Hoja: Motor vehicle inatakiwa ilipwe na kila mtu anayetumia Barbara hata Kwa kutambaa

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
6,466
2,000
Habari zenu wadau!

Naomba kutoa hoja ya ufafanuzi kuhusu kufutwa Kodi ya magari barabarani.
Nianze Kwa kuipongeza serikali Kwa kuamua jambo jema kama hili la kuondoa miongoni mwa kodi ambazo ni mizigo!

Motor vehicle license kuwekwa kwenye gari pekee! Ni kodi iliyokuwa na mlengo hasi Kwa wamiliki Wa vyombo vya moto, ni kodi iliyowafanya watu wengi waamini kwamba anayepaswa kuirinda barabara ni mwenye gari pekee! Mrundikano Wa kodi Kwa mwenye gari uliwafanya watu wengi waamini kwamba gari ni chombo cha starehe, kuna watu wala hawakuwahi kushughurisha bongo zao kwamba, mbali na biashara kuna watu walemavu, wagonjwa n.k ambao wanalazimika kuwa na usafili wao binafisi, usafili wao ndiyo ilikuwa miguu yao, kuna watu gari kwao ni kama wheel chair! Pasipo gari hatoki, mtu Wa namna hii hatofautiani na mtembea Kwa mguu anayetumia barabara bila malipo!

Kodi hii iliwafanya baadhi wajione kwamba wana special offer ya kutumia barabara, ndiyo maana hawa watembea Kwa miguu wanatajwa kuhusika na uharibifu Wa miundombinu ikiwemo, kung'oa alama za barabara ni, kuchimbua barabara, kufungua mabolt ya madaraja n.k hii yote ilisababishwa na kutokujua umhimu Wa Barabara!

Sasa Kwa bajeti hii mpya kila mtu atalipia barabara, ni haki na wajibu Wa kila mtumia barabara haijalishi una gari au hauna gari, katika kuimarisha miundo mbinu sote tunapaswa kuwajibika! Ni kodi rafiki Kwa kila mtu,

"Lips kadri unavyotumia" ni utaratibu Wa kiungwana kabisa huu, kila mtu ataguswa na ulinzi Wa barabara! Ambaye anasema kaonewa muulize hatumii barabara? Kila mtu anatumia barabara iwe Kwa mguu, Kwa punda n.k wapo waliochangia kuharibu barabara Kwa kupitisha mifugo bararani au kulima kando kando ya barabara! Hawakujali kwakuwa walijua haiwahusu!

Naipongeza sana serikali Kwa kuweka kodi nzuri namna hii,
Sasa majembe na Yono watafte kazi nyingine! Wasiojuwa ni kwamba hii kodi ya magari imekuwa inachangia sana watu kufisiwa Kwa magari yao kupigwa mnada, screpa kutozwa kodi; ni kodi iliyochangia kufilisi watu wengi, ni kodi iliyochangia vifo Kwa presha.

INALILLAH MAJEMBE NA YONO!
********KIRUUUUUUUUU********
 

imhotep

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
22,586
2,000
Safi sana serikali,sasa ni zamu ya kudhibiti wapiga nyoka wa wese mitaani ili mapato yasipotee.
 

mansakankanmusa

JF-Expert Member
Sep 30, 2010
4,175
2,000
Sasa Kwa bajeti hii mpya kila mtu atalipia barabara, ni haki na wajibu Wa kila mtumia barabara haijalishi una gari au hauna gari, katika kuimarisha miundo mbinu sote tunapaswa kuwajibika! Ni kodi rafiki Kwa kila mtu/mdudu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom