Hongera Prof. Kitila Mkumbo

Hongera Prof. Kitila Mkumbo

lulumba

Member
Joined
Mar 23, 2014
Posts
60
Reaction score
67
Ulivyoanza kuandika ama kuchambua kuhusu habari za urais 2015 katika gazeti la kila Jumatano la Raia Mwema hasa sifa za rais ajaye, basi niliona ni yale yale ya kina fulani na wengineo za kututajia sifa za raisi ajaye lakini yanapotokea mambo makubwa na muhimu kwa Taifa hatusikii na wala hawasemi lolote mpaka yanapita. Swala nyeti la mchakato wa katiba mpya hatukusikia misimamo wala mitazamo yao japo kulikuwa na mambo mengi ya ajabu ajabu yaliyohitaji kuonya ama kukemewa kabisa, maswala uwekezaji tata katika rasilimali zetu, kutungwa kwa sheria mbaya na tata na bunge letu hata kusainiwa na Raisi kiushabiki wa kichama lakini huwezi kusikia lolote hata likiwa wazi ni baya na lina ukakasi mwingi; Kina fulani hawa na wengineo hawasemagi lolote wakati michango yao ikihitajika kwa namna jinsi jamii inavyowaheshimu na kuonekana kama ni watu muhimu katika Taifa hili. Lakini hili urais 2015 wanalisema utafikiri uzalendo unapimwa kwa kutaja sifa za rais ajaye.

Nilijua sasa waja na hadithi zile zile tofauti ni msimuliaji tu. Lakini tangu nianze kusoma makala za Prof. Mkumbo Kitila zimenivutia na zimenisaidia kuwafahamu watarajiwa mbalimbali, sio kwa sifa tu hata udhaifu wao, fursa kwa kila mmojawao na tutarajie nini toka kwao. Ni uchambuzi mzuri nafikiri una faida kwa watanzania na hata wahusika wenyewe. Kwa jinsi unavyowakilisha hata wahusika wanaweza wakakupa ushirikiano mzuri katika maandalizi ya makala hizo, sio kwamba uwapendelee bali wakuwezeshe kuandika kiuhalisia zaidi.

Kwa kweli ni kitu cha pekee kinachoweza kufanywa na mtu pekee. Ni uzalendo na huduma ya kizalendo kwa Taifa lako. Hongera, nafikiri watanzania watajivunia uwepo wako kama mtanzania.
 
Kama umekosa mtu wa kumpa sifa bora umsifie mmeo! Au prof kitila ni mumeo
 
Mh. Jamii forum sasa ni mahali pa mitusi tu? Hoja huondolewa kwa hoja sio matusi ndugu zangu be patient tuwe wema.
 
Back
Top Bottom