EWGM's
JF-Expert Member
- Jul 22, 2013
- 1,521
- 2,112
Ndugu wa-Tanzania wenzangu kama tunavyoelewa sintofahamu iliyoko visiwani ni kama mafuta ya petroli yaliyo wazi yanasubiri chanzo cha moto ili kulipuka.
Seif Sharif Amad ameshatoa tamko kuwa subira yake ina kikomo na kesho ni mwisho hataweza kuivumilia tena sababu subira yake inaweza ikamletea kiungulia.
Chonde chonde wenye WENYENCHI madaraka yasiwapunguzie maono, matatizo ya Zanzibar ni ya kwetu wote. Yakiripuka visiwani moto ule wa mafuta unauwezo wa kutembea juu ya maji na Tanganyika utafika.
Ninayaona mimi isije ikawa mwisho wa neon hili TAN-ZAN-I-A, kwa hali ilivyo sasa na yanayojiri linaweza kumeguka vipande vipande ikiwa WENYENCHI wasipokuwa makini. Kama MWANANCHI nachukua nafasi hii kuwaomba WENYENCHI kaeni chini muyamalize na busara ifuate mkondo wake, aliyeshindwa akubali matokeo hata kama ni machungu kumeza.
Tunaomba busara itumike ili tuweze kupata suruhu ya huu mvutano uliopo visiwani. Kauli ya Jecha isije ikawa chanzo cha moto huko visiwani ili kuyapa nafasi mafuta kulipuka na pia naamini kuwa WENYENCHI wanaweza kuifuta kauli ya Jecha kupitia vyombo vyao husika.
WANANCHI sisi ni masikini sana tunategemea kukidhi mahitaji yetu kutokana na misaada ya hao MABWANA WAKUBWA. Tumeona yanayoanza kuwapata jirani zetu Burundi, ni WANANCHI ndiyo tunaoumia na siyo nyie WENYENCHI.
Vurugu ni kama KANSA tu ni vizuri ukaiwahi kwenye hatua za mwanzani kabisa kuliko ikasambaa na kushindwa kuithibiti. Kuna watu wanasubiri waone nani anaanzisha basi na wao wanafata mkumbo na itakuwa hatari sababu hata Wabara wakiona kumbe Visiwani wameweza kwa nini na sisi tushindwe. Tukifika hapo inawezekana basi itakuwa tayari WENYENCHI mmechelewa na haipendezi na wala siombei tufikie huko.
Kwa sasa kauli za vitisho au maneno yasiyo na busara hayafai WENYENCHI kaeni chini meza moja muyamalize, kuna kukubali kwa kutokubaliana ili mradi muafaka ufikiwe na mnusuru nafsi zetu sisi WANANCHI masikini.
Hatma ya TAN-NZA-I-A iko mikononi mwenu WENYENCHI tumieni hekima mliyopewa na Mwenyenzi Mungu ili mnusuru nafsi zetu sisi WANANCHI maskini.