Hofu yatada tena Mtwara

Hofu yatada tena Mtwara

tunduruboy

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2013
Posts
423
Reaction score
218
HALI ya wasiwasi kwa wananchi wa Manispaaya Mtwara, Mkindani, imeanza tena baada ya jana kusambaa kwa ujumbe kwenye simuza mkononi unaowataka wakazi hao kufanya shughuli zao hadi kesho na keshokutwa hawatakiwi kufanya kazi zozote. Ujumbe huo ambao umesambazwa kwenye simu zamkononi, unalenga kuwahamasisha wananchi hao wasifanye kazi Jumatano ya wikihii, ili waangalie mjadala wa bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwakawa fedha 2013/2014.
Pamoja na mambo mengine, wanataka kujua hatmaya gesi iliyopatikana mkoani humo.

Ujumbe huo uliopatikana unasomeka hivi:"Waziri wa Nishati na Madini ameghairi kuzungumzia bajeti ya Nishati na Madinikwa muda wa siku 4, ina maana mpaka Jumatano. Kwa hiyo, kama una shughuli yakufanya, fanya ili Jumatano tafadhali usifanye kwa sababu machafuko ambayoyanataka kutokea si ya kawaida, tafadhali wafahamishe watu wa kusini wote ambao wanataka mabadiliko. Tusiache kauli mbiu yetu ni gesi kwanza, uhai baadaye.

Kutokana na kusambaa kwa ujumbe huo,wananchi mkoani hapa wameanza kujawa na hofu, ambapo mkazi wa Manispaa yaMtwara Mikindani, Amina Saidi aliiambia MTANZANIA, kuwa kitendo cha kuibukatena kwa ujumbe huo ni cha hatari.

"Sasa tunaambiwa tusifanye shughuli zetu na mwisho Jumanne, ujumbe huu unatutia wasiwasi mkubwa, tena unatunyima raha kwasababu tuna watoto wadogo.

"Na tumetakiwa kupitia ujumbe huu kuwa sikuya Jumatano tuangalie Bunge, kwani kitendo hiki kinatuogopesha sana kwanikatika ujumbe huu, unasema kuwa kutatokea machafuko, sasa sisi tuna watoto wadogo tutakimbilia wapi na watoto wetu?" alisema na kuhoji Amina.

Akizungumza na MTANZANIA kwa njia ya simu,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Linus Sinzumwa, alisema hawezi kuzungumziasuala hilo hadiafanye uchunguzi.

Jumatatu, Mei 20, 2013 04:42 Na Fatuma Maumba, Mtwara


HALI ya wasiwasi kwa wananchi wa Manispaaya Mtwara, Mkindani, imeanza tena baada ya jana kusambaa kwa ujumbe kwenye simuza mkononi unaowataka wakazi hao kufanya shughuli zao hadi kesho na keshokutwa hawatakiwi kufanya kazi zozote. Ujumbe huo ambao umesambazwa kwenye simu zamkononi, unalenga kuwahamasisha wananchi hao wasifanye kazi Jumatano ya wikihii, ili waangalie mjadala wa bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwakawa fedha 2013/2014.
Pamoja na mambo mengine, wanataka kujua hatmaya gesi iliyopatikana mkoani humo.

Ujumbe huo uliopatikana unasomeka hivi:"Waziri wa Nishati na Madini ameghairi kuzungumzia bajeti ya Nishati na Madinikwa muda wa siku 4, ina maana mpaka Jumatano. Kwa hiyo, kama una shughuli yakufanya, fanya ili Jumatano tafadhali usifanye kwa sababu machafuko ambayoyanataka kutokea si ya kawaida, tafadhali wafahamishe watu wa kusini wote ambao wanataka mabadiliko. Tusiache kauli mbiu yetu ni gesi kwanza, uhai baadaye.

Kutokana na kusambaa kwa ujumbe huo,wananchi mkoani hapa wameanza kujawa na hofu, ambapo mkazi wa Manispaa yaMtwara Mikindani, Amina Saidi aliiambia MTANZANIA, kuwa kitendo cha kuibukatena kwa ujumbe huo ni cha hatari.

"Sasa tunaambiwa tusifanye shughuli zetu namwisho Jumanne, ujumbe huu unatutia wasiwasi mkubwa, tena unatunyima raha kwasababu tuna watoto wadogo.

"Na tumetakiwa kupitia ujumbe huu kuwa sikuya Jumatano tuangalie Bunge, kwani kitendo hiki kinatuogopesha sana kwanikatika ujumbe huu, unasema kuwa kutatokea machafuko, sasa sisi tuna watotowadogo tutakimbilia wapi na watoto wetu?" alisema na kuhoji Amina.

Akizungumza na MTANZANIA kwa njia ya simu,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Linus Sinzumwa, alisema hawezi kuzungumziasuala hilo hadiafanye uchunguzi.
 
lets go never give up, united we stand divided we fall
 
Back
Top Bottom