Hoja zisizopendwa na walinda amani wetu!

Hoja zisizopendwa na walinda amani wetu!

Gwalihenzi

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2011
Posts
5,125
Reaction score
1,301
MKUU wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi nchini, Kamishna Paul Chagonja, ni mweledi wa kuzungumza hasa pale ambapo watendaji wake (polisi), wanapokuwa wanatuhumiwa kwa makosa ya wazi.

Lakini wakati anapozungumza anasahau kwamba, taarifa yake inaweza kuonekana ya kujihami au kuupotosha umma na hata kuvunjia heshima Taasisi anayoitumikia.

Wakati wa tukio la mauaji ya mwandishi wa habari wa Channel Ten, lililowahusisha polisi, Chagonja alizungumza na waandishi wa habari akisema hakuna picha halisi inayoonyesha marehemu Mwangosi aliuawa na askari wake, kwamba picha zilizopo kwenye magazeti si halisi, zimetengenezwa.

Hata hivyo, ushahidi wa picha pamoja na Tume zote zilizoundwa baada ya tukio hilo, ikiwemo ya Waziri wa Mambo ya Ndani Dk. Emmanuel Nchimbi, Baraza la Habari Tanzania (MCT), pamoja na ya Haki za Binadamu na Utawala Bora iliyoongozwa na Jaji Kiongozi mstaafu, Mussa Kipenka, zilithibitisha polisi kuhusika moja kwa moja na mauaji hayo.

Katika tukio la ulipuaji bomu kwenye Uwanja wa Soweto, ulipokuwa mkutano wa kisiasa, Chagonja alirudia kosa lile lile la awali, akisema wananchi wanahusika kumlinda aliyedhaniwa kurusha bomu hapo.

Hivyo kufanya polisi wenye mafunzo ya kutosha kuhusu ukamataji wa wahalifu, kushindwa kufanya kazi waliyoisomea!

Lakini, hakuishia hapo, Chagonja alikwenda mbali zaidi akisema katika uwanja huo waliokota silaha pamoja na risasi na kwamba risasi moja ilionekana ya moto ikiwa imeonesha kutumika. Kwa ujanja uleule, Chagonja akawaambia wananchi walijilipua wenyewe.

Lakini wakati anasema hivyo, shuhuda nyingi za watu waliokuwa kwenye tukio wakiwemo wanahabari zinawatuhumu moja kwa moja polisi kwamba ndiyo waliohusika kurusha bomu hilo.

Maswali magumu ambayo yanamfikirisha yeyote mwenye akili, ni polisi kuhusishwa na vifo vilivyotokea. Lakini kubwa ni tuhuma za mtuhumiwa kutoroshwa na gari la polisi zilizotolewa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.

Ushuhuda wa mtoto Abubakar Adam (11), ambaye alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Mount Meru Arusha, kwamba kifo cha mtoto mwenzake, Amir Ally (7) pamoja na yeye kujeruhiwa vibaya vimetokana na kupigwa risasi na polisi.

Wakuu wa polisi walikiri kupatikana kwa maganda ya risasi katika eneo la tukio, jambo ambalo linathibitisha nguvu nyingine nje ya bomu iliyotumika katika uwanja huo.

Maswali magumu ambayo wananchi wangependa kupata majibu yake ni kwa vipi mtuhumiwa ambaye wananchi walimuona kwa macho, lakini polisi na watu wengine wa usalama wameshindwa kumkamata hadi leo?

Ni mbinu gani ya kisayansi inayoelekeza askari waliopewa kazi ya kulinda usalama wa wananchi, kuamua kuzima moto kwa kutumia moto mwingine!

Chagonja atueleze, katika taharuki na mashaka ya kila mtu kujaribu kuokoa maisha yake mwenyewe katika tukio kama lile, wananchi wanawezaje kuzuia polisi kumkamata mhalifu? Hiyo nguvu waliipata wapi?

Simulizi za waandishi wa habari waliokuwa katika eneo la tukio, hazionyeshi kabisa kuwepo kwa tukio wala dalili za wananchi kuzuia polisi kufanya kazi yao, je polisi hao waliamua kutumia risasi za moto kwa sababu gani na kwa manufaa ya nani?

Rejea simulizi ya mwandishi wa habari wa gazeti la Raia Mwema, Paul Sarwatt, Juni 19 -25 mwaka huu, hazionyeshi kuwepo kwa upinzani wowote kati ya wananchi na polisi.

Kamishna Chagonja aseme, kwanini polisi waliamua kutumia silaha za moto kwa raia ambao hawakuwa wakihatarisha maisha ya askari kama sheria inavyosema?

Ni vipi polisi watumie mabomu ya machozi katika tukio kama hilo lenye taharuki na mashaka makubwa?

