Hongera: Wanawake ni watu wazuri sana

affinitytz

Senior Member
Feb 10, 2020
109
500
Wanawake ni watu wazuri sana.

Nikikumbuka haya matukio huwa nawatazama wanawake na kuwaona kuwa ni watu wazuri sana. Leo nitazungumzia uzuri wa wanawake ambao hawakuwahi sina undugu. Hawa ni wale tu ambao nilikutana nao barabarani.

1. Yupo mwanamke alinipenda sana kwa sababu tu ya kuwa karibu na mtoto wake mdogo ambaye alikuwa na albinism (alikuwa na uzeruzeru). Huyu dada nilimkuta kwenye nyumba niliyokuwa nimepanga watu wengi pale mtaani walikuwa wakimnyanyapaa huyu mtoto, niliishi pale kwa raha sana, nikaanza kumzoea mtoto, nikitoka jumapili jioni naenda naye kutembea, nikirudi pale tutakimbizana na kufurahi pamoja. Mama wa mtoto akanielewa sana, kwa kweli nilifaidi sana. Maana niliambiwa hata kupika nisipike na nikawa nakula kwa huyu dada.

2. Nikikumbuka yule mama pale Kijitonyama aliyeniambia nisilipe kodi baada ya kugundua kuwa nilikuwa sina kazi baada ya kumaliza chuo. Alinisaidia mpaka kupata kazi. Wanawake ni watu wazuri.

3. Nikikumbuka yule mwalimu wangu wa kike aliyejitolea kuninunulia chai kila siku nikiwa shule fulani hapa mjini kwa miaka miwili kwa sababu tu nilikuwa nafaulu somo lake. Wanawake mna sifa za kipekee.

4. Nikikumbuka yule mama ambaye alikuwa ananipa hela za shule ili tu nimsaidie binti yake kupenda hesabu na kumshauri kwenye masuala ya kusoma na kuepuka mambo ya makundi, hakika wanawake ni watu wema sana

5. Nikikumbuka yule dada wa Cafteria pale chuoni ambaye baada ya kuniona kila siku nakula wali mbogamboga au nikibadili wali nyama akaamua kunipa offer ya bure kula wali kuku kila wiki mara mbili. Huyu alikuwa dada anauuza cafeteria, yeye ndio alikuwa anapokea vile vikaratasi vilivyoandikwa aina ya chakula ulicholipia na kukupakulia.

6. Nikikumbuka yule dada ambaye alinipokea ofisini akiwa ndio mkuu wangu wa idara lakini akanielekeza kazi kwa upole sana, na alipokuwa anaacha kazi akapendekeza mimi na kuwa mkuu wa idara licha ya experience yangu kuwa ndogo miaka ile. Wanawake ni watu wema sana.

7. Nikikumbuka namna ambavyo dada mrembo Ramla alivyojitolea kuniletea chakula kila siku wakati nikiwa nakaa camp na wanafunzi wenzangu kujiandaa kwa mtihani wa kidato cha sita. Binti ilikuwa ananifungashia mapochopocho, analeta chakula cha kutosha usiku na kuniambia kingine nibakishe kwa ajili ya chai asubuhi. Wanawake mpo juu sana.
Nikikumbuka namna ambavyo yule dada alikubali tuyamalize mimi na yeye baada ya kuonyeshwa mipaka feki ya kiwanja na kuingia sehemu ya kiwanja chake. Badala ya kuniambia nivunje lakini alikubali kuacha ukuta niliojenga ndani ya kiwanja chake bila malipo yoyote.

8. Nikikumbuka yule dada aliyenilipia nauli ya kurudi Dar baada ya kupoteza pochi yenye pesa pale Mkwakwani Tanga, huyu baada ya kugundua nimepoteza pochi akaniuliza una nauli ya kurudi Dar, nikamjibu hapana. Akatoa elfu thelathini 30,000/- sikuwahi kukutana naye tena. Nilirudi Tanga lakini alikuwa amehama na namba niliyopewa haipatikani.

Nina mengi mazuri ya kuandika juu ya wanawake, lakini niishie hapa. Wanawake ni watu wazuri sana.
 
Scolari

JF-Expert Member
Aug 25, 2017
648
500
Wanawake ni wakarimu Sana

Namshukuru mama yangu Kwa kunizaa na kunilea ktk maadili Bora

Namshukuru mama yangu Kwa upendo wa ajabu kwangu

Namshkuru Sana yule dada aliejitolea kunipenda na kujali Kwa kunipa kila kitu

Wanawake ni watu wakatili sana
Wewe mdada uliekua unasoma chuo Dodoma niliekupenda Kwa dhati pamoja na kunionesha mara kadhaa kwamba unanisaliti ikiwemo kutuma picha zako za uchi Kwa watu ambao walianza kukutisha kwamba watazitoa ili uwape hela nikakusaidia kwenye Hilo tatizo lakini bado ukansialiti Kwa sababu ulikua siwezi kukuacha na mwisho wa siku nikashindwa uvumilivu nikakutema na sasa hivi unanisumbua Acha ukome na Roho mjinga wewe

Wanawake wapuuzi mnaotafuta mimba kisha mnazitoa nyie ni wapuuzi

Wanawake mnazitoa mimba na kuridhia kuiba watoto wa wenzenu hospital nyie ni mbwaaaaaa

Wanawake mnaotoa mimba halafu mnaogopa kuua mende ndani acheni unafiki nyie mbwaaaaaa

Wanawake mliotayari kuwanyonya wanaume wenu kiuchumi ilihali mnajua Wana Hali ngumu nyie ni mbwaaaaaa

Wanawake msioshiriki shughuli za kifamilia na mna dai HAKI Sawa nyie ni mbwaaaaaa

Wanawake mnaosema HAKI sawa huku mkitegemea wanaume wawalishe an kuwavalisha mpaka mnatoka vitambi nyie ni mbwaaaaaa

Wanawake mna wanyima papuchi waume zenu nyie ni mbwaaaaaa

Itoshe kuishia hapa niwape break au niendelee??
 
leloic

JF-Expert Member
Apr 6, 2013
621
1,000

Mkuu mbona unachafua uzi wa watu siufungue wakoo
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom