Homa ya mapafu (pneumonia): Gonjwa lililosahaulika linalowatafuna watoto. Kila Novemba 12 ni siku ya Pneumonia Duniani

The Sheriff

JF-Expert Member
Oct 10, 2019
617
1,800
pneumonia.jpg

Leo ni Siku ya Homa ya Mapafu (Pneumonia) Duniani. Siku hii inaadhimishwa kila tarehe 12 Novemba kila mwaka.

Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinasema ugonjwa huo uliua watoto 808, 694mwaka 2017, ukiwa unasababisha 15% ya vifo vya watoto walio chini ya umri wa miaka mitano (5).

WHO inasema kuwa ugonjwa huu unaua watoto wengi zaidi kuliko magonjwa mengine kama malaria, UKIMWI na surua yakiwekwa pamoja.

WHO pia inasema homa ya mapafu inawaathiri watu wote kote duniani, lakini zaidi ni katika maeneo ya Asia Kusini na Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara. Ugonjwa huu unaweza kuzuiwa kwa gharama nafuu na huduma za afya za teknolojia ya chini tu.


Kuhusu ugonjwa huu, tembelea:

 

Similar Discussions

Back
Top Bottom