meningitis
JF-Expert Member
- Nov 17, 2010
- 8,394
- 4,748
Natoa hoja ni jinsi gani Taifa hili adhimu linavyotakiwa kuendelea kuwa imara miaka 50+ ijayo.
Niliwahi kufundishwa kwenye historia na somo la siasa kuwa wakati wa ukoloni wazungu waliwekeza kwenye elimu ya muafrika mtanzania kujifunza kazi za ukarani na kidoogo mambo ya management na sheria.
Yote hii ilikuwa ni kujaribu kuwapata watumishi wa kurahisisha utawala wao.
Elimu ya mzungu haikuwekeza kwenye utaalamu au teknolojia ya baadaye.
Mfumo huu wa kielimu na attitude hii ya serikali ya mkoloni ulirithiwa na serikali yetu baada ya uhuru kimatendo na pia ilirithiwa na jamii yetu kifikra.
Utawala wa Mkapa uliweka misingi ya utekelezaji wa kuongeza wasomi tu japo haukuwa specific ni wasomi wa namna gani haswa waliohitajika na watakaohitajika katika soko huria la kidunia.
Jk aliendelea kuwaridhisha wanajamii kwa kuongeza idadi ya vyuo again bila kuwa specific sana ingawa alijaribu kuongeza watumishi katika eneo la afya na elimu zaidi.opportunity hii ilitumiwa na jamii kipofu kwa kukomalia elimu rahisi rahisi na za kupiga mdomo au blah blah ili kupata mkate wa kila siku.hapa ndipo makanjanja na wasio na uwezo walipofanikiwa kupenya na hatimaye leo hii wamejaa mitaani na kwenye taasisi zetu wakitusumbua kwa maneno mengi na ujuvi usio na muekekeo.Hapa unakutana na kundi kubwa la wanasheria,wanahabari na wachumi nusunusu.hapa ndipo jamii ilipogundua umuhimu wa kufoji vyeti
NIkienda moja kwa moja kwenye mada ...nasisitiza kwa kutoa hoja binafsi ili tuichambue na pengine ikiwezekana ichukuliwe na watunga sera.
Huu ni wakati wa serikali kuachana na kusomesha au kudhamini wasomi wa kozi za kupiga tumba kama nilivyozitaja hapo juu.
Ni wakati wa kutoa udhamini kwa wataalamu wa afya,elimu ya sayansi ,kilimo ,electronics,nishati
na mafundi mchundo ambao watakuwa ni watendaji na wabunifu zaidi.
Anayetaka kusomea kupiga blah blah na tumba ajidhamini au adhaminiwe na familia yake.
Wazo hili lina athari za kisiasa lakini lina faida kubwa sana kwenye kututoa hapa tulipo na kuendana na dunia ya kileo au sera ya viwanda tuliyoahidiwa.
NAWASILISHA.