Hongera TANESCO kwa kuonyesha ustaarabu

Hongera TANESCO kwa kuonyesha ustaarabu

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,685
Ni kawaida kwa shirika la umeme TANESCO kukata umeme bila kutoa taarifa kwa wateja wao tunaoishi mabonde kwinama (hasa nje ya mji).

Nashukuru kwa Mara ya kwanza katika eneo langu kuwaona TANESCO wakipita na gari lenye kipaza sauti wakiwatangazia wananchi kuwa watakata Umeme na kuurudisha kwa muda (...) uliopangwa.

"BigUp TANESCO mnaanza kujitambua, na kututhamini sisi wananchi, na kutambua kuwa sisi ndiyo wateja wenu' tunaowalipa mishara, na kulipa kodi kwa serikali".
 
Mkuu, chunguza vizuri, labda kuna kigogo wa ccm kapata kiwanja huko bondeni kwenu. Siye huku tunalaani hilo shirika tukitamani ligawiwe watu masikini waliendeshe. Vyombo vyetu vyote vya umeme kwisha habari yake. Pa kwenda kulilia hakuna, tumebaki na mafriji kuwa kabati na mafriza kuwa matangi ya maji. Hongera zenu mlio ambiwa mapema
 
Mbona siku zote wanatoa taarifa katika vyombo vya habari na hata mitandao ya kijanaa kabla ya kukata umeme.sema sisi huwa hatuna utaratibu wa kufatilia habari maana Kila siku wanatoa taarifa hata humu jf huwa wanatoa pia
 
tanga ndio wamerudisha mida hii tokea asubuhi na tushazoea,kama kuna sehemu magufuli anahujumiwa na hili shirika bas ni tanga sijui sisi wananchi tunaotegemea umeme kujipatia riziki tukale wap
 
Back
Top Bottom