Hoja ya uchokozi: Ya mansoor na rasimu ya 2 ya katiba

Hoja ya uchokozi: Ya mansoor na rasimu ya 2 ya katiba

Joined
Sep 9, 2012
Posts
43
Reaction score
11
Kwanza kabisa naomba niwatakie wadau wote maandalizi mema ya kuupokea mwaka mpya wa 2014 masaa machache yajayo.

Hoja yangu ni kumhusu waliyemwita msaliti wa msimamo wa ccm kuhusu muundo wa serikali unaofaa kutumika Tanzania kwa wakati huu.

Ikumbukwe ccm wanaamini katika mfumo wa serikali mbili yaani serikali ya mapinduzi ya Zanzibar na serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kitu ambacho kinaonekana kupingwa na wadau wengi kwa mustakabali wa kuunusuru muungano wa Tanganyika na Zanzibar unaoonekana kuyumba sana siku za hivi karibuni.

Sasa, hoja yangu nimeitoa mara tu baada ya kuzinduliwa na kukabidhiwa kwa rais wa JMT na rais wa SMZ rasimu ya pili ya katiba. Katika rasimu hiyo tumeshuhudia pamoja na mambo mengine yaliyoreshwa kama yalivyokuwa yameainishwa katika rasimu ya kwanza ya katiba ni kuhusu muundo wa serikali ambako rasimu imetanabaisha wazi juu ya muundo wa serikali tatu yaani jamhuri ya watu wa Zanzibar ,jamhuri ya Tanganyika na jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Si hivyo tu bali hata mwenyekiti wa tume kapambanua na kusisitiza bila ya kumumunya maneno kuwa muundo wa serikali tatu "HAUEPUKIKI" kwa sasa kulingana na maoni ya wananchi wengi na ili kuunusuru muungano tulionao sasa.

Hoja yangu pia imerejea maoni ya ccm kuhusu rasimu ya pili ya katiba mara baada ya uzinduzi wa rasimu hiyo ambako vyombo vya habari vimemnukuru katibu wa itikadi na uenezi wa ccm Nape Nauye akiipongeza tume kwa hatua walipoufikisha mchakato wa katiba na alipoulizwa kuhusu muundo wa serikali uliopendekezwa na tume kwa mara ya pili ambao ni kinyume na msimamo wa ccm alikiri kuyapokea maoni ya na yatapimwa kwa kujadiliwa katika vikao halali vya chama chao kulingana na hoja zilizotolewa na tume na kutoa msimamo wa chama.

Hoja yangu ni je? kama ccm watatafakari hoja za tume juu ya muundo wa serikali tatu na kuziona zenye mashiko watakuwa tayari kubadili msimamo wao wa awali?, je kama watakubali kubadili msimamo wao huo, chama kitakuwa tayari kumrudishia Mansoor uwakilishi wake wa kiembesamaki na kumuomba radhi kwa walichomfanyia? kwa kuwa alivuliwa uwakilishi huo baada ya kutofautiana kimtazamo na chama chake kuhusu msimamo wa chama juu ya muundo wa serikali katika katiba mpya.

Na je vipi kama watashindwa kukubaliana na hoja za tume juu ya muundo wa serikali nini kitatokea?

Naomba kutoa hoja.
 
!
!
Chungu japo ni ndiyo dawa yenyewe, watakubali tu ila kumrudisha kundini ndio itakuwa ngumu
 
Hapa ma ccm yalikosea na kukurupuka ,kama cc ya chadema ilivyokosea kumvua unaibu katibu mkuu bara ZZK kwa kuvunja katiba yao na kanuni wenyewe kwa upofu wa victimisation
 
Hapa ma ccm yalikosea na kukurupuka ,kama cc ya chadema ilivyokosea kumvua unaibu katibu mkuu bara ZZK kwa kuvunja katiba yao na kanuni wenyewe kwa upofu wa victimisation

Tehe tehe tehe...Namuona Mwanasheria mahiri Tundu Lissu pale. Huyu anajua kuzungusha zungusha sheria kweli! na anawasumbua kweli! Tehe tehe. (...Kikwete 30/12/2013)
 
Back
Top Bottom