MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,244
- 7,970
Hivi watanzania ni kwanini tunapenda kujitoa ufahamu kwa makusudi? Ni kwa faida ya nani ?ni sifa? Kwanini mtu unakurupuka na kuanza kuhoji jambo pasipo kuangalia uzito wa jambo?
Kama mbunge akiwepo bungeni akitoa hoja hasikilizwi, akisema jambo hasikilizwi, hata kama ni jambo linalowahusu wananchi wa jimbo lake hasikilizwi, Hivi akikaa bungeni atawakilisha kitu gani? Atamtetea mwananchi wake kwa njia ipi maana akitoa hoja haisikilizwi? Mnataka akae kwenye kiti kimya kuanzia asubuhi mpaka jioni asiseme kitu abaki kupiga meza? Mnataka aungena na wabunge wa CCM kuitikia "ndiooo" au sio?
Naombeni mnijibu akae bungeni kumwakilisha mpiga kura kwa utaratibu upi?haya hata tukisema wasitoke wabaki ndani wajenge hoja,watajega kwa utaratibu upi maana kila wasemacho huambiwa kaa chini? Kwa maswali yangu haya bado mnahoji ni kwanini wabunge wa upinzani wanasisia vikao vya bunge?
Ninawashangaa sana watu wanaohoji kitendo bila kutazama uzito wa hoja pamoja na jambo au tukio lenyewe.
Ile hekima ya "Wengi wape na wachache waheshimiwe" iko wapi?