Hongera Mh.William Vangimembe Lukuvi

Hongera Mh.William Vangimembe Lukuvi

[/B][/COLOR]
Isingekuwa sera nzuri ya CCM hata hiyo lugha ya mkoloni uliyotumia kuweka msisistizo usingeijua..tatizo lenu CHADEMA imewapandikiza chuki kiasi mnaona kama CCM haijafanya lolote...wewe unajua maendeleo ya Jimbo la ISAMAN yaliyoletwa na Ccm au unabisha tu
Ukitaja Isman, namkumbuka Kulak mkuu ustaadh Mwamwindi!
 
jamaa mpuuzi kwel, tena nahc we ndo yule tapel unayetumia jina la lukuvi kutapel na sasa unajisafisha kwa kumsifia. Usiwe kama Chris Lukosi anayejipendekeza ccm kwa kujifanya anaisifia kwenye mitandao huku akilenga kuitwa apewe nafasi fulan wakata lumumba pameshajaa, ye arudi uingereza akauze magazeti kazi aliyokuwa anaifanya awali.
 
ahaa kumbe yule fisadi wa elimu duh anatisha jamaa kwa kufoji vyeti aiseee
 
Tena mkuu ni mikutano isiyo na tija kaka....wala hajuna maendeleo,yeye ni kutoa Quotation za kwenye biblia,sisi tunataka maendeleo kama ya Wenzetu wa ISIMAN...NJOO KAKA NJOO TUKUPE JIMBO,MCHUNGAJAI MSIGWA ARUDI KANISANI...TUMEMCHOKA

Hata Msigwa amesikia kuwa Iringa mjini kuna watu wawili (mmoja yuko UK) wamemchoka......
 
Kweli mkuu,
Huyu anapanda jukwaani kuhubiri badala ya kuwaeleza wanachi anafanya nini bungeni.
Nimeona video yake juzi anasema eti wananchi wa Iringa wanapenda vurugu, huu ni utoto, wananchi wanataka maendeleo na utatuzi wa kero zinazowasumnbua miaka nenda rudi. haya mambo ya vifungu vya biblia kanisani sio jukwaani.
Halafu kuna mchango nilimkabidhi aakmpatie mjane wa Mwangosi sijapata taarifa kama zile hela zilifika

Hiyo miaka nenda rudi yeye ndio amekuwepo hapo? Tukiwaambia what have you done in 50 yrs mnasema "Rome was not built in a day" leo unaanza kulia na mtu mwenye only 3 yrs....mtahangaika sana but hakuna chenu...you will always be the best second!
 
Wacha uongo wako. Katika majimbo ya Iringa Isimani ndo jimbo maskini zaidi. Wadanganye walio mbali. Nakuambia kama atacheza fair play hata wana ccm wenyewe wanampiga chini kura za maoni.

Mie nilipita hapo kipindi wana janga la njaa...leo wanajifanya kusahau....huyu jamaa aliepost bila shaka ndiye yule aliekamatwa anajiita mtoto wa Lukuvi....anaanza kujipendekeza taratibu ili familia imtambue kwa mchango wake!
 
Naona hii thread imejaa magamba yanapongezana ujinga tu..ivi Ismani kuna maendeleo gani hamna umeme wala maji? Wanakijiji wanaamka usiku wa manane kutafuta maji mnatuambia nini? Ivi ww chris lukosi upo nje unajua wananchi wa Isman shida zao au unaropoka tu..
 
unabandika mada kwa I'd ya Ngaliba Dume.

unaanza kuchangia mwenyewe kwa I'd kinyanambo huu si ujinga unamdanganya nani.?

