MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,244
- 7,970
Hua napata tabu kidogo kusikia kwamba eti kuna watu wanajinasibu kua kua UKAWA watashindwa sana uchaguzi mkuu 2020. Najiuliza mengi sana juu ya hili, UKAWA watashindwaje? Wataanza anzaje?
Kwa maana hiyo ukisema CCM itashinda UKAWA watakua wamekaa tuu au wamesimama?Kuna anayependa kupoteza kiti chake? Wananchi watakua wajinga kiasi gani kukubali kukipa kura chama ambacho walishakikataa? Unafikiri Magufuli anaweza kubeba hadi magari chakavu ambayo yanajikongoja ambayo yalikwishakataliwa na umma?
Kuna wanaofikiri kua kwa jaribio la serikali kutaka kuzuia mikutano ya kisiasa kunaweza kuwabeba hadi uchaguzi 2020, hawatambui kua hili suala la mikutano ni la kikatiba na ni wajibu mojawapo wajibu wa vyama vya siasa, hata hao wanaofikiri kudhibitiwa kwa vyama vya siasa kufanya mikutano hawajui kua hata wao hawatapata muda wa kujenga ushawishi kwa wananchi,maana wao wakiruhusiwa kufanya mikutano UKAWA nao hawatakubali hata kama iweje na watakua tayari kwa lolote lile.
Kwa sasa UKAWA wameshaapa kua hakuna atakayewazuia kufanya mikutano kwakua ni suala la kikatiba na watakua tayari kwa lolote(By James Mbatia 20 June 2016 &Bavicha taifa). Hivyo kwa maneno ya Mbatia kama watafanya hivyo CCM hawatakua salama. Kwa sababu kama UKAWA wakitekeleza hayo wanayoyasema kwa kutorudi nyuma kama walivyoapa kunaweza kuleta mtafaruku mkubwa kwenye jamii na atakayelaumiwa ni serikali na ndipo CCM watakapokabiliwa na wakati mgumu.
Kwaa maana hiyo CCM wanaweza kua katika wakati ngumu sana kwa maeno mawili! Moja ni pale ambapo UKAWA wakifanya mikutano yao kwa kuzunguka nchi nzima kuwaeleza wananchi nini kinachofanywa na serikali ya Magufuli kwa sasa ikiwa ni pamoja na kutoa sababu ya wao kutoka nje ya bunge, hii hali ukilinganisha na hali ya maisha ilivyo kunaweza kusiwaache CCM salama.Pili ni pale ambapo UKAWA wataamua kufanya mikutano yao nchi nzima kwa kigezo cha haki yao ya kikatiba na kuamua kuingia kwenye vurugu na jeshi la polisi nchi nzima, pia ni hali itakayoichafua serikali na chama kwa ujumla na kuwapa wakati mgumu 2020 kinyume na matarajio yao.
Kujinusuru na hali hii serikali na CCM watumie diplomasia zaidi kuendesha nchi kuliko nguvu, wajenge hoja zaidi kuimarisha serikali na chama kuliko nguvu. Ni ngumu sana kutumia mababvu kutawala nchi ambayo imejaa wasomi na werevu wengi, walishaazoea demokrasia na amani muda mrefu, Utawala wa mabavu Tanzania kwa sasa umeshachelewa sana serikali ishauriwe juu ya hili.
"RAMADHAN KAREEM"