JembeNaNyundo
JF-Expert Member
- Dec 9, 2016
- 533
- 652
Naangalia sakata la Mo Enterprises kudaiwa kodi kwa kitu ambacho kalipia na mlipwaji kutoa risiti halali lakini kwa sababu za mlipwaji kutotunza kumbukumbu vizuri kesho anarudi kukudai malipo aliyolipwa!!! Ajabu atakuomba uthibitishe kulipa kwa kutoa risiti aliyokupa yeye mwenyewe.
Hii shida iko kila sehemu katika taasisi zote za serikali na binafsi. Mimi hili lilikuwa likinisumbua sana sekondari na chuo kikuu, hususani kipindi unapofanya clearance.
Nakubali kwamba kutunza risiti za malipo ni muhimu sana, lakini utunzaji wangu wa risiti usikupe mlipwaji ahueni ya kutotunza taarifa vizuri na hivyo kesho kuanza kunisumbua.