Mkuu Invisible tunashukuru kwa kuwaumbua watu kama hawa.!!!!
 
nimeamua kuingia muda huu wa sherehe za muungano kujibu uwongo wa ngaliba dume kama raia wa tz. Ni uwongo usio wa kifani kuhusu lukuvi ni kwamba wakati anaingia isimani kulikuwa hakuna njaa lakini sasa njaa kila mwaka, kulikuwa na maji sasa wananchi wanahangaika sana na maji, inawezekana ngaliba dume yupo dar na si isimani au iringa. Kiukweli maeneo yote ambao anasema anapendwa ni kwamba hawamtaki hata kumwona kama akitaka basi ajaribu kugombea 2015 , hatapita hata kwa uchawi, kiukweli mwaka 2010 dr. Kapwani alijichanganya mwenyewe kwa maana alipokea rushwa kwa lukuvi ili asirudishe fomu na akafanikiwa lakini asingejichanya kapwani angekuwa mbunge wao. Kijana ngaliba dume jihadhari kuwa tambala la deki kwa vile baada ya kazi yote hufichwa , hivi unalipwa tshs ngapi. Nikuulize hiyo unayosema lami hivi kweli lukuvi alate lami? .ungesema kikwete ningesema sawa kwa sababu hiyo ni miradi ya serikali, kwa sababu sio kweli kuwa mfano lamii zinazojengwa moshi au hai ni mbowe au ndesa? Hapani mbowe mwenyewe alimkiri jk kuwa kweli anafanyakazi kuhusu barabara za lami. Nadhani ngaliba dume umelipwa ua una mtindio maana siwwezi kuamini sifa unazompa ambazo hata hivyo hazipo jifunze kutafuta chako, hivyo visendi vya wanasiasa siku moja vitakutokea puani. Usamehewe bure shame on you. kuhusu huko mbungeni ni mtazamo tu , ukiwa unapenda udikiteta utamsifu lakini pia kama ndio wajibuwake hakuna atakayemlaumu ila kuhusu jimboni kwake kule hali mbaya .
 
Yaani kweli njaa mbaya jamani. Hivi mtu kama huyu anatungiwa urongo huu na bila aibu anakwenda post JF, analipwa buku mbili na anarudi nyumbani kifua mbele kuwa katoka kazini na watoto wanaimba ...baba huyooo katoka kazini, na debe la ulanzi...!!!

Nakuhakikishia sera hizi za urongo na ushuzi hazitawasaidia kamwe !! Muda wa kuwaongopea wananchi kwa uji, pombe, kofia na eti nitamleta rais wakati wowote ect umepitwa ...!!

Huyu kwanza kihiyo...hana cheti chochote halali zaidi ya kuwa kiongozi wa chipukizi na umoja wa vijana ! Pili, hili jimbo bado ni moja ya top 3 majimbo duni na masikini kuliko yote duniani !!

Tatu, wewe hata hujui au umeambiwa tu nenda ka-post lakini sisi wananchi tunajua ukweli na hatutachoka kuwaumbua !!

Yaani nimeshikwa tumbo la uharo kusoma ----- huu...Msigwa si alinunuliwa tangu enzi ya NCCR Mageuzi...unataka tukupe jina la nani ali donate kale kagari..? Je mbona husemi kuwa jamaa alikuwa hata nyumba hana kwao, ikabidi ajengewe chap chap pale kwa mapogoro...ambako ndiyo makao makuu ya usangoma wote...!!
Na uongo wa kila siku kuwa yeye ndo analeta wazungu wa miradi yote unadhani sasa wananchi hawajui kuwa miradi inakuja kirahisi sababu ya umasikini wa eneo hili...!!!!

je, unataka asifiwe bila hata aibu ya usangoma wa kuchoma moto ile shule ya sekondari-mabweni na kuua watoto wa watu..!! Mbona tunajua ...yaliyotokea idodi...!!

Na mbinu mpya ya kuwatuliza vijana machachari wa ndani ya CCM ambao walikuwa tayari wanaongoza hata kura za maoni, mkaishia kuwalilia weee na kuwahonga mapesa, na sasa wengine mmewapa U DC kuwatuliza na kuwatupa kusini lakini bado haisaidii utashangaa siku moja...!!

Mama Mbega....lol alifanya nini haswa cha kuwaongopea watu na alipigwa chini kwa sababu gani..?? Wale waarabu wenu majangili wa tembo wooote na michango yooote na kugawa mafuta lakini bado mlipigwa chini, na unadhani leo hii ndo ataweza huyu fisadi ambaye mambo yake tunayajua na biashara zake hata CAG alishashtuka..!!!

