Hongera Manispaa Kinondoni Kwa Ujenzi Wa Barabara Za Makumbusho Lakini....

shujaa6

Member
Nov 18, 2016
11
1
Habari Zenyu Waungwana,
Kuna Ujenzi Unaendelea Wa Barabara Za Ndani Ktk Eneo La Makumbusho Kurahisisha Uingiaji Wa Mabasi Kwenye Kituo Cha Makumbusho Ni Jambo Jema, Ila Kabla Hawajafika Mbali Na Kazi Hiyo Naomba Nishauri Wazingatie Kuweka Maeneo Huru Ya Watembea Kwa Miguu Ili Kuepusha Watu Kugongwa Na Magari. Kwakuwa Kasi Ya Magari Sasa Itaongezeka. Waige Mfano Wa Strabag Waliojenga Barabara Za Mwendokasi Jinsi Walivyotenga Njia Za Watembea Kwa Miguu Kiasi Wameweka Nguzo Ili Kuzuia Magari. Usalama Kwanza Hatutaki Ajali Tunataka Kuishi. Naomba Mwenye Maoni Au Ushauri Tuutoe Kwa Hawa Wakandarasi.
 
Hivi mkuu barabara ilivo nyembamba vile litapatika eneo LA watembea kwa miguu?
 
Hivi mkuu barabara ilivo nyembamba vile litapatika eneo LA watembea kwa miguu?
Ni ujinga na ushenzi wa hali ya juu kujenga barabara za mjini bila kuweka sehemu za waenda kwa miguu! Barabara nyingi Dar zimejengwa bila kujali sehemu za waenda kwa miguu! Watapaa? Wana mabawa? Waafrika bado kabisa ufahamu wetu uko sawa na wa manyani.
 
Ili kupata eneo la watembea kwa miguu itabidi watu wabomolewe nyumba zao. Watu wakishabomolewa tutakuja tena kulalamika.
 
Ni kweli kabisa.. wewe unayeuliza kama kuna sehemu ya kuweka njia za waenda kwa miguu.. jiulize kama wamepata sehemu ya kuweka mitaro ya maji kwa nini hiyo mitaro isiwekewe pavement kwa juu kuwa sehemu ya waenda kwa miguu..

Barabara nyingi zina mitaro mikubwa bila ya sababu na mingi inaishia kuwa majalala ya takataka.. angalia barabara za Stabag za mwendokasi zote mitaro ipo ndani kwa ndani, kwa nini wasiige kwenye barabara nyingine?
 
Back
Top Bottom