Hodi Hodi ninaingia viwajani

MPIGA ZEZE

JF-Expert Member
May 16, 2011
2,539
2,296
Wana-JF ninayo furaha ya kujiunga nanyi katika viwanja vya JF. Mimi ni MPIGA ZEZE yule wa Mwalimu na mwanafalsafa E. Kezilahabi. Niwamegee kidogo anavyojitambulisha:
"Nitaimba wimbo gani tofauti na za zamani?
Je nitaeleza kisa cha kichaa
Aliyepotea njia akagonga mlango
Wa nyumba yake kuuliza?
Au cha Anastazia msomi
Aliyeiba senene waliokaangwa?
Mtaniita mwongo nikiwambia
Kuwa Deusi alikufa kimzaha
Roho yake ilitoka Pap! Ikaepuka
Harufu mbaya ya zizi la ng'ombe
Na kutokomea gizani ikitabasamu
Na kusindikizwa na kwaya ya kunguru
Waliomcheka Padri aliyeleta Sakramenti
Ungekuwepo kumwona ndama aliyezaliwa
Akalambwa na mamaye kisha akasimama
Akayumbayumba kutafuta ziwa shingoni
Ni mimi MPIGA ZEZE kipofu wa kijijini
Nikilewa naimba matusi..."
 
Kipofu wa kijijini ni mfu hapa mjini. Kafie kwa vipofu wenzio . . . . Mpiga zeze weeh.
 
tehe tehe tehe!
Karibu sana.
Akifika Katavi utapata kinywaji, we msubiri hapo hapo sebuleni.
 
Wana-JF ninayo furaha ya kujiunga nanyi katika viwanja vya JF. Mimi ni MPIGA ZEZE yule wa Mwalimu na mwanafalsafa E. Kezilahabi. Niwamegee kidogo anavyojitambulisha:
"Nitaimba wimbo gani tofauti na za zamani?
Je nitaeleza kisa cha kichaa
Aliyepotea njia akagonga mlango
Wa nyumba yake kuuliza?
Au cha Anastazia msomi
Aliyeiba senene waliokaangwa?
Mtaniita mwongo nikiwambia
Kuwa Deusi alikufa kimzaha
Roho yake ilitoka Pap! Ikaepuka
Harufu mbaya ya zizi la ng'ombe
Na kutokomea gizani ikitabasamu
Na kusindikizwa na kwaya ya kunguru
Waliomcheka Padri aliyeleta Sakramenti
Ungekuwepo kumwona ndama aliyezaliwa
Akalambwa na mamaye kisha akasimama
Akayumbayumba kutafuta ziwa shingoni
Ni mimi MPIGA ZEZE kipofu wa kijijini
Nikilewa naimba matusi..."


Nilikua sina jinsi but kukupa thanks yako ya kwanza...lol... Karibu..


The Following User Says Thank You to MPIGA ZEZE For This Useful Post:

Asha D (Today)​
 
Back
Top Bottom