Hongera CGI, Dr. Anna Petter Makakala

Man-zoo

New Member
Mar 16, 2016
2
0
Uapiswaji wa CGI ( Kaminshina Generali wa Uhamiaji)

Mama ume aminika, mkuu wa nchi ame kuona kua uta ongoza vyema idara yako hii Nyeti kwa Taifa hili.

Mkuu ameshauri total reform ya idara yako aki anza na Ukusanyaji, lakini kuna mengi zaidi unayafahamu zaidi ya mtu yoyote yule kwani baadhi nasikia alisha wahi ku kukuta.

1 . Idara ina ubaguzi mkubwa, kwa wasio na jina husota mpaka hujuta kuajiriwa na IDARA hii
2. Ukabila nadhani bado una zidi kusikia katika IDARA yako hii
3. Nafasi za kwenda MASOMONI sina haja ya kulizungumzia kwa kua UNALIJUA vyema kabisa
4. VYEO, idara nzima inajua kua mwenye dhamana ya nani apewe na nani asi pewe ni Bwana Mkubwa J.K mzee wa Kasikazini. Huyu ndugu na timu yake naamini wenye mioyo mwepesi HUMUABUDU kabisa. Tuna amini kuwa baadhi wana nunua vyeo kutokana na trend ya UPANDAJI wa vyeo katika IDARA hii.
5. Ufichwaji wa FAILI za Askari wako, hili lina enda sambamba kabisa na UPANDAJI wa VYEO, faili za watumishi wengi hu semekana hu fichwa kwa makusudi kabisa hili uta kuthibitisha ikiwa UKIAMUA kuhunda TIMU itakayo PEKUA faili zote za WATUMISHI wako na uone mtiririko wa UPANDAJI wa VYEO.
6.Upendeleo, hii inahusu kila mahali, kuanzia VYEO hadi UNIFORM , kuna mahali utakuta uniform zinapatikana kwa wakati ila kwingine watu wana amua kujishonea, kwa UNIFORM ambazo hazishoneki basi huna jinsi.
7. Kuchafuliwa kwa baadhi ya watumishi kwa faida za watumishi wachache, hili ni kubwa sana na lime athiri watu wengi sana. Haya na mengine yote yana ombewa kufuatilia kwa karibu sana.

Mapendekezo:

1. Kitengo cha UTUMISHI kina hitaji REFORM kubwa mnoo.

2. Kitengo cha UTUMISHI ikishindikana kabisa basi ni vyema KIONGOZWE kwa ROTATION yaani asiwepo wa kudumu, maana hii hu vutia HAKI KUTOTENDEKA na KUABUDIKA kwa baadhi ya WATU.

3. Uanzishwe MFUMO wa ki teknolojia utakao KUSANYA taarifa za ASKARI wote za KIELIMU na Zinginezo, mfumo huu PIA uwe huru kuchangia Mawazo humo ili nawe CGI uwe una uwezo wa Kupata matatizo ya ASKARI wako kwa urahisi kabisa, maana ASKARI atakua huru kutoa maoni na malalamiko ilimradi havunji TARATIBU za jeshi na NCHI . Hii itapunguza kuabudu baadhi ya watu kama huyu wa UTUMISHI. Maana Ukifika sehemu husika zenyewe unakuta unazidi kujenga chuki na wahusika kwa maana wengi wao hawapendi kuona kuwa wame kosea.

Ki jeshi baadhi ya ma pendekzo ni magumu, ila ili kupunguza URASIMU wa baadhi ya idara NDOGO ndani ya JESHI hili basi yote yana wezekana.

Nakutakia UTENDAJI mwema ULIOTUKUKA.

image.jpg
 
Mbona kuhusu rushwa mnazokulaga hujagusia aanze na rushwa kwanza mengine tayatafa
 
View attachment 469853

Naomba nikujibu hoja zako kama ifuatavyo;
1. Kwanza kabisa wewe ni muongo kabisa tena mwenye chuki za kutaka kumharibia CGI mpya. Wewe ni mmoja wa kile kikundi kinachotaka upendelea maalumu hata kama elimu zenu ni kidato cha nne. Nikianza na kujibu namba moja hapo juu, si kweli kuna upendeleo kwa sasa labda kama zamani.

2. Suala la ukabila kama wengi katika hiyo Idara mnavyoajiaminisha kuwa Wa-Kaskazini wanapendelewa halina ukweli wowote kwa sasa, angalia vitengo vingi kama vinaongozwa na Wa-Kaskazini, tatizo lenu shule hamtaki kwenda ila madaraka mnayataka.

