Hongera wabunge kwa kuwa wamoja | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hongera wabunge kwa kuwa wamoja

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by rutebukasabas, Jul 19, 2011.

 1. r

  rutebukasabas Member

  #1
  Jul 19, 2011
  Joined: Apr 18, 2011
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inapendeza kuwaona wabunge wamekuwa pamoja kwa kupinga budget ya Nishati na madini. Hili ni swala la kitaifa zaidi kuliko chama. Hili ni fundisho kwa serikali kuwa haitaweza kuwafanya rubber stamp kwa uozo ulio wazi kwa kila mtu.

  Wiki tatu walizopewa wasiishie kutoa mapendekezo tu ya Nishati,bali wachukue hatua pia kwenye mikataba mibovu ya madini isiyo na tija kwa wananchi.

  Kumbe ina wezekana! Hongera Upinzani kwa kuwa INDUCE wa bunge wa CCM. Wakati wa wabunge wa CCM kuwa kamati ya chama na kuwa rubber stamp umekwisha. Haya ni mafanikio !!!!!!!!

   
 2. S

  SEAL Team 6 JF-Expert Member

  #2
  Jul 19, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hao waliopokea rushwa kutoka kwa jairo nao wapo pamoa na wabunge watiifu?????
   
 3. M

  Mbalinga JF-Expert Member

  #3
  Jul 19, 2011
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 1,381
  Likes Received: 407
  Trophy Points: 180
  Nadhani si sahihi sana kusema kuwa walikuwa wamoja. Baada ya Waziri mkuu kuchomoa hoja ya Bajeti ya Wizara ya Nishati, niliwasikia baadhi ya wabunge wakishanglia CCM! CCM! na wengine wakisema People's power, sasa haya mambo ya vyama yanatoka wapi tunapozungumzia suala nyeti la kitaifa?

  Ukweli ni kuwa Chadema wamejiona kama wapinzani wa serikali, na wabunge wa CCM wamestuka kuwa kama wataunga mkono hoja hiyo basi CDM wakienda kwa wananchi watawamaliza. Bado nadhani uzalendo wa kweli bado haujapatikana. Bado tuna safari ndefu sana kuwa pamoja na kuiwajibisha kabisa serikali hii lege lege.
   
 4. d

  dotto JF-Expert Member

  #4
  Jul 19, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  WAbunge kuwa kitu kimoja ni maamuzi ndani ya ukumbi wa Bunge na sio kuamua nje na Ukumbi wa Bunge. Huo ni unafiki.
   
Loading...