Hoja zangu 13 Katiba Mpya. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hoja zangu 13 Katiba Mpya.

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by leroy, May 5, 2012.

 1. leroy

  leroy JF-Expert Member

  #1
  May 5, 2012
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 834
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 60
  1. ''WATANZANIA WARUHUSIWE KUPIGA KURA YA URAIS POPOTE WALIPO DUNIANI''.
  2. ''KUFUFULIWA KWA NCHI YA TANGANYIKA ILIYOPATA UHURU TAREHE 09 DESEMBA 1961, NA KUUNDWA KWA SERIKALI TATU (Muungano, Tanganyika na Zanzibar) KAMA ILIVYOPENDEKEZWA NA TUME YA JAJI NYALALI.
  3. iwepo haki ya kikatiba wanachi kumuondoa,kumshitaki na kumhoji kiongozi waliyemchagua pindi ikionekana amevunja vifungu vya katiba au amekiuka kiapo chake cha uongozi.
  4. Matokeo ya urais yaweze kuhojiwa na kupingwa mahakamani, Rais Mstaafu aondolewe Kinga na kuburuzwa mahakamani kwa makosa alofanya akiwa madarakani.
  5. Tanzania itambulike Kikatiba kuwa ni nchi ya KIBEPARI inayosadifu na kufuata misingi na nadharia za SOKO HURIA, uhuru wa mwanadamu (liberty) ambapo kila raia ana uhuru wa kuchagua (Freedom of Choice)
  6. *********''TUME HURU YA UCHAGUZI''*************
  7. ******ADHABU YA KIFO IFUTWE NDANI YA KATIBA****no human being is supposed to take away other human's life. LIFE IMPRISONMENT ndio iwe adhabu ya mwisho mahakamani.
  8. FUTILIA MBALI NAFASI ZA VITI MAALUM BUNGENI, kipengele cha katiba kinachompa Rais uwezo wa kuchagua idadi yoyote ya mawaziri apendayo kifutwe na Rais apewe limit ya idadi.
  9. Kiundwe chombo HURU chenye uwakilishi wa wananchi cha kupitisha na kuthibitisha mikataba YOTE yenye maslahi (IMPACT) ya kitaifa.
  10. *******Uraia wa nchi mbili (dual citizenship)********Mtanzania awe na uhuru na haki ya kuwa na uraia wa nchi nyingine moja anayotaka.
  11. *******Kuruhusu wagombea ''BINAFSI'' katika ngazi ya ubunge kwa majimbo mbalimbali na Udiwani wa vitongoji pekee*****
  12.
  KATIBA IWEKE WAZI KUWA TAIFA LA TANZANIA LINATAMBUA UWEPO WA MUNGU (GOD), licha ya wananchi wake kuwa na dini tofauti na wengine kutokuwa na dini. PIA TAIFA LIWE NA MOTTO RASMI kama vile (United States of Africa-In God we trust) na sisi (United Republic of Tanzania-God is Great).
   
 2. E

  EVODIUS RWECHUNGURA Member

  #2
  May 6, 2012
  Joined: May 4, 2012
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  KISWAHILI kiendelezwe kuwa ruga ya taifa kiwekewe mkazo kama ni wawekezaji wawe wanajua kiswahili kama awajui basi wajifunze kwanza kabla ya kuekeza au kufanya kazi mashule ya kiswahili yapo tusijishushe kwani rugha inayotambulika wa watanzania wote ni lugha ya kiswahili kama ilivyo kwa nchi zingine na hii itachangia uchumi kukua kwa haraka sana mikataba yote ya kishwahili na Rugha za mikutano na kazini kote ndani ya nchi iwe kishwahiri itakapobidi atakuwepo mkarimani kwa ajiri ya kutafusiria wageni na si vinginevyo hii ni nchi imekua kubwa ni vigumu kuburuzwa kwani chanzo cha uchumi ni mtu wa chini kwanza.
   
 3. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #3
  May 9, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,739
  Likes Received: 1,451
  Trophy Points: 280
  Mchakato wa katiba ulivyo sasa una kasoro nyingi. Mfano:

  1) Composition ya wajumbe wa Tume; it was entirely JK's.

  2) Hayo maoni yanapelekwa kwake, anaweza kuchakachua chochote asichokipenda.

  3) Wameweka (winners' majority kuwa just over 50%).

  4) Wamezuia Muungano usijadiliwe. Pamoja na madhaifu yake lukuki

  5) Wameweka vitisho ktk ukusanyaji wa maoni.

  Kimsingi ninaunga mkono hoja zako, ni nzuri. Lakini mchakato huu kwa namna ulivyo hauko huru, haki na uwazi hivyo tunaweza "kupewa" katiba mbovu au isiyokidhi haja.
   
