HOJA KUNTU: Uhuru ni Bora kuliko utumwa; Misaada basi tujitegemee!

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
17,506
16,004
Amani iwe kwenu.

"Give me Librty Or Give Me Dearth" ni maneno ya Gavana wa Virginia aliyatamka tarehe 23,Machi 1775 akipinga utawala wa mfalme wa uingereza (japo nayeye alitokea uingereza). Hotuba hii maarufu ilitaka rasilimali zinazopatikana Marekani zibaki hapo kunufaisha wamarekani na sio uingereza na kutaka uhuru wa kupanga mambo yake.

Hivyo Marekani ilipata uhuru tar.4,Julai 1776.Miaka 169 baadaye US kupitia mpango wa Marshall anazikopesha nchi za ulaya ikiwamo uingereza zilizofilisika baada ya vita ya pili ya dunia,1945 takriban dola bilioni 13 (sawa na dola bilioni 130 machi,2016,wikipedia).

China kwa kudhibiti rasilimali na kufanya Kazi kwa bidii ni nchi ya kwanza duniani kwa vigezo vya GDP "PPP" ikiiacha marekani.Mifano yote miwili inatufundisha hakuna nchi duniani iliyowahi kuupiga vita umaskini kwa kutegemea misaada.

Misaada ina masharti mazito sana ambayo mara nyingi huambatana na kutoa rasilimali zetu zenye thamani kubwa kwa kupewa vidonge na vyandarua. Kwa takwimu zilizopo IMF/WB nchi nyingi za ulaya na marekani wamezidi ukomo wa kukopa "Debt/GDP ratio" ni zaidi ya asilimia 100 huku mkopeshaji mkuu wa nchi hizo akiwa China.Tusidanganyike hawa jamaa hawana pesa za msaada kwa ajili ya umeme,maji,barabara sana sana wanatoa misaada ya kibinadamu kama dawa,vyandarua na kufadhili propaganda zao kupitia NGOs na Vyama vya kiraia.

Kama taifa tunahitaji kuwa na akili ya kawaida "common sense" anayotumia kijana kutoka nyumbani kwao na kwenda kujitegemea kuanzisha familia yake.

Kuwabaini na kuwapuuza mabepari na vibaraka wao ndani na nje ya nchi ambao kazi yao huwa ni moja ya kukatisha tamaa wananchi na serikali kwa kuharibu mwelekeo.

Kuunda na kusimamia sheria ili kudhibiti vitendo vyovyote vyenye kuhujumu uchumi na uzalendo.

Misaada imeleta madhara yafuatayo kwenye nchi yetu.

1.Imesababisha watawala kuwafurahisha na watoa misaada na sio wananchi wanaopiga kura.

2.Viongozi wameondoa wajibu wao na kuyatwika kwa USAID,DFID nk.

3.Mbaya zaidi imeuwa uwezo wa ubunifu kutoka kwa viongozi kwani misaada hiyo huja na "blue print" na wasimamizi ni wenyewe wazungu.

4.Misaada imechangia rushwa na ufisadi kwa kiasi kikubwa.Wanasiasa wa nchi wafadhili hushirikiana na wanasiasa wa hapa jinsi ya kuiba fedha hizo. Mf.Rada.

5.Misaada husababisha vita na mifarakano.Wahisani wanafadhili uchaguzi/demokrasia kwa lengo la kuweka madarakani vibaraka wao.

Ninajua humu JF wajuvi ni wengi na ni matumaini yangu kuwa wanasiasa wetu wanakodolea macho JF huu ni ushauri kuntu hasa tukizingatia wito wa Raisi John Magufuli (PhD) kuwa Tanzania ni tajiri.

Wamarekani waligundua hili karne ya 18 wakaachana na uingereza na kutengeneza dola kubwa kisiasa na kiuchumi kwa uamuzi tu wa kujitegemea. China walifanya mapinduzi ya kiuchumi miaka zaidi ya 60 iliyopita lakini kwa sasa wapo juu kiuchumi.

Lazima tubadilike inawezekana.
 
Back
Top Bottom