kalulukalunde
JF-Expert Member
- May 27, 2016
- 1,056
- 1,083
Katika kipindi cha takribani mwezi mmoja sasa, nchi yetu imekumbwa na matukio ya kihalifu yaliyosababisha vifo vya takribani watu 20.
Katika nchi ambayo imekuwa ikijulikana kama kisiwa cha amani na utulivu, haya ni matukio ya kuogofya na yanayoanza kuuliza maswali kuhusu nini hasa kinaendelea hapa nchini.
Hata hivyo, ni wakati sasa wa kuvipongeza vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kutokana na kazi kubwa wanayoifanya hivi sasa.
Katika siku chache tulizopata, tumeshuhudia askari wetu wakipambana na wahalifu hao katika mazingira ya hatari yanayoweka rehani maisha yao.
Ni rahisi kusema kwamba vyombo hivyo vinafanya kazi yao. Lakini, umefika wakati kufahamu kwamba wenzetu hawa wanahatarisha maisha yao kwa ajili ya kutuwezesha akina sisi kuendelea na kazi zetu za kila siku.
Mara nyingi, ni rahisi kwa wananchi kutoa lawama dhidi ya vyombo vya dola kwasababu yoyote ile. Sababu kubwa ni hiba (legacy) iliyojengwa na vyombo hivyo wakati wa ukoloni ambayo bado haijafutika.
Ingawa bado baadhi ya wahusika katika vyombo hivyo hawajabadilika vya kutosha, ukweli ni kwamba kuna mabadiliko makubwa kati ya vyombo hivyo wakati wa wakoloni na sasa.
Ndiyo maana, tunaona ni vema kuvipongeza vyombo hivi na kuvitia shime katika wakati huu ambapo tunaona taifa linatikiswa na maadui na wao ndiyo wenye uwezo na mbinu za kupambana na hali hii.
Katika namna ya kipekee kabisa, tungependa kushauri Watanzania wenzetu kwamba katika kipindi hiki ni muhimu sana kutoa ushirikiano na kutiana shime na vyombo vyetu hivi ili viweze kutimiza majukumu yake ipasavyo.
Katika hili, ni muhimu kusema kwamba hatushawishi watu wasifie hata pale ambapo kunaonekana kuna matatizo au makosa yanayotakiwa kurekebishwa. Tunachosisitiza ni kutoa lawama pale ambapo kuna ushahidi wa kutosha na usio na shaka.
Kwenye dunia hii ya sasa ya utandawazi, kuna wakati tukio moja linaweza kuwa linahusiana na lingine mbali kabisa kutoka hapa kwetu. Ni muhimu kuwa waangalifu katika kutoa shutuma au lawama katika mambo ambayo hatuyafahamu vizuri.
Sasa ni wakati wa kuviruhusu vyombo vyetu vifanye kazi ya kulinda watu wetu na mali zao na sisi kutoa kila aina ya ushirikiano; katika namna, hali na wakati wowote itakapohitajika.
Chanzo: Raia Mwema