Hongera Tanasco

tungatagaga

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2024
Posts
708
Reaction score
955
Muda mrefu wananchi walikuwa wanatamani kupata huduma za ukweli na uwazi kutoka katika vyombo vya umma.Tanesco mnaonyesha kujali wateja wenu kwa kuwapa taarifa mapema za kukatika ummeme kwa sababu mbalimbali.Hii inasaidia wananchi kujiandaa katika shughuli zao na kutafuta njia mbadala kwa muda.
Ingependeza na Taasisi zingine kuiga mfano huu kwani inaonyesha kudhamini wateja.Si vibaya kuwambia wateja kwamba mto ruvu umekauka hivyo mtapata maji mvua zitakaponyesha
 
Habari ndugu mteja.

Asante kwa pongezi zako. Tunathamini mrejesho wako na tunaendelea kuboresha huduma zetu ili kutoa huduma kwa ufanisi zaidi. ^RS
 
Tanesco wako vizuri sana kwakweli...
 
Sasa muendelee ivo ivo

isije ikawa "mbuzi akisifiwa tembo hulitia maji"
 
Mi kwangu bado hawajafikia kiwango kizuri hasa wanavyokata umeme utasema wanaunguza vitu vyote .
Nakwanini wanakata ovyoo umeme kama leo wamekata umeme tokea asubuhi .
Eti wanapongezwa kwa lipi bado hawapo makini nakazi zao kuna muda luku haziingii kwenye tokeni.
Unakuta wanakata wapangaji hela ya pango.
 
Sasa muendelee ivo ivo

isije ikawa "mbuzi akisifiwa tembo hulitia maji"
Habari ndugu mteja.

Tunathamini sana mrejesho wako na tunaendelea kujitahidi kuboresha huduma zetu ili kutoa huduma kwa ufanisi zaidi.

Asante.^RS
 
Habari ndugu mteja.

Tafadhali elewa kuwa kukatika kwa umeme hakumaanishi kwamba TANESCO wamekata umeme kwa makusudi. Wakati mwingine, kukatika kwa umeme husababishwa na hitilafu za dharura ambazo zinahitaji kushughulikiwa haraka. Hivyo, tunalazimika kutatua changamoto hizo ili kuhakikisha kuwa huduma bora na endelevu inapatikana kwa wateja wetu. Asante. ^RS
 
Finally someone said it.

Kuna mtu/watu walianza kuimpact positive changes Tanesco toka kipindi fulani hadi sasa, Tanesco wana jitahidi sana. Isingekuwa miundombinu duni tungekuwa kama ulaya sa hivi. (La miundombinu duni bado)
 
Finally someone said it.

Kuna mtu/watu walianza kuimpact positive changes Tanesco toka kipindi hiko hadi sasa, Tanesco wana jitahidi sana. Isingekuwa muongo mbinu duni tungekuwa kama ulaya sa hivi. (La miundombinu duni bado)
Habari ndugu mteja.

Asante kwa pongezi zako. Tunathamini mrejesho wako na tunaendelea kuboresha huduma zetu ili kutoa huduma kwa ufanisi zaidi. ^RS
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…