Hoja binafsi bungeni

Hoja binafsi bungeni

Chereko

Member
Joined
Jul 20, 2009
Posts
54
Reaction score
16
Ningekuwa mbunge ningetoa hoja binafsi kama ifuatavyo:

HATUA DHIDI YA MAJANGA YA BARABARANI: Kutokana na madereva wa vyombo vya moto kutobanwa na sheria kali, uzembe utaendelea nchini na tutazidi kuwapoteza ndugu zetu kutokana na ajali. Aidha ajali zinaathiri uchumi kutokana na ndugu wa wahanga kujikuta wanahangaika na misiba au kuuguza badala ya kufanya shughuli nyingine za maendeleo. Pia madaktari wanaongezewa mzigo wa kazi ambazo sio lazima kwani zingeweza epukika.

1. KUDHIBITI PIKIPIKI
Kwa kuwa tangu pikipiki zimehalalishwa kufanya biashara ya abiria, nchi imepoteza nguvu kazi kubwa kutokana na vifo na kuacha watu wengi vilema, hali ambayo kwa kiasi kikubwa inasababishwa na utovu wa kutofuata sheria za barabarani kwa waendesha pikipiki, na kwa kuwa waendesha pikipiki hao hawasikii, basi iwepo sheria ya kukamata na kupiga mnada pikipiki yoyote itakayoendeshwa kwa makosa, pamoja na mwendeshaji kunyang'anywa leseni.

2. KUDHIBITI MWENDO KASI WA MABASI
Kwa kuwa vifo vingi vimetokana na mwendo kasi, basi au lori litakalopatikana linaenda mwendo kasi, lori au basi hilo likamatwe na kufungiwa kutembea sio chini ya mwezi mmoja, wakati huo huo hifadhi yake ilipiwe Tshs50,000 kwa siku bila serikali kuwajibika kwa lolote wakati wa kipindi hicho, na endapo mmiliki wa chombo hicho atashindwa kukomboa, basi hilo au lori hilo lipigwe mnada. Wakati huo huo dereva mhusika anyang'anywe leseni.

3. KUTANUA BARARABARANI
Kwa kuwa madereva wengi wanatanua barabarani, gari lolote linalotanua likamatwe na kuwekwa yadi siku saba kwa malipo ya Tshs 50,000 kwa siku na kama baada ya siku saba mmiliki wake ameshindwa kulikomboa gari hilo lipigwe mnada. Pia dereva wake anyang'anye leseni. Adhabu kama hizo zitolewe kwa wale wanaokatisha barabara wakati taa nyekundu zimewaka.

4. WAENDAO KWA MIGUU
Wananchi wanakatisha barabara hovyo na kukwepa magari kwa "Vibega" bila kujali wakati magari yanaenda na hawatumii au hawavuki kwenye alama za Pundamilia. Watu hawa wakamatwe na kulipa fine ya hapo kwa hapo Tshs 2,000 na kama hana afungwe pingu za miguu na kukalishwa chini kwa muda wa masaa matatu.


Kutekeleza hayo serikali itumie askari wa barabarani pamoja na makampuni ya udalali ambao watakamata na kuzuia magari, kudai pesa na mwishowe kuuza kwa mnada. Kwa nini tuhangaike kuwatoza wafanyakazi kodi kubwa wakati kuna pesa nje nje zimekaa?

Nawakilisha!
 
Back
Top Bottom