Hongera Kikwete, ni watu wachache tu ndiyo watakuelewa juu ya Usuluhishi na Kagame

Lukolo

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
5,143
3,196
Mwanzoni mwa mwezi huu nilileta hapa post ya kupendekeza Kikwete azungumze na Kagame ili wayamalize. Wapo wanaona mbali, waliisifia post ile na wapo wanaoona karibu walinitusi, kunikejeli na hata kuniita Mnyarwanda. Sasa Kikwete amesikiliza pendekezo langu, na hapa chini ni uthibitisho. Tena amefanya kama nilivyopendekeza. Sijaediti ile post, ipo kama nilivyoiweka. https://www.jamiiforums.com/jamii-intelligence/499266-kikwete-zungumza-na-kagame.html

Ni lazima nitamke kwa herufi kuu kwamba Kikwete hapa ameonyesha uanadiplomasia wa hali ya juu. Hajataka kuonyesha umwamba kama ambavyo Kagame anafanya, ameamua kushuka kwa faida ya nchi yetu na watu wake. Hii ni credit kubwa sana kwa Kikwete, katika hili, Kagame anaonekana ni bonge ya kubwa jinga.

Kwa dhati ya moyo wangu nakupongeza sana Rais wangu. Japo sikubaliani na wewe katika masuala mengi ya kiuongozi, lakini najivuna kuwa na rais mwenye hekima kiasi hiki. Big Up Kikwete.

----------------------------

Mada - The Tanzanian government has reached out to President Museveni to help mediate in its simmering row with Rwanda

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...hisha-mgogoro-kati-ya-tanzania-na-rwanda.html
 
kwa hiyo yakiisha wale wa mtukula wataruhusiwa kurudi walikokuwa ? maana naona kama JK ali-panic kwa maamuzi yale.
 
kwa hiyo yakiisha wale wa mtukula wataruhusiwa kurudi walikokuwa ? maana naona kama JK ali-panic kwa maamuzi yale.
Sina uhakika kama wale walitimuliwa kutokana na mgogoro wa Kikwete na Kagame. Wale walitimuliwa kutokana na kukithiri kwa ujambazi.
 
Kwanza naungana na Mh Kikwete kwakuamua kutatua mgogoro huu kidiplomasia,

Lakini nimefedheheshwa sana na pendekezo la kumuomba Mseveni kuwa msuluhishi wa mgogoro huu,

Kwasababu kuu mbili,

1) Mseveni ni mbia wa mkataba wa Lemera wa kuigawa kongo uliosainiwa vilima vya virunga kaskazini mwa Goma Lemera kati ya Paul Kagame, Yoweri Mseveni na Laurent Kabila, hivyo anamaslahi kwa Kagame,

2) Vita vya M23 na Jeshi la serikali ya Kongo ambako UN imepeleka majeshi yake huko ndani ya Bataliani 1 ya JWTZ ni kuwa Kagame na Mseveni wanahusika kwa asilimia 100,

Ripoti ya CIA na UN mwezi jana imethibitisha pasina shaka kuwa Uganda na Rwanda zinawafadhiri waasi wa M23 ambao 90% ni Wanyarwanda, mpaka hapo Mseveni ana maslahi na mgogoro wa Kongo ambao ndio chimbuko la mgogoro wa Tanzania na Rwanda,

Kumbuka juzi tumempoteza mwanajeshi wetu aliyeshambuliwa kwa kombora la M23,
Jana majeshi ya UN yamepambana uso kwa uso na majeshi ya Rwanda yaliyovuka mpaka kwenda Kongo kwa sababu ambazo Rwanda haijatoa ufafanuzi stahiki,

Binafsi napinga Mseven kuwa msuluhishi wa mgogoro huu,

Tanzania itafute mtu mwingine na sio huyu!

Mzee Kibaki yupo, na tunaweza kuangaza mtu mwingine kusini mwa jangwa la sahara lakini sio Mseveni!
 
Kwanza naungana na Mh Kikwete kwa dhana ya kutatua "migogoro" kidiplomasia,

Lakini nimefedheheshwa sana na pendekezo la kumuomba Mseveni kuwa msuluhishi wa mgogoro huu,

Mgogoro wa Rwanda na Tanzania hauhitaji Tanzania tuombe suluhu,

Hii ni fedheha kwa taifa letu huru kwasababu kuu mbili,

1) Mseveni ni mbia wa mkataba wa Lemera wa kuigawa na kuiuza Kongo uliosainiwa vilima vya virunga Kaskazini Mashariki mwa Goma Lemera kati ya Paul Kagame, Yoweri Mseveni na Laurent Kabila, hivyo Mseveni anamaslahi kwa Kagame hawezi kuwa refa wa haki kwa hili,

2) Vita vya M23 na Jeshi la serikali ya Kongo ambako UN imepeleka majeshi yake huko (Tz na SA) Tanzania ikipeleka Bataliani 1 ya JWTZ ni kuwa Kagame na Mseveni wanahusika kwa asilimia 100,

Ripoti ya CIA,UN,HRW na nyaraka za kijasusi za Tanzania zimethibitisha pasina shaka kuwa Uganda na Rwanda zinawafadhiri waasi wa M23 ambao 90% ni Wanyarwanda kwa malengo ya kuiba raslimali za Kongo,

Mpaka hapo Mseveni ana maslahi na mgogoro wa Kongo ambao ndio chimbuko la mgogoro wa Tanzania na Rwanda, Hivyo hawezi kuwa refa wa haki kwa hili.

