Hoja ya chiligati imeeleweka? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hoja ya chiligati imeeleweka?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Anold, Apr 14, 2011.

 1. A

  Anold JF-Expert Member

  #1
  Apr 14, 2011
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,378
  Likes Received: 296
  Trophy Points: 180
  Juzi katika kile CCM ilichoita kujivua gamba, nilimsikia mzee Chiligati akieleza bayana kuwa wale watu wote wanaotajwatajwa kwenye kashfa za Richmondi na Dowans wajipime na kuchukua hatua za kukinusuru chama. Mimi hili nimelipokea kwa mikono miwili ila sina uhakika kama kweli mzee huyu alichotamka anakielewa au ni kutokana na furaha ya kurudi kwenye nafasi yake. Ninasema hivi kwa kuwa inapokuja suala la "wanotajwatajwa kwenye Kashfa ya Richmond na Dowans" ukiondoa mtu kama Rostam Azizi na Lowasa, Kuna baadhi ya viongozi waandamizi wa serikali ambao nao wametajwatajwa kuhusika kwa njia moja au nyingine kwenye kashfa hizo je nao tangazo hilo la kuwajibika linawahusu au siasa za kuoneana haya na unafiki zitaendelea ndani ya ccm? Maana unapozungumzia haya masuala ya Dowans, kama haki ikitumika, nafikiri serikali nzima ilihusika vilivyo kutufikisha hapa tulipo. Mzee Chiligati anataka atueleze kuwa kama ulihusika lakini hukutajwa sio tatizo, huu kwangu ni mchezo wa kuigiza maana kwa siasa hizi sasa sidhani kama ni za kukisaidia chama, maana huu ni mwanzo wa uhasama na kutakiana mabaya, sasa makundi ndani ya chama ndiyo yataibuka na sina uhakika kama ule mshikamano wa kwanza utarudi. CCM inajaribu kupiga mswaki kuondoa harufu wakati tumbo ndiyo linatatizo.
   
 2. L

  Lilombe JF-Expert Member

  #2
  Apr 14, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 242
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yeye aliyetamka yale aliyetumwa na kiranja mkuu; CCM ni wafa maji wakati huu wamebanwa sana na CDM sasa wanafuta pa kutokea pasipo kujali huko nyuma RA na EL walitumika sana kuratibu zoezi la wizi wa kura. Hiki ni kipindi cha kujisafisha machoni mwa wadanganyika mengine yataeleweka mbele ya safari hata kama EL na RA wanapotea katika ulingo wa siasa za Bongo hilo kiranja mkuu halijali
   
 3. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #3
  Apr 14, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  Katika wizi wa fedha EPA Benki Kuu, Mhe Jakaya Kikwete pia litajwa kuwa fedha hizo zilitumika kumuingiza Ikulu, Hivyo naye anatakiwa kujiuzulu kama kweli CCM imedhamiria kujisafisha. Bila ya Kikwete kujiuzuru hakuna mtu yoyote atakayejiuzuru kwani utakuwa ni mchezoi wa kuigiza tuu.
   
 4. O

  OgwaluMapesa JF-Expert Member

  #4
  Apr 14, 2011
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 10,948
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Yeye ajionaye amesimama Chiligati ajitazame asije akaanguka. Kuvuka kwa gamba ni suala la muda na kusudio la kazi husika.
   
 5. A

  Anold JF-Expert Member

  #5
  Apr 14, 2011
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,378
  Likes Received: 296
  Trophy Points: 180
  Kumbe ndiyo maana viongozi wengi wa ccm walikwenda kupata kikombe Loliondo !!:second:
   
 6. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #6
  Apr 14, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Kwa sisiemu wamebadili usemi na kusema maneno hukidhi haja maridhawa kuliko matendo badala ya kinyume chake!
   
Loading...