Napenda kutoa pongezi kwa kituo chetu pendwa cha TBC1 kwa kujaribu na kujitahidi kwa viwango vya chini kabisa kama si sana kutoa habari za wapinzani zenye muelekeo chanya.
Jana nilikuwa napata kinywaji katika viunga vya mji mdogo wa Arumeru [USA RIVER] na bahati nzuri nikawa natazama taarifa ya habari ya saa 2 TBC waliitoa habari ya Mheshimiwa Mbowe kuhusiana na ombi lake la kusafisha magereza kwa Mheshimiwa Jaji Mkuu,IGP na Commissioner General wa Magereza.
Kwa kawaida Mimi si miongoni mwa watazamaji wa TBC,niliacha siku nyingi kuitazama TBC kwakuwa walikuwa wamejikita katika kusifia tu.Habari zao nyingi si balanced hata kidogo,viwango vyake vya habari huwezi kuvifananisha au kuvilinganisha na enzi za Tido akiwa Mkurugenzi Mkuu.TBC ili cover uchaguzi wa Kenya baina ya Raila na Mwaikibaki katika viwango ya BBC.
Leo TBC imekuwa kichekesho,kituko kwajinsi inavyowapatia habari waTanzania,unaweza kufikiri Dr Rioba kalogwa au pengine si yeye.Ni bahati mbaya jana nilikuwa bar nyumbani kwangu ni marufuku kuitazama TBC.