Hongera ACT kwa kupata usajili wa muda lakini

Hongera ACT kwa kupata usajili wa muda lakini

Centrehalf

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2013
Posts
509
Reaction score
145
Salaam wana jf,

Napenda kuchukua nafasi hii kukipongeza chama kipya cha act kwa kupata usajili wa muda.Pia nichukue nafasi hii kuwapongeza wale wote walioshiriki kwa namna moja ama nyingine,kwa kificho au kwa uwazi kuanzisha na hatimae kufanikisha kupata usajili wa muda.Ninaomba sana viongozi watimize masharti haraka sana ili chama kipate usajili wa kudumu.

Kwenye daftari la msajili wavyama vya siasa tulikua na vyama 21 na act ina fikisha idadi ya vyama 22 mpaka sasa.Ukiangalia katika orodha ya vyama 21 ni vyama vinne (4) tu ndio vinavyofanya kazi za siasa ama kusikika.Vyama hivyo ni CUF CCM CHADEMA NA NCCR.

Katika kazi ya siasa kuanzisha chama ni hatua ya kwanza,lakini kukijenga na kukiendeleza chama na kazi ngumu sana na penye hatua hii ndipo vilipokawama vyama vingi hadi vingine kufikia hatua ya kuomba uswahiba na chama tawala.Ni bahati nzuri kuwa chama hiki kinaongozwa na watu wazoefu kwenye medani ya siasa wazoefu wa majukwaani na wanaoelewafika maana ya siasa.

Tunategemea maneno waliuokuwa wanaongea majukwani kabla ya kuanzisha hiki chama yaanze kutekelezwa na demokrasia waliokuwa wanaihubiri kabla itamalaki chamani.

Mwisho na kipongeza chama cha act kwa kupata usjili wa muda lakini kazi bado maana hakuna aliyeiona kazi ya act katka jamii inayotuzunguka kuaminika kwa chama na kupuuzwa kwa chama kutatokana na muundo wa uongozi,sera,katba na mwenendo wa viongozi wa chama.

Nawasilisha.
 
Hapa ndipo utajua sisi waafirika tunafikiri kwa kutumia nini. Nchi zilizoendelea zinazotupa misaada ya fedha na utaalamu kuna vywama visivyozidi vine nchi nzima lkn kuna vyama viwili tu vyenye nguvu......Huku kwetu kila mtu anataka awe mwenyekiti wa chama akishindwa ananzisha chake. Kila mwanachama anataka awe katibu mkuu wa chama akishindwa kupata nafasi anahama au ananzisha chama ambapo ameahidiwa madaraka Fulani. Mwanachama akikosa ubunge eti anahama chama na kwenda kule alikoahidiwa ubunge wa viti maalum au anaanzisha chama chake. Hapo hakuna maslahi ya taifa ni kufikiria njaa na matumbo yao tu basi. Sasa tumeingia kwenye mwelekeo wa vyama vya kimikoa na kikabila na vya dini. MFUMO WETU WA KUWA NA VYAMA UTITIRI UNACHOCHEA ZAIDI KUWACHANGANYA WATZ ZAIDI KULIKO KUWAELIMISHA.Yaani hapa kwetu kwenye hivyo vyama 21 haiwezekani vyana 8 vikakaa pamoja na kuunda nguvu ya kweli kwa sababu kila mmoja kati ya hao nane anataka awe mwenyekiti. HISTORIA INAJIONESHA KUWA SISI MITANZANIA NDO TUMEZIDI NA MPAKA KUFIKIA WAKATI WA UCHAGUZI 2015 TUTAKUWA NA VYAMA ZAIDI YA 50 VIKIWEMO (VIMEMO POLITICAL PARTY, USHOGA PARTY, MIGEBUKA DP, MTU PESA PP, JIGIJIGI PARTY, CCPK-CHAMA CHA PAPUCHI KUBWA NA VINGINEVYO VINGI TU................................Hii sio demoktrasia inayoongelewa nadhani sisi tuna practice kitu kingine tofauti.
 
Alliance of Coward and Traitors-Tanzania....Tanzania haiitaji vyama vingi vya kugombania ruzuku na kugawana wapiga kura ili kuua chama kingine tunataka Taifa salama na siasa safi.
ACT ni aina ya mipasho ya kisiasa iliyobuniwa na wanasiasa kujibu mapigo ya CDM na si kusaidia wananchi tunalijua hilo na tutatoa elimu sana kuwa Tanzania haihitaji vyama vya kinafiki vinavyoota kwa chuki tunataka siasa safi.
 
Salaam wana jf,

Tunategemea maneno waliuokuwa wanaongea majukwani kabla ya kuanzisha hiki chama yaanze kutekelezwa na demokrasia waliokuwa wanaihubiri kabla itamalaki chamani.

Mwisho na kipongeza chama cha act kwa kupata usjili wa muda lakini kazi bado maana hakuna aliyeiona kazi ya act katka jamii inayotuzunguka kuaminika kwa chama na kupuuzwa kwa chama kutatokana na muundo wa uongozi,sera,katba na mwenendo wa viongozi wa chama.

Nawasilisha.
mkuu wewe mwenyewe hapo ulipo ni kiongozi na ni lazima ufanye jambo.Katika hatua za awali amua kuwa kiongozi wa mfano katika eneo lako kwa kuanzia.kila mmoja akifanya hivyo na baadaee nguvu zikiunganishwa hatimae inaweza kuleta matunda mema.
 
Uanzishwaji wa vyama uendane na mazingira, sasa hawa ndio wanaanza, hawajui hata kusolve migogoro ndio kwanza wamekimbia migogoro, hawa watakuwa kama SAUTI, CHAUMA , kazi kujaza karatasi la vyama, au wanataka Dunia iwatambue kuwa walikuwepo, tushachoka na uraghai.
 
kuliko CHADEMA ICHUKUE NCHI BORA CCM ITAWALE MILELE. HATUWEZI KUONGOZWA NA PADRI
 
Back
Top Bottom