monde arabe
JF-Expert Member
- Oct 22, 2017
- 8,883
- 13,621
Habar za leo wanajukwaa,
Awali ya yote,naomba niwatake radhi wale ambao watakwazika kwa Uzi huu
Pia,naomba ieleweke kwamba;sijaleta Uzi huu wa kumpongeza Ndugu 'Ephraim Majinge' ili niweze kupata cheo vilevile sijauleta Uzi huu ili niweze kujipendekeza kwake
Ndugu zangu wanabodi na wanazuoni wote tuwe na tabia ya kuwapongeza au ku-appreciate mambo mazur wanayoyafanya wanadamu wenzetu ili na wao wazisikie pongezi hizo wangali hai ( simaanishi kuwa huyu Bwana Majinge ndyo amekaribia kuiaga Dunia...hapana kifo ni mipango ya Mungu hata mm naweza kutangulia baadae ndyo akafuatia yeye), kwa kuwa wakati mwingine mwanadamu anaweza kufanya jambo kubwa ambalo binadamu wengine hawawezi kulifanya na asitambue kuwa amefanya jambo jema mpaka hapo atakapo pongezwa
WHO IS EPHRAIM MAJINGE ( EPHRAIM MAJINGE NI NANI)
Huyu Bwana ni Afisa Elimu Msingi Wilaya ya Misungwi,na alianza kukitumikia cheo hicho cha Uafisa Elimu kwa ngazi ya Primary kati ya mwaka 2010 au 2011 mpaka hivi sasa
KWANINI NIMEAMUA KUMPONGEZA?
Bwana Majinge wakati alipopata cheo hiki cha Uafisa Elimu kwa ngazi ya Msingi,Shule nyingi za Msingi ktk Wilaya ya Missungwi zilikuwa na changamoto zifuatazo;
1.kuwepo kwa madai ya walimu ya muda mrefu
2.Walimu wengi hawakuwa wakifundisha au kuhudhuria vpnd vyao ipasavyo
3.Shule nyingi zilikuwa na migogoro na jamii hasa kwenye upande wa ardhi na ikafikia mahali wanajamii wakawa wanatishia kuwadhuru walimu ( mfano Shule ya Msingi Nyamayinza)
4.migogoro miongoni mwa walimu (hasa walimu wakuu na walimu waliokuwa chini yao kiutawala)
5.Walimu kuwa na matatizo ya kifamilia uliokuwa unasababisha kushuka kwa kiwango cha utendaji kazi
6.Baadhi ya walimu kupewa nafasi za upendeleo kama vile kusimamia na kusaisha mitihani
Jamaa baada ya kupewa cheo hicho,alianza kwa kuitisha vikao mbalimbali kwaajili ya kuwasikiliza walimu,kero zao na kupendekeza namna ya kuzitatua,nakumbuka kikao cha kwanza kwa kata ya Koromije kilifanyikia Koromije Shule ya Msingi na slogan ilikuwa inaitwa "FUNGUKA", Kiukweli walimu walifunguka matatizo mengi ambayo yalikuwa yakiikabili sekta ya Elimu Msingi kwa ngazi ya Wilaya,na kuanzia muda huo akaanza kuyafanyia kazi na hatimaye matunda yakaonekana kwenye matokeo...,hongera sana Bwana Majinge kwa hilo
Pia,najua anafanya kazi na watu wengi na wao wanahitaji kupongezwa kwa kutajwa majina,lkn hapa nitawataja baadhi tu ambao ni;
a)walimu wote wa shule za Msingi ktk Wilaya ya MISUNGWI
b)Nisa,Afisa vielelezo wilaya ( na huyu mtoto huwa ana macho mazuri sana,akikutazama ni kama anakupa kuponi ya kuingia peponi(jokes))
c)Magoti,Aligawesa,Maghembe, Ntalamuka na Eliud Mwaiteleke (Mkurugenzi)
Narudia tena hongera sana Ephraim Majinge kwa kazi nzuri inayoambatana na ubunifu
MSISITIZO:sijauleta Uzi huu ili niweze kupandshwa cheo au kujipendekeza ( kwanza najua hanifaham na hawezi nifaham hata kidogo kwa Id hii)
WITO WANGU KWA SERIKALI;kama kuna watu aina ya Majinge hapa nchini,basi wapewe priority ktk nafac za uongozi na hata katka utengenezaji wa sera za kitaifa,najua yapo mengi sana aliyoyafanya huyu Simba damu (jamaa ni shabiki sana wa simba FC),lakn yatosha kumpongeza kwa hayo machache niliyoyataja
Asanteni sana kwa kuusoma na kuutafakar Uzi huu!