Hongera Maalim Seif / Lipumba lakini.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hongera Maalim Seif / Lipumba lakini..

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pope, Feb 28, 2009.

 1. Pope

  Pope Senior Member

  #1
  Feb 28, 2009
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 117
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Napenda kuchukua nafasi hii kuwapongeza Viongozi wa CUF Maalim Seif na Ibrahim Lipumba kwa ushindi wao wa kishindo katika uchaguzi uliopita majuzi ndani ya chama hico.
  Binafsi nimeshtushwa na ushindi huo si kwamba nilitazamia waangushwe la hasha kwani kushinda kwa asilimia 98.6 kwa Lipumba na asilimia 99.5 kwa Seif si mchezo hasa kwa siasa tata za nchi zetu.
  Mgombea Abdallah Safari ambaye alikuwa akigombea nafasi hiyo ya Maalim Seif alipata kura 6 sawa na asilimia 0.9, kilichonipelekea kuandika hapa ni huyu Bwana Safari. Kama mnakumbuka Prof, Safari alipoteza kazi yake Serikalini kwa sababu ya CUP, akiwa ni mtumishi wa Serikali ndani ya Wizara ya MAmbo ya Nje, Chuo Cha Diplomasia kama Mkurugenzi wa Mipango na MAsomo na wakati huo huo akiwa anatumiakia Professional yake kama wakil Prof Safari aliwatetea CUF ambapo washtakiwa Lipumba a Seif walishinda na malumbano hayo yalipelekea yeye kupoteza ajira,
  Swali langu je kweli CUF wameshindwa kuona uchungu wa Prof Safari kwa Chama hiki, maana nina imani Uongozi anaweza, Je Zimwi la Serikali bado linamuandama?

  Wabbillah Tawfiq
   
 2. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #2
  Feb 28, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Sasa kama ni wakili bora abakie huko huko ,siasa si lelemama ,na huwezi kujua jamaa alikurupuka tu na kutaka kugombea uwenyekiti ,lazima wazee wa busara washituke,unajua kuingia kwenye timu inabidi uwaze mazoezi na timu,toka unawekwa kando mpaka unazogezwa kwenye benchi mpaka unaambiwa angalia wenzako,mpaka unawekwa risavu mpaka unachezeshwa mechi za majaribio na baadae unapata namba ya kudumu ndani ya timu ,Safari hakuiweza safari alitaka adandie moja kwa moja ,lazima patakuwa pagumu hapo na ni tabu sana wanaopiga kura kushawishika na la ajabu jamaa baada ya kushindwa anazindua kitabu cha matatizo ndani ya CUF ,jamani si angelisuburi japo mwezi.
   
 3. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #3
  Feb 28, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Demokrasia kweli..yaani mtu anapata 98%? Amekuwa Nguema wa Guinea ya Ikweta?

  CUF hakuna wengine wanaoaminika licha ya Lipumba na Seif?

  Afadhali hata demokrasia ndani ya CCM!
   
 4. Pope

  Pope Senior Member

  #4
  Feb 28, 2009
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 117
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndio maana nilidhani labda huyu angewezakuleta kaupinzani kidogo na kwa uzito alionao na kwa jinsi alivyojitolea kwenye chama kwa mtaji huu basi Maalim Seif na Lipumba watatawala mpaka ....
   
 5. p

  p53 JF-Expert Member

  #5
  Feb 28, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 613
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  uchaguzi siku zote ni maandalizi.kama una nia ya kugombea nafasi fulani lazima ufanye maandalizi ya kutosha.siasa ni zaidi ya kiwango chako cha elimu,status yako nk.sasa unapokurupuka from no where then ukataka kugombea nafasi fulani tena ya juu na nyeti tena unagombea na mtetezi wa hiyo nafasi aliyekwisha jiwekea mizizi tayari,anayejulikana vizuri na wapiga kura na ukategemea kushinda kiulaini kwavile ulisimamia kesi ya chama,ukija kukosa hata kura ya mkeo usimlaumu mtu!
   
 6. k

  kanda2 JF-Expert Member

  #6
  Mar 1, 2009
  Joined: Apr 22, 2007
  Messages: 1,318
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Maswali aliyoulizwa na Mheshimiwa Hamad Rashid yalilenga kumwangusha kwa wapiga kura.Professor Safari labda kapanda gari bila kujua gari hilo linaelekea wapi?Tuwe makini na vyama vya siasa vingine vina wenyewe!
   
 7. Pope

  Pope Senior Member

  #7
  Mar 1, 2009
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 117
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sasa hapo ndipo maswali yanapokuja, simtetei Safari ila najaribu kufikira Je CUF hakuna wengine wa kuongoza hili JAhazi zaidi ya LIPUMBA NA SEIF? nafikiri kimsingi watu wameshajaribu kugombea zaidi ya mara 2 hata kama kura ziliibwa nafikiri ingeleta chachu kama wangewapisha watu wengine nao wajaribu.
   
 8. K

  Kwaminchi Senior Member

  #8
  Mar 1, 2009
  Joined: Dec 30, 2007
  Messages: 154
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwani wenye uchungu wa chama ni wale wanaogombea uongozi wa chama tu?
  Wale wanaopiga kura nao wana uchungu wa chama chao pia. Na wao ndio wenye uwezo wa kumchagua wanayemtaka awaongoze kwa njia ya kura zao.

  Kwa nini maamuzi ya wapiga kura nayo yasiheshimiwe?
   
Loading...