Hoja si nani analipia/amelipia matibabu ya Lissu, hoja ni akina nani walimshambulia na ni kwanini walimshambulia Lissu

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,197
25,517
Tunafahamu kuwa Mbunge wa Singida Mashariki na Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Wakili Msomi mwenzangu na Rais wangu wa Chama cha Mawakili wa Tanganyika Tundu A.M. Lissu ameshambuliwa kwa risasi katik viunga vya nyumbani kwake huko Area D,Dodoma. Kwasasa, Lissu anapokea huduma za kitabibu huko Nairobi, Kenya.

Kwa wingi wetu, tunaendelea Lissu kuomba ili arejee kwenye afya yake njema na kurejea kwenye majukumu yake ya Ubunge, uongozi wa TLS, uongozi wa CHADEMA na Uwakili. Tunafahamu sasa kuwa Jeshi la Polisi tayariu limeanza uchunguzi kuwabaini wahusika wa shambulio la Lissu ili waweze kufikishwa kwenye mikono ya sheria.

Kunaibuka kwa kasi malumbano yasiyo na tija (kwa maoni yangu) juu ya nani hasa analipia au amelipia matibabu ya Lissu kule Nairobi kuanzia kusafirishwa kwake na hata sasa. Sioni mashiko ya hoja hii kwakuwa suala lililopo ni Lissu kupata matibabu. Mchangiaji yeyote, awe wa chama chake au chama kingine au asiye na chama wa ndani na nje ya Tanzania, aweza kuchangia matibabu ya Lissu na kusiwe na hoja.

Kwa hali ilipofikia, mambo ya uvyama yanazidiwa nguvu na mambo ya ubinaadamu na uhai wa mtu kwa ujumla. Hoja iliyo mbele yetu, na mikononi mwa Jeshi la Polisi, ni akina nani walihusika na shambulio la Lissu na walisukumwa na jambo gani hasa. Majibu ya hoja hiyo yatatufunza na kutuimaisha kimaisha, kisiasa, kiusalama na kiutawala.

Pray for Hon. Tundu A.M. Lissu to quickly recover!
 
Eti watu wasiojulikana, hahaha...waweze kuingia mpaka ndani kabisa ya mageti ya Area D yenye waheshimiwa likuki na kulipo na ulinzi 24/7 tena huku wakiwa na gari lisilo na Plate no. ?

Waliomvamia Tundu Lissu ni wale walioumizwa sana na suala la Mh. Mbowe kumpeleka Dereva wa Lissu Nairobi.

Narudia tena, Suala la huyo Dereva kupelekwa kule ni "Best Trick" na inawaumiza sana hawa jamaa, akirudi tu na kupewa muda wa kuzungumza huku wakiwepo wataalam wa upelelezi, mithili ya FBI, baas itatupa picha kabisa ni nani waliomshambulia Tundu Lissu.

Wabillah Tawfiq,
 
Swali la nyongeza:
Wakati wa uwasilishwaji wa ripoti za Almasi na Tanzanite, Ndugu BASHITE alikuwa wapi na kwa udhuru upi? Maana twamjua anavyopendaga kutokea "Font Fedi"
 
Kwa hali ilipofikia, mambo ya uvyama yanazidiwa nguvu na mambo ya ubinaadamu na uhai wa mtu kwa ujumla. Hoja iliyo mbele yetu, na mikononi mwa Jeshi la Polisi, ni akina nani walihusika na shambulio la Lissu na walisukumwa na jambo gani hasa. Majibu ya hoja hiyo yatatufunza na kutuimaisha kimaisha, kisiasa, kiusalama na kiutawala.
Wale waliouliwa kibiti sio watu.ila Tundu Lissu ni super human ndio maana unataka watu wajadili risasi zake
 
Wale waliouliwa kibiti sio watu.ila Tundu Lissu ni super human ndio maana unataka watu wajadili risasi zake
Hakuna MTU aliyezuia kujadili ya Kibiti.Uliwahi kuzuiwa na nani na lini?

