Hongera Rais Kwa Kupambana na Uzembe

James Martin

JF-Expert Member
Apr 2, 2016
1,206
1,509
Kwanza napenda nimpe pongezi Mh. Rais kwa kanzi nzuri anayoifanya ya kupambana na rushwa, kuongeza ufanisi wa kazi kwa watumishi wa serikali na kuongeza mapato ya serikali kutokana na ukusanyaji wa kodi. Nakiri kwamba hivi vitu vyote anavyovifanya sikuvitegemea wakati alipokuwa anatoa ahadi zake mwaka jana wakati wa kampeni. Mimi nilikuwa upande wa upinzani na nilitaka Lowassa ashinde kwenye uchaguzi wa urais walau kwa kipindi kimoja. Si kwamba nilitegemea kwamba Lowassa angefanya kazi nzuri kuliko marais waliomtangulia, lakini nilitaka CCM wapate fundisho na wajue kwamba wananchi wamechoka na matatizo yanayoikabili nchi yetu kama umasikini, huduma duni za afya n.k.

Nikiwa Mtanzania niishie nje ya nchi kwa miaka mingi nilikata tamaa kwamba siku moja tutapata kiongozi ambae ataweza kutupa mwelekeo mpaka mwaka jana kwenye uchaguzi mkuu. Kitu kilichonifanya kurudisha moyo kwenye mambo ya nchi yetu ilikuwa ni kuona kwamba wapinzani walikuwa na nafasi nzuri ya kushinda kwenye uchaguzi wa urais. Ingawa kwenye kipindi cha kampeni nilikuwa nikisoma habari za Tanzania na kuongea na ndugu zangu waishio nchini kuhusu mambo aliyoyafanya Mh. Magufuli akiwa waziri lakini sikuamini kwamba angeweza kubadilisha mambo kwenye serikali ya CCM. Hata hivyo mambo aliyoanza kuyafanya yamenibadilisha mawazo. Moja ya kitu kikubwa ninachomsifu ni kupambana na UZEMBE.

Watanzania tuna asili ya uvivu. Kama unakaa ndani ya nchi ni vigumu kukiona hichi kitu kwasababu umezungukwa na mazingira hayo hayo. Nakumbuka nilivyoanza kufanya kazi huku Ulaya nilikuwa nikishangaa mkuu wa idara yetu alikuwa ni wa kwanza kufika kazini na wa mwisho kutoka wakati huko kwetu ni kinyume. Kitu cha kufanya siku moja Mtanzania itamchukua siku saba! Huu ni utamaduni ambao tumekua nao na itaweza kumchukua Magufuli hata vipindi vyote viwili vya urais kuubadilisha na atawachukiza watu wengi kwa jinsi anavyopambana nao lakini angalau tumepata sehemu ya kuanzia. Ki desturi mwanadamu huwa hapendi mabadiliko, lakini inahitajika mtu shupavu kubadilisha tabia za watu.
 
Ulilolizungumzia ni swala ambalo hata Rais aliligusia wakati wa kampeni akilitaja kwa jina la mchakato. Unakuta vitu ambavyo vinapaswa kufanyika kwa masaa machache ama siku moja,mtu analifanya liwe ni swala la kufuatilia kwa miezi au miaka kwa sababu tu imezoeleka kuwa uzembe na uvivu ni kama ustaarabu wa aina fulani hivi kwa maana ya kuwa,mtu hajihangaishi kushughulikia swala kwa dhati na uzalendo kwa vile tu ana uhakika na mshahara wake na ajira.
La msingi na ambalo Tunaliona katika maeneo mengi mpaka sasa,ni kuwa mambo ya kupotezeana muda yameanza kuondoka baada ya wahusika kuanza kujitumbua wenyewe baada ya kuona yanayowatokea wenzao.
Watanzania tunapaswa kujifunza kuwajibika bila kutegemea kusukumwa na mtu mkali mpaka tufikie kupata ulcers, BP na stress. Hata idadi ya watu wanaoumbuka sasa hivi ni ushahidi wa uozo ambao ulimea na kustawi katika maeneo mengi, ni kama vile kila mahali hakuna muadilifu kabisa katika safu fulani za uongozi mpaka inatia hasira ila kikubwa ni kuwa Tunakoelekea ni kuzuri maana Tutanyooshana tu.
 
Kwakweli hii kasi nimpya, nidhamu ya kazi iliyopotea kuanzia utawala Wa Mwinyi,mkapa mpaka kikwete ambapo watu ndiyo wamekua free zaidi fulu kujiachia imefika kikomo. Sasa maendeleo yatapatikana maana wizi unazimwa kazi zinawaka...shime tuungane na Rais kupiga kadi kiufanisi
 
..."Watanzania kwa asili ni wavivu..." sina hakika sana na hiyo, unaweza kuwa ume-overgeneralize.
 
Back
Top Bottom