Slim5
JF-Expert Member
- Jan 7, 2014
- 28,163
- 37,801
Kukataliwa!
Umewahi kukataliwa? Kukanwa? Kutoswa? Kuachwa? Na yanayofanana na haya! Kifupi ni ile hali ya kutokukubalika tena! Wengi wanaichukia hali hii, hawaipendi, inawaumiza, lakini nakusihi soma hili andiko mpaka mwisho ujionee faida za KUKATALIWA, KUKANWA au KUTOSWA! Mara kadhaa KUTOSWA huja katika sura tofauti tofauti zikiwemo kauli za kiungwana mf. Katika masuala ya ajira utaskia: Kwa sasa hivi hatuhitaji mtu wa aina yako, labda baadae! Uko vizuri ndugu, kinadharia na vitendo, utatufaa sana ktk kampuni yetu, lakini tumefikiria kumchukua mtu mwingine! Katika Mapenzi utaskia, ni handsome/beautiful lakini siwezi kuwa na wewe! Nakupenda lakini ni ngumu kuendelea na wewe kwa sasa! Hizi zote ni siasa, kifupi hutakiwi! Katika masuala ya Siasa kuna kufukuzwa kama Msaliti, kuna kulazimishwa kujiuzulu, kuna kukatwa, n.k.
1. Kutoswa kunatumotisha kufanya vizuri zaidi!
Yale maneno ktk matokeo ya interview za ajira eti umefanya vizuri lakini tuna nafasi moja tu na hivo tumeamua kumchukua Yule, yanaumiza lakini ukweli unabaki pale pale kuwa huyo wanaemsema wanamchukua kafanya vizuri zaidi yako, hivo ni fursa sasa ukajipange upya kama ni practically ama theoretically ili wakati mwingine uweze Kutoka! Kifupi kama ungekubaliwa ungeenda kuanza kazi ukiwa na uboya ama mapungufu kibao! Bora walivokutosa, ukajifunze upya!
2. Kutoswa kunatukumbusha kuwa “sisi ni binadamu!”
Maisha ni movie na kila mtu ni star wa movie yake, ukiwa kama star, wanaokuzunguka wanataka ustar kwa kukushusha wewe, hivyo basi kubali kuumia, kuumizwa kwani sio kila binadamu anapenda kuona ulipo! Hiyo ndio hulka kwa wanadamu, wengi huishi na philosophy yao ya tuwe ote sawa!
3. Kutoswa kunatufunza SUBIRA!
Waswahili ni mabingwa wa faraja, Utawaskia. Kuvunjika kwa koleo…..! Wengine utawaskia: Kufa kwa Imamu….! Huvuki mto mpaka ….! Au Kila Masika na Mbu wake! Kifupi wahenga wanasema kutoswa kunauma, sana, lakini ni mapito tu, unapaswa kuwa na subira ya hali juu ili upate kuvuka salama! Kwamba kunamaisha baada ya kutoswa!
4. Kutoswa kunakupa njia mbadala!
Wanasema wenye kusema, mapenzi kiti cha basi, ukishuka…! Umekataliwa na Anna, akili inakupeleka kwa Mwajuma. Umeshindwana na Yanga, Azam na Simba wanakunyatia. Yamekufika hapa SISIEMU, huyooo unaenda zako CHADEMA! Wengi hatujui tu, haiwi kutoswa kunatokea isipokuwa mtoswa ana njia mbadala ambayo ilifungwa na uwepo wa maisha yale ya awali! Ukitoswa njoo tukale bata!
5. Kutoswa kunatusukuma tujiangalie upya!
MwanaFA aliwahi kusema katika moja ya nyimbo zake: “Kama unatoswa jiulize, ni fukara ama huna hela!” vyovyote iwavyo, mwenye kutoswa akisema na moyo wake bila unafki, atajiona na mapungufu yake, labda kama atajitoa ufahamu kama mbuni, kuficha kichwa mwili ote nje!
6. Kutoswa kunatulazimisha kubadili dira au malengo yetu!
Hujaumbwa kung’ang’ana na mtu mmoja, chama au sehemu moja, yamekushinda DSM basi kajaribu Mwanza, yamekushinda Tanzania nenda kajaribu Palestina, kama umetoswa na James, kaa tulia, msubirie Jane amtose Charles ujibebee! Kwa kifupi malengo yako sio msahafu, kaa tayari kuyabadilisha wakati wowote ule, acha uboya, no situation is permanent!
7. kutoswa ndio chanzo cha mabadiliko!
Kuna watu wagumu kubadilika mpaka watoswe! Hawadiliki mpaka wakatwe, wakataliwe, watoswe, usiwe kama mti au gogo, kama kusoma huwezi, kodoa macho kwa picha, simama, jikung’ute. Anza mwendo! Hata usiku hupisha mchana!
8. kutoswa kunakufanya upate akili mpya!
Ukishatoswa akili mpya itakujia. Mawazo mapya, mazingira mapya. Kifupi kutoshwa kunakupa akili na macho mapya ya namna ya kuyaona mambo, maisha na watu wake tofauti na ulichokuwa unaamini ama kuona mwanzo!
9. kutoswa kunakufanya uwe mwenye nguvu!
Ukimuona nyani kazeeka ujue kakwepa mishale mingi. Kubali kuoana na mtalaka, kuna raha yake, keshatumika sana! Anajua mengi. Atakupa mengi. Wanaopenda chura, pia hupenda doggy! Usisahau msemo wa wazungu: experience matters. Kwa kifupi wengi waliotoswa huja kuamka na nguvu ,mpya, inawezekana ikawa nguvu kubwa!
10. Kutoswa ndio kukua!
Sio kilakutoswa unakuchulia katika mtazamo hasi. Wengi wetu hapa tulipo leo, ni matokeo ya kutoswa ama kukataliwa wakati Fulani, pahala Fulani, na watu Fulani. Inawezekana hapa tulip oleo tusingefika ama tungechelewa kufika kama watu wale, wa sehemu ile, nyakati zile wasingetukataa, wasingetutosa!
Somo langu kwako, ukitoswa, ukikataliwa, usikurupuke na kuanza kujuta ama Mipango ya kurevenge, la hasha. Kaa chini, pumzika, andaa mkakati wa kugeuza kutoswa kwako kuwa ndio njia mpya, mwanzo mpya na hatimaye kuwa mtu mpya!