Hoja: Halmashauri zote nchini zifutwe

Majizi chadema mwambieni Mbowe alipe Deni la Nhc na pia alipe wafanyakazi wa gazeti la Tanzania daima.

Mwambieni aache maigizo ya kukata, funua na kushika ukuta
Kama serikali inashindwa kudai deni la mtu mmoja mbowe basi ni dhaifu sana. Yaani mtu kulipa deni mpaka aambiwe na wengine wakati serikali inayomdai ipo.
 
Itapunguza gharama za uendeshaji,jiulize kama kuna mwenyekiti wa kijiji na mtendaji wa kijiji sio sababu ya kuwepo diwani.
Diwani ni nafasi tumeiga kutoka nchi za wenzetu,sio lazima kuiga kila kitu.
Angalia diwani analipwa posho,wakati mwenyekiti wa kijiji anajitolea.
Na kiwango cha elimu kama kigezo cha sifa ya kugombea hizi nafasi kinapaswa kurekebishwa iwe angalau elimu ya kidato cha 4.
 
Trump alishasema Africa kuna demokrasia na akiwa rais ( ni rais mteule sasa) atahakikisha madikteta wote wanaondoka madarakani. Ataanza na Mgabe
 
Itapunguza gharama za uendeshaji,jiulize kama kuna mwenyekiti wa kijiji na mtendaji wa kijiji sio sababu ya kuwepo diwani.
Kisheria na kimfumo Mwenyekiti wa kijiji ana "Serikali" lakini Diwani ni mwakilishi tu wa mawazo ya wenye serikali zao kwenye Halmashauri. Lakini kwa kuwa kwa muda mrefu Halmashauri nyingi zilikuwa chini ya CCM Madiwani walikuwa ni wajumbe wa Kamati za siasa za Kata kwa ivo kichama walikuwa na nguvu na ushawishi mkubwa sana kuliko wenyeviti wa vijiji ama mtaa. Matokeo yake Madiwani wakati mwingine hujifanya kuwa wao ni mabosi wa Wenyeviti wa mitaa/vijiji.

Pia sheria za serikali za Mitaa zina utata. Wakati kwa maeneo ya vijijini wenyeviti wa vijiji wamepewa hadhi kamili ya kuwa dola, yaani wana Ardhi, Chombo cha Usalama na Mfumo wa utoaji haki kimahakama, kwa mijini ni tofauti. Lazima kuwe na uwiano na ni lazima sheria itambue maamuzi ya hizi Halmashauri kutoingiliwa na watu wa serikali ya JMT au ya Tanganyika kwa kuwa mambo ya serikali za mitaa si ya Muungano.
 
Kwa sasa Halmashauri karibu zote ziko taabani. Hakuna fedha inayoshushwa kwa ajili ya miradi,other charges. Inafikia wakati hata hela ya kununua rimu moja ya karatasi wanakosa. Kwa kweli Serikali Kuu iwashushie fedha zao kama zilivyopangwa na kuidhinishwa kwenye bajeti.
Mirija imekatwa wapiga deal
 
Kwa sasa Halmashauri karibu zote ziko taabani. Hakuna fedha inayoshushwa kwa ajili ya miradi,other charges. Inafikia wakati hata hela ya kununua rimu moja ya karatasi wanakosa. Kwa kweli Serikali Kuu iwashushie fedha zao kama zilivyopangwa na kuidhinishwa kwenye bajeti.
Yani kamaa mm nilifiwa na mtoto wangu halmashauli Ya Mkuranga walishindwa jlkuniudumia wakasema nizike tu watanirudishia gharama zangu lakini mwaka sasa unaisha kilanikifuatilia naambiwa Pesa hazijaletwa yanishida kwelikwel
 
Mirija imekatwa wapiga deal
Hela zilizoibwa kwa wingi nchi hii hazikuibwa kwenye ngazi ya Halmashauri bali kwa hao hao unaodhani wamekata mirija ya wenzao. Magufuli wakati akiwa waziri wa Ujenzi, wizara yake ilituhumiwa na CAG kufuja mabilioni ya shilingi ya wizara hiyo. EPA, Kagoda, Tangold,Meremereta, Escrow,IPTL,TTCL, na madudu mengi yaliyoifilisi hii nchi yetu hayakutokea kwenye ngazi za Halmashauri bali kwenye ngazi yao wapenda ugandamizaji wa Halmashauri.
 
Leo nimeambiwa Halmashauri nyingi ziko mahtuti kifedha ila wanaogopa kusema kwa kuwa wengi wao wameajiriwa na "serikali Kuu" kupitia utumishi. Yaani Halmashauri zinataka kuajiri watendaji wa mitaa na vijiji hawaruhusiwi kwa kuwa "Utumishi" hawajatoa kibali cha kuajiri. Yaani mahitaji ya Halmashauri kuajiri lakini ni Utumishi ndiyo wanatoa kibali cha kuajiri. Zifuteni tu hakuna haja ya hizi Halmashauri kuwepo!!
 
Back
Top Bottom