Tutawang'oa ulimi nyie kimbieni na kucha... !!!

Ha ha ha mleteni huyu fisadi Lukosi, tena huyu kazi itakuwa rahisi sana


Nikiwa kama mdau wa siasa za Iringa,naomba nichukue nafasi hii kumpongeza Mh.Lukuvi kwa juhudi zote anazozifanya katika Bunge la JMT...Akiwa kama Mnadhimu kwa upande wa Serikali,ameonyesha kuimudu vyema sana nafasi hiyo,amecontrol jazba na nidhamu ya wabunge wa upande mwingine,ameonyesha weledi mkubwa wa hekima na busara akitofautiana na mnadhimu wa upande wa pili
Kama umelifuatilia Bunge utakubaliana na mimi kuwa huyu Mh. ameonyesha kujua sana kanuni za bunge,kujenga hoja na kujibu miongozo na hoja ya wabunge wanaokurupuka...hakika Vangimembe unawakilisha...bila unadhimu wako Bunge lingetawaliwa na wahuni wanataka kumtukana Rais hata billa sababu...
Kwa wanaofuatilia siasa za Iringa Jimbo la MH.LUKUVI haliwahi kuguswa na upinzani sbb ISIMANI watu wanaipenda CCM na CCM imewafanyia mambo mengi sana,hata DR KAPWANI alipojaribu kugombea kwa tiketi ya CHADEMA allishia kukimbia dakika za mwisho mana wana ISIMAN walimwambia hana chake na CHADEMA yake,wao wako na LUKUVI toka 1995 na wameahidi tena kumpa 2015...
Nenda Pawaga,Idodi,Lwang'a,Izazi mpaka Migoli..huku kote ni maendeleo ya CCM na MH.LUKUVI..Ameleta maji na sasa barabara inajengwa kwa kiwango cha lami toka Iringa-Lwang'a-Izazi-Migoli hadi Dodoma...Siasa safi na maendeleo aliyoleta Mh.LUKUVI yamefanya CHADEMA wasikanyaga kabisa ktk Jimbo la ISIMAN mana hakuna watalaosema,ndio maana ktk mkoa wa Iringa ndo Jimbo pekee ambalo si Mbowe wala Padre Slaa aliwahi kukanyaga,mana wanajua hawana chao,hata pale Iringa mjini ni vile Mama Mbega hakuwa chaguo lao..wao walimtaka Mwakalebela..2015 Mchungaji Msigwa atarudi kwenye mradi wake wa kanisa,wana Iringa hawahitaji tena siasa za maandamano bila maendeleo.
Jimbo la Isimani litaendelea kuwa mikononi mwa CCM sbb ya maendeleo walioletewa na CHAMA CHA MAPINDUZI
..HONGERA SANA WILLIAM VANGIMEMBE MWALUKUVI :yo::second:
 
Tumekupata mkuu
 

Attachments

  • uploadfromtaptalk1366980168988.jpg
    uploadfromtaptalk1366980168988.jpg
    22.5 KB · Views: 46
mi nimeambiwa jimbo la isimani lipo wazi. Halina mbunge huyo lukuvi ni kihiyo. Kiujumla hajawahi kusoma sekondari hata drs moja lakini cha kushangaza ana eti masters. Dawa yake inachemka tuonane
 
Wacha uongo wako. Katika majimbo ya Iringa Isimani ndo jimbo maskini zaidi. Wadanganye walio mbali. Nakuambia kama atacheza fair play hata wana ccm wenyewe wanampiga chini kura za maoni.

Kama anafanya vizuri acha wamsifu kwani aisifuye mvua, imemnyea. Lakini kama ni propaganda za siasa itakuwa very unfortunate. Lakini watu wajifunze na waelewe kuwa upinzani siyo uadui bali ni uwajibishanaji. Cha kushangaza wako watu wamelishwa sumu na wamekubali kuwa upinzani ni uadui. Cha kusikitisha pia ni kwamba baadhi ya hawa watu ni wasomi wazuri ila wamekataa kabisa kutumia akili zao na badala yake wameamuwa kushabikia hata upuzi kabisa. Where are we heading to?
 
Back
Top Bottom