Polisi walishakamilisha ushahidi ndio maana wakasomewa maahtaka. Watu wamechoshwa na haya mambo bwana.. hakuna sheria ya dini wala ya nchi yetu inayoruhusu mtu kumuua mtu mwingine. Mimi niko moshi hii kesi imevuta watu wengi sana na ndicho kilichonifanya hata mimi kufika. Juzi kesi ilisomwa chumbani polisi walisema walifanya hivyo kiusalama na walihofia wingi wa watu. Waliingizwa watu wachache akiwemo mama na baba ake msuya na kaka mwingine waliyesema mtoto wa baba mkubwa. Baada ya yule mama kuwaona watuhumiwa alizimia ikalazimu police wate familia yake iliyokua nje kwa msaada, hapo ndipo ikaanza tafrani na waandishi wa habari watoto wanalia mama kazimia waandishi wako busy kuwapiga picha hawakutaka kuona hicho kitendo. Wakasema wa naumia kuwaona watu waliomuua ndugu yao halafu waandishi waliwahi kuandika kua ndugu wa marehem wazimia baada ya kesi kuhairiswa, wakahoji kwani wao hawajui kua hii kesi ni lazima ihairiswe? Alikua analalamika ndugu mmoja wa familia.