 4. ZWANGE

  ZWANGE Member

  #4
  May 25, 2012
  Joined: Nov 10, 2010
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  1.kiswahili kitumike kufundisha shuleni. vidudu hadi chuo kikuu
  2.uchaguzi uwe siku yeyote ile isipokuwa jumapili, ijumaa au jumamosi
  3.kuwe na bodi ya ajira
  4.pasiwepo mkuu wa wilaya au mkoa, mkurugenzi anatosha
  5.mamlaka ya rais yapunguzwe
  6. rais mstaafu aweze kufikishwa mahakamani kama akikutwa kufanya ufisadi, ubadhirifu n.k alipokuwa madarakani
  7. iwepo serkali ya majimbo
  8. uwepo wa mgombea binafsi katika ngazi zote
  9.muungano uvunjwe
  muundo mzima wa mahakama na uteuzi wa majaji uchunguzwe upya
  10.kuwa na tume huru ya uchanguzi
  11.takukuru itizamwe upya- viongozi wake wasiwe wa kuteuliwa
   
 5. GHIBUU

  GHIBUU JF-Expert Member

  #5
  May 25, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,188
  Likes Received: 705
  Trophy Points: 280
  Siku ya ijumaa iwe siku ya mapumziko kwa waislamu kitaifa,kama vile jumapili kwa christian.
   
 6. M

  MWANAIDEA Member

  #6
  Jun 16, 2012
  Joined: Jun 16, 2012
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ยท[FONT=&quot] NAPENDEKEZA YAFUATAYO KATIKA KATIBA MPYA

  MIKATABA YOTE INAYOHUSU NCHI IPITIWE NA TUME/JOPO LA WATAALAMU ALAFU IPELEKWE BUNGENI KABLA YA KUSAINIWA NA RAISI.

  UWEPO WA MABUNGE MAWILI


  (I) BUNGE LA UWAKILISHI
  Hili ni bunge ambalo litatokana na kuchaguliwa kutoka kila wilaya ,na mbunge atakua mwenyekiti wa hamashauri husikahivyo basi kila wilaya itakuana mbunge mmoja .hii itasaidia kupunguza idadi kubwa ya wabunge , kuondoa mgongano wa madaraka kati ya mbunge na mkiti wa halmashauri, pia kuwa kiungo kati ya serikali kuu na serikali ya mitaa.yaani halmashuri.kwa mfano kwa sasa tungekua na wabunge133.Nafasi ya mkuu wa wilaya isiwepo majukumu yake yachukuliwe na mkurugenzi wa wilaya.
  (11)BUNGE LA WANANCHI
  Hili ni bunge litakalotokana na kila mwananchi kuwa na nafasi ya kushiriki ,kuchangia ,kupanga , na kuamua masuala ya kitaifa litakua na m/kiti na katibu wake hili ndilo litakua msingi wa maamuzina ushauri kwenye bunge la uwakilishi ,kila mtanzania atapata fursa ya kushiriki na kusema chochote atakachoona kinafaa ili kuimarisha taifa.linaweza likawa linafanyika kwamwaka mara tatu kwa mwaka kujadili mustakabali wa taifa,

  BARAZA LA MAWAZIRI

  baraza la mawaziri liwe ni chombo cha kiutendaji ,hivyo basi liundwe na wataalamu waliobobea ambao watakua ni watumishi wa wa umma nawatawajibika kwa bunge kwa utendaji wao.na watakua wanapewa malengo endapo watashindwa kufanikisha malengo hayo watatolewa kwenye nafasi zao ili kuondoa siasa zisizotekelezeka,

  USIMAMIZI WA FEDHA

  Usimamizi wa fedha uwe chini ya CAG na HAZINA, hazina watatakiwa kupeleka fedha zote kwakuingiza kwenye akaunti zinazohusikakama ni miradi,vijiji, shule,halmashauri au taasisi kupitia akaunti zao mkurugenzi wa wilaya atakua ni msimamizi tu hii ni kuondoa ubadhirifu wa fedha za umma.la msingi ni kuimarisha taasisi hizi.

  UWEPO WA TUME HURU YA UCHAGUZI

  Tume ya uchaguzi huru isiyofungamana na upande wowote,pia iwe na mamlaka ya kushitaki au kushitakiwa na mtu yeyote kikundi au taasisi yeyote,chama.

  IAINISHE VIPAUMBELE VYA TAIFA

  Katiba mpya inatakiwa kuainisha vipaumbele vya taifa,ili kila kiongozi au utawala utakaochukua madaraka ujikite kutekeleza vipaumbele hivyo.kwa upande wangu napendekeza teknolojia ndio kiwe kipaumbele namba moja.[/FONT][FONT=&quot][​IMG][/FONT][FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
   
Loading...