Kamishna Chagonja asikwepe wajibu wake. Atoe majibu yanayoeleweka kuhusu mazingira yaliyosababisha matumizi ya silaha za moto, mabomu ya kutoa machozi wakati huo tayari kuna bomu limerushwa na kusababisha mauaji na majeruhi ya watu.
Source: Mtanzania 23/7/2013
 
Chagonja ni Mgonjwa ila naamini watanzania hatushindwi kupambana maana kama wangepiga watu kwa makofi bila shaka kila kukicha tungeona maiti za polisi zikizagaa mitaani kwa kupigwa na wananchi ila kwakuwa wanatumia risasi walizopewa na haohao wanaowaua naamini ipo siku silaha zitaingia hapa Tanzania bila wao kujua na ndipo mapinduzi ya umwagikaji damu mkubwa yatakaposhuhudiwa...Viongozi wauaji wa Ccm wanafikiri kwamba hilo watanzania eti hawaliwezi!Kwa ufupi hakuna kinachoweza kuzuia silaha zisiingie hapa nchini hasa kwenye mazingira ambayo polisi wanaua watanzania kwa risasi na mabomu huku viongozi waliojipachika vyeo vya Uwaziri Mkuu na raisi Dhaifu na Juha kama huyu JK wakifurahia.Kibaya zaidi wamegeuza Majeshi ya Nchi ya Nchi kuwa Majeshi ya Chama Chama Mapumbuzi...Kiongozi Juha kama Pinda na Chagonja wanasubiri kushuhudia miujiza ya watanzania siku itakapofika na kushuhudia silaha za kuwindia Swala zikiwamaliza polisi wa Ccm..Tuvute subira ili washuhudie ushenzi wao unaligeuza taifa kuwa Dimbwi la Damu...
 
kashfa zenu na hata matusi ya waziwazi hayana limitation,mnamtusi kila mtu tena bila ya kujiuliza mara mbilimbili..uweledi wote wa chagonja ambao kila mtanzania anautambua nyinyi mnajifanya hamuutambuwi,mnavunja heshima ya kila mtu...si kweli kwamba kila kiongozi hapa nchini anajihusisha na matendo machafu.hao ni wachache sana..muwaheshimu akina chagonja.wanafanya kazi kubwa kuwalinda raia na mali zao
 
Wengi mnafanya kwa unafiki, kwa kuwa m/unalipwa na m/unalinda kibarua, pia chagonja analinda ajira tu. Wengi wamechoka sana kwa sasa. Sasa hivi hata viongozi wa chama chenu wanafichua mipango yenu michafu kwa kuwa katika hali ya kawaida watu huchukia vitendo vya ajabu kama hayo mabomu yenu. Nategemea hata aliyerusha bomu Arusha ni kwa sababu mlimlazimisha, mkamuhakikishia ulinzi ikabidi atekeleze. Tunao wengi wa kuja kuyasema maovu yenu mpaka sasa.......
Dr. Ulimboka, aliyemmwagia tindikali mwandishi wa gazeti la mwanahalisi, Askari aliyempiga bomu mwandishi- Mwangosi, huyo aliyerusha bomu katika mkutano wa CHADEMA Soweto.................

Siku zenu zinahesabika, hamtapona.
 
Chagonja ni Mgonjwa ila naamini watanzania hatushindwi kupambana maana kama wangepiga watu kwa makofi bila shaka kila kukicha tungeona maiti za polisi zikizagaa mitaani kwa kupigwa na wananchi ila kwakuwa wanatumia risasi walizopewa na haohao wanaowaua naamini ipo siku silaha zitaingia hapa Tanzania bila wao kujua na ndipo mapinduzi ya umwagikaji damu mkubwa yatakaposhuhudiwa...Viongozi wauaji wa Ccm wanafikiri kwamba hilo watanzania eti hawaliwezi!Kwa ufupi hakuna kinachoweza kuzuia silaha zisiingie hapa nchini hasa kwenye mazingira ambayo polisi wanaua watanzania kwa risasi na mabomu huku viongozi waliojipachika vyeo vya Uwaziri Mkuu na raisi Dhaifu na Juha kama huyu JK wakifurahia.Kibaya zaidi wamegeuza Majeshi ya Nchi ya Nchi kuwa Majeshi ya Chama Chama Mapumbuzi...Kiongozi Juha kama Pinda na Chagonja wanasubiri kushuhudia miujiza ya watanzania siku itakapofika na kushuhudia silaha za kuwindia Swala zikiwamaliza polisi wa Ccm..Tuvute subira ili washuhudie ushenzi wao unaligeuza taifa kuwa Dimbwi la Damu...

Hivi alishawataka radhi wananchi kuhusiana na kauli za uongo kwenye issue ya Mwangosi?

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
kashfa zenu na hata matusi ya waziwazi hayana limitation,mnamtusi kila mtu tena bila ya kujiuliza mara mbilimbili..uweledi wote wa chagonja ambao kila mtanzania anautambua nyinyi mnajifanya hamuutambuwi,mnavunja heshima ya kila mtu...si kweli kwamba kila kiongozi hapa nchini anajihusisha na matendo machafu.hao ni wachache sana..muwaheshimu akina chagonja.wanafanya kazi kubwa kuwalinda raia na mali zao
Analinda raia wanaounga mkono uuaji wa raia wengine tena wema mfano police ni raia wa Tanganyika ambao hulindwa na Cha=gonjwa wakiua, na wauaji wengine kama Mchumba Magulu tu. Siku yao yaja
 
Back
Top Bottom