Nalipanga kudamka,siku itapowadia
Foleni kuziepuka,kwani huleta udhia
Kura npige haraka,bila kuzua ghasia
Hodari kaenguliwa,kura yangu ni hapana
Hamasa imetoweka,amekatwa mgombea
Ambaye nilimtaka, kura yangu kumgea
Hamu imenchujuka,mwanzo ilo nkolea
Hodari kaenguliwa,kura yangu ni hapana
Kituoni nitafika,haki yangu kutumia
Hapana ntaandika,kwa uchungu na hisia
Kwani nnayo hakika,hafai alobakia
Hodari kaenguliwa,kura yangu ni hapana
Yazamani nakumbuka,vile tulivyozoea
Wengi wasoelimika,fomu hawakukosea
Sasa imezoeleka,kuwa ni patapotea
Hodari kaenguliwa,kura yangu ni hapana
Mzalendo sitochoka,bado nimeazimia
Kuepuka kudhurika,kura sitozisusia
Ndio njia isoshaka,ya kukomboa jamia
Hodari kaenguliwa,kura yangu ni hapana
DARUWESHI MKULU WANYIKA
MWENE SESEME NOGAYA WA SABA (Vll)
MAGOMENI MWEMBECHAI DAARUSSALAAM
Foleni kuziepuka,kwani huleta udhia
Kura npige haraka,bila kuzua ghasia
Hodari kaenguliwa,kura yangu ni hapana
Hamasa imetoweka,amekatwa mgombea
Ambaye nilimtaka, kura yangu kumgea
Hamu imenchujuka,mwanzo ilo nkolea
Hodari kaenguliwa,kura yangu ni hapana
Kituoni nitafika,haki yangu kutumia
Hapana ntaandika,kwa uchungu na hisia
Kwani nnayo hakika,hafai alobakia
Hodari kaenguliwa,kura yangu ni hapana
Yazamani nakumbuka,vile tulivyozoea
Wengi wasoelimika,fomu hawakukosea
Sasa imezoeleka,kuwa ni patapotea
Hodari kaenguliwa,kura yangu ni hapana
Mzalendo sitochoka,bado nimeazimia
Kuepuka kudhurika,kura sitozisusia
Ndio njia isoshaka,ya kukomboa jamia
Hodari kaenguliwa,kura yangu ni hapana
DARUWESHI MKULU WANYIKA
MWENE SESEME NOGAYA WA SABA (Vll)
MAGOMENI MWEMBECHAI DAARUSSALAAM