figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,487
Ikiwa zimesalia siku saba kuanza tena zoezi la bomoa bomoa kwa wakazi waliojenga mabondeni kasi ya Kuweka alama za X katika nyumba za mabondeni limeendelea kushika kasi katika maeneo ya Mto msimbazi huku baadhi ya wananchi wakiendelea kuchukua hatua ya kunusuru mali zao huku wengine wakiendelea kupatwa na mshangao kutokana na zoezi hilo.
Katika barabara ya kawawa eneo la mkwajuni maafisa zaidi ya mia moja kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi ya Mazingira NEMC pamoja na wale wa manispaa ya Kinondoni wamekuwa wakiweka alama za x katika nyumba zilizopo Mambondeni hali ambayo imeonyesha kuwastua wakazi wa eneo hilo baada ya kuelezwa kuwa januari 5 zoezi hilo litahamia eneo hilo.
Mwanasheria kutoka Nemc Manchare Suguta amewataka wananchi kuzingatia Muda uliotolewa na serikali kwa kuokoa mali zao ili kupisha zoezi hilo.
Katika eneo la Jangwani huku kukiwa na Ulinzi mkazi wa FFU kazi ya kuweka alama za X huku baadhi ya nyumba zilizojengwa eneo hilo zikitambuliwa na manispaa hiyo ingawa walipotakiwa kuthibitisha baadhi ya wananchi walitoa hati za viapo vya mahakama au AFFIDAVITY badala ya hati za umiliki wa nyumba.
Chanzo: Channel ten