Lissu kufanyiwa hayo yaliyotokea ni sababu tosha ya kumfanya awe tofauti na hao wa Kibiti. Upende au usipende huo ndiyo ukweli!

Tangu uzaliwe hadi Leo nani kafanyiwa kama Lissu unayemfahamu? Tutajie.

Ambaye haoni mchango wa Lissu ktk nchi hii ama ni mnafiki,mwongo au ana wivu usio na tija. Wanaoishi maeneo ya migodini,waliowahi kuonewa kwa kubambikiwa kesi/kuporwa haki mahakamani ni mashahidi wa hili.

Kutompenda kwako Lissu hakuondoi thamani na umuhimu wake.
 
Hivi Malya! Malya yulee! Yule Dereva, dereva wa Chacha (RIP), ati wapi siku hizi, ama karudi Libya alikopatia yale mafunzo? Nimeuliza tu!
 
Swali la nyongeza:
Wakati wa uwasilishwaji wa ripoti za Almasi na Tanzanite, Ndugu BASHITE alikuwa wapi na kwa udhuru upi? Maana twamjua anavyopendaga kutokea "Font Fedi"

Huyo kwa waliokaribu naye wanasema alikuwa Dodoma na asubuhi chwe alio ekana Morogoro. Na lile gari linalotuhumiwa limepigwa kiberiti hapo Morogoro.

Hovyo kesi imeishakwisha
 
Eti watu wasiojulikana, hahaha...waweze kuingia mpaka ndani kabisa ya mageti ya Area D yenye waheshimiwa likuki na kulipo na ulinzi 24/7 tena huku wakiwa na gari lisilo na Plate no. ?

Waliomvamia Tundu Lissu ni wale walioumizwa sana na suala la Mh. Mbowe kumpeleka Dereva wa Lissu Nairobi.

Narudia tena, Suala la huyo Dereva kupelekwa kule ni "Best Trick" na inawaumiza sana hawa jamaa, akirudi tu na kupewa muda wa kuzungumza huku wakiwepo wataalam wa upelelezi, mithili ya FBI, baas itatupa picha kabisa ni nani waliomshambulia Tundu Lissu.

Wabillah Tawfiq,
Je wewe unawajua?
 
SIDHANI KAMA WANAENDELEA NA UCHUNGUZ.

TUKIO LIMETOKEA MCHANA KWEUPE TENA NDANI YA NYUMBA ZA WABUNGE KATIKA MJI MKUU WA NCH HADI LEO HAJAKAMATWA MTU

LAKN GEN. MRITABA KAPGWA RISAS NJE YA MJI HUKO WATU WAMEKAMATWA HARAKA.
 
Tanzania tuna taratibu na ustaarabu wetu.
Hizi siasa za awamu hii za kuuana sio ustaarabu na taratibu zetu.

Na Yeyote ambae anaenda tofauti na taratibu zetu mwisho wake upo karibuni sana
 
Ya malipo muhimu sana
Waambie viongozi wenu waweke hata bank statement kuonyesha pesa wanadai wamelipa walilipa wao au njia walitumia kufanya hayo. Walipewa pesa kama alivyosena Spika wao wakaenda kulipa na kupewa risiti.. hiyo haishangazi as kwani tunajua hawawezi kuandika jina la aliyewapa msaada

Upinzani mkianza kula pesa mnateteana...eeeeh ila ukweli haufichiki jamani.. wekeni docs tuzione kila kitu.. lazima tuongelee pesa kwasababu wanapokea pesa za watu pia wenye roho nzuri kumsaidia mgonjwa bali wao haoooo matumbo mbele.
 
Inakuuma nini Mkuu nenda kajibu kwanza maneno ya mange kuhusu jinsia yako mkuu
 
Wale waliouliwa kibiti sio watu.ila Tundu Lissu ni super human ndio maana unataka watu wajadili risasi zake
Hao tulishawajadili sana humu tafuta nyuzi zake au anzisha uzi wake lakini uzi huu unamhusu Tundu Lissu aliyetaka kuuliwa hivi karibuni
 
Back
Top Bottom