3. Ukiongelea nafasi za kwenda Shule ntakushangaa sana kwani ww uliomba kwenda nje ya nchi kusomeshwa ukijua fika kwamba idara haina fungu katika bajeti yake, ukaanza kulalamika weee kuwa wengine wanasomeshwa na ww umekataliwa na ulieleweshwa hilo ila huelewi kwa kuwa ushaamini kuwa kuna upendeleo. Na unajua fika kuanzia mwaka jana hakuna fedha za kusomeshwa watumishi hata ndani ya nchi.

4. Kuhusu suala la vyeo nakupinga kwa nguvu zote, kwani unajua fika kuwa vyeo vinapanda baada ya muda gani na unajua kuwa kuna vyeo ukifika lazima ufanye mitihani ya Lower au Higher ndio upande. Pia kuna vyeo huwezi kufika kama elimu yako ni chini ya Bachelor. Hilo unalijua na kwa kuwa ww ulikosa nafasi ya kwenda kusoma nje ukasusa kusoma ndani ya nchi, nakujulisha kuwa utakaa kwenye cheo chako hadi unastaafu ikiwa hutokwenda shule.

5. Kwenye hoja yako namba tano nazidi kukushangaa sana, hivi ni hujui kuwa kuna Confidential files? Pia ww unashangaza sana kwani huwa unataka ulione faili lako la wazi (PF) ukijua kabisa kufanya hivyo ni kinyume cha utaratibu ndio maana huwa unajibiwa kuwa faili lako halipo.

6. Hoja yako namba 6 haina mashiko kabisa kwani unajua fika kuwa idara ina upungufu mkubwa wa fedha na mara nyingi uniform hugawiwa kutokana na 'priority'. Kipaumbele namba moja unajua kuwa ni vituo vya kuingia na kutoka nchini ambapo askari wote wanatakiwa kuwa na uniform ili iwe rahisi kwa wao kutambulika na wageni na raia wanaoingia na kutoka. Kwenye ofisi za Makao Makuu, Mikoa na Wilaya wanaopewa 'priority' ni wale wanaokutana na mteja hasa katika vitengo vya Customer care, Pasipoti na Permit.

7. Kuhusu kuchafuliwa kwa baadhi ya watumishi kama ulivyodai katika hoja yako namba 7 naiunga mkono kwani hata ww umemchafua huyu J.K. wa Kaskazini pasina kuwa na ushahidi wowote. Naomba ulete tuhuma zenye ushahidi hapa kama kweli humchafui.

Mapendekezo.
1. Tatizo sio kitengo cha UTUMISHI ila ni chuki zako wewe na wale wanaokutuma kuwa hawapandi vyeo. Na ukumbuke kauli ya Mheshimiwa Rais JPM kwamba mwenye elimu ya Form Four afanye kazi kulingana na elimu yake. Sasa wewe elimu yako ya kuunga unga bado unataka mwa-Vyeo makubwa wakati ukijua fika huna uwezo huo. Utaendelea kulia lia mitandaoni ili uonewe huruma ila kwa Utumishi hauto onewa huruma kupanda cheo hadi ukasome kwanza.

2. Pendekezo lako namba mbili unazidi kuandika uongo, katika kitengo hicho hakuna Afisa wa kudumu sema wamekaa muda mrefu. Na mwenye muda mrefu ana miaka 10 na mwingine tisa huku wengine wakiwa na miaka miwili tu ndani ya ofisi hio.

3. Pendekezo lako la 3 nakuunga mkono ila kabla ya kuanzishwa mfumo huo bado una haki zote za kumuona CGI moja kwa moja na kufikisha malalamiko yako. Na huu ni utaratibu wa miaka yote haijawahi kutokea mtu akakataliwa kuomuona CGI, labda kama unataka kuanzisha Thread hapa Jamii Forums muwe mnatoa malalamiko kama ulivyofanya.

Mwisho kabisa fahamu kuwa ukiwa mtumishi wa umma (hasa wa Kijeshi) hutakiwi kuposti uongo uongo humu mtandaoni ukijua fika kuwa ni ni za uongo kwa nia ya kuwachafua watumishi wenzio ambao hawapo katika kambi yenu ya 'Vilaza' nakushauri kuwa toa malalamiko kwa viongozi wa juu kwa kufuata utaratibu unaotambulika kisheria kwani wewe siku zote umekosa imani na kitengo cha Utumishi. Unapokuja kuwalalamikia wana-jamiiForums huo ni uoga uliodhahiri wa ku-face reality.
 
Mbona kuhusu rushwa mnazokulaga hujagusia aanze na rushwa kwanza mengine tayatafa
Huyu ndo kinara wa rushwa, ameonywa sana na akahamishwa kwenda mkoani akaanza kulia lia anaonewa kisa yeye si wa Kaskazini. Kusoma kwenyewe kaunga unga analelewa tu ila kwa kuchongoa domo hajambo
 
Back
Top Bottom