Hizi simu janja kwenye mapezni ni balaa

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Oct 26, 2018
21,713
35,514
Habarini wana jamvi,

Wiki hii kuna ticha mmoja huko Shinyanga kaamua kuachana na UBAHARIA, na kumpeleka manzi wake wa siku nyingi kumtambulisha kwao.

Jamaa akajua akifika home hawezi kula mzigo so akaamua kulala gesti na bishosti akajisevia. Demu kila mara anachati na Simu yake, ticha akamind ila akala kimya, kulipokucha akachukua boda na mamzi wake kuelekea kwao, wamepanda mshkaki.

Kufika porini njiani wakashuka (kumbe amenunua panga) akamcharanga mapanga na ndoa ikaishia hapo, ila bora kamnyoosha (angemchazara vibao na mitama ingetosha)

JANA:
Naelekea zangu home mida ya saa2 usiku maana nlichelewa kutoka kibaruani. Kufika Kimara Korogwe kukawa na JAM ya kufa mtu nkaamua kukaa kwenye Bar Mpya karibu na kanisa la KKKT inaitwa IBUNGU.

Kuna Baharia yupo na manzi wake ila yupo bize sana na smart phone yake. Manzi ni mkali kinyama, kumbe pembeni mabaharia kibao wanamtolea macho nikiwemo mimi.

Bidada akatoka kwenda chooni, aisee alivamiwa baharia flani (aliniwahi)akachukua namba, lijamaa lipo bize na simu yake baada ya nusu saa yule fala akasepa nae (karoho kaliniuma kiaina) lijamaa lake linang'aa macho tu (shenzitype).

Mkitoka out na wenza wenu mzime simu, sio mko bize na magroup ya whatsap mtachapiwa sana.

nshamaliza.
 
Nuggas be looking for shit just to have an excuse to use the word 'baharia'. Don't give a fvck whether shit is understandable the victory is in using the word 'baharia'
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom