unafikiri kuwepo na mfuko wa kusaidiana wasanii wakati wa maradhi au kuchangia mamia ya malioni ya kula ubwabwa ni kipi cha muhimu?
Tehe tehe tehe teheee. CCM Oyeeeee!:smile-big:
 
Wasanii wa tz ni mandoroooobooo manyau kabisa
 
Back
Top Bottom