Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,487
Mkuu wa Wilaya ya Magu, Karen Yunus amemtolea maneno ya vitisho mwandishi Neema Emmanuel wa Nipashe na kudai Atammaliza na kumhoji iwapo kuna mtu anamtuma kutokana na kile alichodai kuwa ni mwandishi huyo kumchafua kwa namna anavyong’ang’ania kuripoti hali mbaya ya Shule ya Msingi Lupemba iliyopo wilayani kwake.
Shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 2006 na kuwa na wanafunzi 651, ilifungwa kwa muda usiojulikana mapema mwaka huu ili kupisha ujenzi wa vyumba walau vinne vya madarasa.
Baada ya kuchapishwa kwa habari hiyona NIPASHE , DC Karen alimpigia simu mwandishi wa habari hiyo na kumpa vitisho kutokana na kile alichodai kuwa hajamtendea haki. DC Karen alipiga simu hiyo Jumapili iliyopita, majira ya subuhi.
“…kwa sabababu haya mambo unayoyaandika yanasomwa na wengine ambao wana maamuzi makubwa… wee unatumwa nini? Kuna mtu anakutuma? Na kama hakuna mtu anakutuma kwa nini unang’ang’ania hivyo?”
“Mi nakwambia... halafu wee bado mtoto mdogo… wee una miaka mingapi… wewe ni mwanangu wa mwisho… mi nakwambia Neema… lakini kwa sababu umeamua kutumaliza, tutamalizana… lakini na wewe you should wait for your chance (usuburi nafai yako), na hayo mambo yapo nakwambia," alisema DC Karen katika baadhi ya vitisho alivyotoa kwa mwandishi.
"Andika neno karma… usipende kuharibia watu wanajihangaikia maisha yao, kwa miaka mingi, eeh.” Alisema DC huyo.
Naye Mwandishi wa habari alipohojiwa alikiri:
“Ni kweli nimepata vitisho kutoka kwa Mkuu wa Wilaya… lakini sioni nilichokosea kwa sababu hakuna lisilokuwa la kweli katika ripoti hiyo,” alisema mwandishi Neema wakati akizungumza na mwandishi wa habari hii kuelezea vitisho alivyopata kuhusiana na ripoti juu ya hali ya shule ya msingi Lupemba.
"Shule imefungwa na wanaosoma ni madarasa ya nne na saba, kuna watoto hivi sasa huishia kuchunga ng’ombe. Yote hayo ni kweli tupu."
Magufuli Kasi yako inawaweka roho juu sana hawa ma-DC waliopewa vyeo na Mkwerre ipo siku watakufa kwa presha.
Source:Nipashe