Hodi hodi naingia, hebu nipeni nafasi

Hodi hodi naingia, hebu nipeni nafasi

Mohammed Hamad

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2011
Posts
3,988
Reaction score
1,310
Naanziliza Karima, alo mwema asilani,
Rabbi mwingi wa huruma, msifika Rahmani,
Illah Mola Karima, Mola uso na kifani,
Hodi wana Jamii, hoja nilete jamvini.

Hodi Invisible hodi, nipange japo pembeni,
Kueleza lisobudi, humu mwako MTANDAONI,
Na tusiwe wakaidi, kwa kujivuna nchini,
Kiswahili na kinyumbani kitumike jamvini.
 
Karibu sana ila subiri utatumiwa 'SHARIA' za humu,
karibu..
 
Karibu sana ila subiri utatumiwa 'SHARIA' za humu,
karibu..

Shukrani sana kwa ukarimu wako na wala usikhofu sheria muhimu popote pale na ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha zinafuata.
 
Naona umekuja na real name yako karibu 2tameet FB

Kwanini wewe unaogopa kutumia jina lako halisi? mbona hii nchi sasa hivi ina freedom of speech ? Kuhusu FB na accept watu ninaowajua tu niliofanya nao kazi sehemu mbalimbali/ndugu/jamaa/marafiki na niliosoma nao. ila hukatazwi kuangalia profile yangu user name Mohammed Hamad Shossi.
 
Ahsante sana na nimeanza kuwa mwenyeji japo nakosea wakati mwingine kupost threads zangu pasipotakiwa but hopeful will be expert soon. Once gain thank you very much bro.

As time goes on utazoea tu hata mbuyu ulianza kama mchicha
 
Karibu Mohammed Shossi,karibu saana tuuu.Siye tupo.ila polepole taratibu:welcome:
 
Mh mi moyo wng unasita kukukarbsha. Nahc km mwnyej vle??? Ila karibu sana bro.
 
Mh mi moyo wng unasita kukukarbsha. Nahc km mwnyej vle??? Ila karibu sana bro.

Hizo ni hisia zako tu na hukatazwi, ninachoweza kusema nimekuwa "guest" for not less than 4 years lakini nikaamua niingie na kuwa member kwahiyo sina ugeni kihivyo! na kikubwa nimeona niingie kwa jina halisi na sio kama wengi mlivyo humu JF.

Mwisho kabisa shukran kwa karibu yako ya mashaka.
 
Back
Top Bottom