Ikumbukwe juzi 28/8/2013 tumempoteza mwanajeshi wetu (Meja) aliyeshambuliwa kwa kombora la M23,

29/8/2013 majeshi ya UN yamepamba uso kwa uso na majeshi ya Rwanda yaliyovuka mpaka kwenda Kongo kwa sababu ambazo Rwanda haijatoa ufafanuzi stahiki,
Inatia simanzi kuona serikali inapiga magoti na kusulubiwa bila kosa na Kagame,

Binafsi napinga Tz kuomba suluhu na zaidi napinga Mseven kuwa msuluhishi wa mgogoro huu,

Tanzania ibaki na msimamo wake kuwa haikumkosea Kagame,

Rais wangu acha ukigeugeu unatutesa watanzania tunaoamini na kusimamia imani ya nchi yetu takatifu tuliyopewa na Alha,

Kagame mambo yakizidi unga yeye ndie anatakiwa kuomba suluhu, na msuluhishi asiwe Mseveni!

Sisi ni Taifa huru na lenye nguvu Afrika Mashariki na Kati,

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika
 
kwanini usuluhishi?Acha kigeugeu,nye ndo wanasiasa wanaofuata upepo wa siasa unakoelekea halafu mnajiita wanamapindunzi na wanaharakati.
We nani asiyekujua humu unaunga mkono wanajeshi kupelekwa kongo leo unakuja tena kwa unafki eti naungana na kikwete kutatua mgogoro kwa njia ya kidiplomasia.
 
Nashindwa kuielewa Tanzania. Nashindwa kuwaelewa watu wanaomshauri Rais Kikwete, nashindwa kabisa. Kwa nini wamfuate Yoweli Museveni? kwa nini wakati huu? mambo mengine ni kama kulifedhehesha Taifa lenu. Maswali haya yamepata majibu? ya Kwanini wamewatenga? wameimega Africa Mashariki tayari halafu unawafuata kuomba msamaha kwa nini? ni mgogoro wa nchi mbili unahusianaje na kuigawa East Africa? na kwanini Kagame yuko na Kenya, Uganda, Burundi, na Tanzania kuachwa inje? mimi nashindwa kuelewa mawazo ya serikali ya Tanzania, nashindwa kuwaelewa kabisa. Nitaanza kuamini kuwa kuna zaidi ya sababu kuliko ya ushauri iliyofanya wakosane. Wangesema tagu mwanzo. kwani Taifa ni la watu wote na si nchi ya mtu Fulani na akawa anaendesha kama shamba lake na anavyopenda. DUH!! kwa nini kudanganya uma? Hata Mkapa asingefanya hivyo. Mambo ya kushangaza sana.!!

Inasikitisha na inakera sana
 
kwanini usuluhishi?Acha kigeugeu,nye ndo wanasiasa wanaofuata upepo wa siasa unakoelekea halafu mnajiita wanamapindunzi na wanaharakati.
We nani asiyekujua humu unaunga mkono wanajeshi kupelekwa kongo leo unakuja tena kwa unafki eti naungana na kikwete kutatua mgogoro kwa njia ya kidiplomasia.
Mimi ni mhafidhina wa Tanzania,

Imani yangu ipo palepale kuwa Rwanda hawastahili suluhu na Tanzania,

Jeshi letu linawajibika kwa ngazi ya kimataifa kuwakomboa wakongomani,
 
Mchawi mpe mtoto akulelee, naona ni Mseveni ni uchaguzi sahihi ili akalikoroge na mshirika wake
 
msimamo wako haujaeleweka bado

Nimetaja kumuunga mkono rais katika dhana ya kutatua "migogoro" kidiplomasia,

Lakini nimeutenga mgogoro huu kuwa Tanzania hatutahili kuomba usuluhishi wa kidiplomasia na Rwanda kwakuwa hatujaikosea Rwanda,

Ikiwa kuna lolote anaetakiwa kusaka suluhu ni PK
 
Yericko,'
Huu si ugomvi kati ya Tanzania na Rwanda. Ni kutokuwepo personal maelewano baina ya Kikwete na Kagame.
That being the case, the only person who can bring these 2 leaders together ni Museveni. Museveni ni rafiki ya Kagame na Kikwete amemwamini kuwa go between. Kikwete amekua na busara kutambua kwamba personal differences zisiachiwe ziathiri uhusiano wa nchi na nchi, na hapo namvulia kofia. Mimi naomba zoezi hili la upatanishi liendelee ili tuzidi kusonga mbele.
 
Sina uhakika kama wale walitimuliwa kutokana na mgogoro wa Kikwete na Kagame. Wale walitimuliwa kutokana na kukithiri kwa ujambazi.
Na katika kauli ya JK kuhusu hilo hakuna sehemu alisema Wanyarwanda warudi kwao, bali wote walioko nchini kunyume cha sheria
 
Yericko,'
Huu si ugomvi kati ya Tanzania na Rwanda. Ni kutokuwepo personal maelewano baina ya Kikwete na Kagame.
That being the case, the only person who can bring these 2 leaders together ni Museveni. Museveni ni rafiki ya Kagame na Kikwete amemwamini kuwa go between. Kikwete amekua na busara kutambua kwamba personal differences zisiachiwe ziathiri uhusiano wa nchi na nchi, na hapo namvulia kofia. Mimi naomba zoezi hili la upatanishi liendelee ili tuzidi kusonga mbele.
Na hakuna ugomvi wowote kati ya JK na KAgame, ni ujinga tu wa huyu Mnyarwanda, alichotakiwa kufanya ni kupuuza ushauri wa JK kama aliona hauna maslahi kwa nchi yake
 
Back
Top Bottom