Hoja isiyojulikana

FUSO

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2010
Posts
36,507
Reaction score
45,129
Nimesukumwa kuandika hoja isiyojulikana sababu tumeamua kuishi kwenye jamii yenye watu wasiojulikana. Nani anataka kumjua mwenzake? hata humu hatujuani. Kutojulikana kwa watu kunaanzaia kwenye ngazi ya familia - kwa mfano nyumba moja mtoto kabakwa aliyembaka hajulikani kwa sababu anatoka katika kundi la watu wasiojulikana - ndani ya nyumba kuna baba, mama, makaka, madada, wajomba, mashangazi, wapwa, wajukuu na vitukuu. Wote hawa hawajui ni nani kabaka ubakaji ambao umefanywa ndani ya nyumba wakati mtoto kalala chumbani na wenzake na watu wasiojulikana.

Dhambi ya watu wasiojulikana inasonga mbele kwa kazi kubwa kutoka kwenye ngazi ya Kaya, Tarafa, Wilaya hadi Taifa; Unapata bia yako mtu anakusogelea huku akikupumulia moshi wa sigara, wewe vipi unanijua mimi? nakuuliza unajijua mimi? Wewe kwa woga unasema sikujui - hapo wasiwasi unakuingia mmhh labda itakuwa ni wale wale watu wasiojulikana ingawa unamcheki kwa sura ila huna uhakika kama anajulikana - unameza mate unasema isiwe taabu unaondoka mdogo mdogo kuinusuru roho yao - ogopa sana kukutana na watu wasiojulikana.

Kuna mwanakijiji kapotea mwezi wa tisa sasa hajulikani alipo; juhudi zote zimefanyika kumtafuta hakuna jibu - watu wanahisi huenda wakawa watu wasiojulikana.

Kuna mwnakijiji mwingine alipotea, then akarudi lakini cha ajabu hajasema alienda wapi, watu wanahisi anaogopa kuwataja watu wasioonekana.

Hapa ndipo tulipofikia, watu wasiojulikana ni miongoni mwetu wenyewe lakini hawajulikani - ngazi ya kaya mtoto kabakwa ndani humo humo na watu wasiojulikana, ngazi ya taifa mtu katishiwa na bastola na hawa hawa watu wasiojulikana; mtu kamiminiwa risasi nyingii sana zaidi ya 30 na hawa hawa watu wasiojulikana.

Hata kama utawajua kwa sura na mwenendo lakini wenzako sifa yao kuu ni kwamba "watu wasiojukalikana".

Watu wasiojulikana wapo kila mahali ila omba usikutane nao, hawajali wewe ni mzuri kiasi gani, nini mchango wako kwa ukoo wako, kijiji chako hata taifa, ukikutana nao ni timbwili la kufa mtu. Tatizo letu kubwa hapa tumeshawakubali wawe sehemu ya maisha yetu kwani hakuna mikakati inayoonekana ya kuwangamua ili wajulikane.

Sasa swali kwa jamii nzima, Je tuendelee kuwakumbatia hawa watu wasijulikana? Je tufanyaje ili waonekane?
Ni lazima tuamue sasa kwa sababu wanaharibu kabisa image ya taifa letu - leo yule mzee na familia yake hapati wageni sababu wanaogopa lile tukio la mtoto kubakwa na watu wasiojulikana -

Narudia ni lazima tulinde image ya taifa letu sasa - hawa watu wasiojulikana sasa wajulikane na jamii kuanzia yule mzee mwenye mji unaobaka watu hadi huku kwenye taifa watu wafanye kazi zao bila woga.

Zamani zama zile miaka ya 70 kweusi watu waliwaogopa sana wanyonya damu sasa hii karne ya 20 shukuru sana ukutane na hao wanyonya damu lakini usiombe kukutana na watu wasiojulikana, sababu hutajua unakwenda wapi ama unatoka wapi - utanyamaza milele.

"Say No kwa watu wasiojulikana" chukua hatua

Alamsiki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…