HOFU YA UKIMWI NA STDS IMEPOTEA

uajekundu

JF-Expert Member
Jan 14, 2016
541
461
Habari wanajamvi,
Kuna jambo linanishangaza sana, siku za hivi karibuni kumekua na wimbi la wanaume wengi kujikuta wakipenda kufanya ngono bila kinga, tena bila hata kujali anayefanya nae ni nani na hamjui kabisa. nna rafiki yangu amekutana na ex boyfrend wake walioachana kwa miaka mi3, juzi wamekutana yule boyfrend akampa lifti mdada akamwambia amemiss anaomba waende wakae sehemu waongee kidogo, jamaa si akampeleka gesti eti anamuomba waingine wakagegedane, imagine hawajaonana kipindi hote hicho na hawajapima, yani mtu mnabebana tu mnaenda ku sex. Jamani wanaume tupende afya zetu, haya maisha tu, tutajikuta tunapotea kizembe zembe, mambo ya kuparamia watu sio mazuri kabisaaa, hata wale wanaoanzisha uhusiano mpya mhakikishe mnapima na wapenzi wenu magonjwa yapo na ukimwi bado upo. tuache tamaa na mazoea.
 
Back
Top Bottom