Hongera sana Waziri Mkuu kwa yako hili

Mathanzua

JF-Expert Member
Jan 4, 2017
17,038
22,714
Kwa muda mrefu sana sisi wakulima tumekuwa wahanga wa ufugaji wa ndugu zetu Wamasai ambao hauzingatii sheria,utaalam na utu.Ilishakuwa kawaida kuona na kusikia vita kati ya Wamasai na Wafugaji na haikuwa ajabu tena kuona mkulima aliyekatwa kiungo, kuuwawa au kujeruhiwa kwa njia moja au nyingine na Mmasai.Hii ilishakuwa aibu ya CCM, Taifa na Watanzania kwa ujumla wao.

Jana Waziri Mkuu akiwa Gairo mkoani Morogoro alitoa tamko ambalo mimi nitaliita la kishujaa,kihistoria na kitaalam,kwamba sasa ufugaji ni lazima uzingatie uwezo wa eneo husika(carring capacity).Kwa mantiki hiyo alisema, itakuwa lazima sasa kwa kila mfugaji kuwa na eneo la kufugia mifugo yake linalolingana na wingi wa mifugo aliyo nayo,kama vile mkulima alivyo na shamba kwa ajili ya mazao yake. Mwishoni akawaagiza viongozi wa Vijiji, hasa Makatibu Watendaji wa Vijiji wakishirikiana na Maafisa Mifugo kusimamia agizo hili kwa umakini mkubwa.

Sisi wakulima tunaishukuru serikali kwa kubaini suluhisho la kudumu la mifarakano iliyo dumu kwa miaka mingi kati ya Wafugaji na Wakulima. Hata hivyo ni vema serikali ikatambua kwamba kubaini tatizo,na kutoa tamko ni sehemu tu ya utatuzi wa tatizo lenyewe.Ni lazima sasa serikali iweke mifumo ya kuhakikisha kwamba tamko hilo linatekelezeka.

Naomba nimalizie kwa kusema kwamba watendaji walio wengi katika ngazi ya Wilaya na Vijiji walikuwa wanafaidika sana na ufugaji holela wa ndugu zetu Wamasai, kwa hiyo watatumia kila mbinu chafu wakishirikiana na ndugu zetu Wamasai, kuhakikisha kwamba zoezi hili halifanikiwi.Kwa hiyo ni vema serikali ikawa makini.

Niseme pia kwamba katika hali ya kushangaza kabisa, yuko kiongozi mmoja aliyejitokeza na kusema kwamba mifarakano kati ya wakulima na wafugaji Wilayani Mvomero imekwisha, kwa hiyo wakulima Wilayani humo watavuna sana mazao.Napenda niseme wazi kwamba mifarakano ya wakulima na wafugaji Wilayani Mvomero bado IPO! Hata hivyo ni kweli kwamba wakulima Wilayani humo watavuna sana, lakini watavuna sana kwa sababu ya hali ya kuwa nzuri,si kwa sababu mifarakano imekwisha.
 
Huwezi kumnyonga mtu afu ukampa haki yake... Hii ni kauli ya walioshindwa
Hii ni lugha tu mkuu.Kunyonga hapa haina maana ya kuua.Inaweza kuwa hata ku-criticise.

Hata hivyo si vema kupinga kila jambo mkuu. Hivi unataka kuniambia kila jambo serikali ya JPM inalofanya ni baya.Si kweli,yapo mengi mazuri,pamoja na hili.Huu ni wivu tu ambao hautufikishi popote.Hii nchi ni yetu sote, kwa hiyo ni lazima tushirikiane wote kuijenga bila kujali itikadi zetu za kisiasa.

Hata hivyoo huzuiwi kutoa an alternative solution to the problem in question,kama kweli nia yako ni kujenga.Criticism tu haisaidii sana.
 
Back
Top Bottom