HIZI NI SERIKALI MBILI TOFAUTI AU??

HIZI NI SERIKALI MBILI TOFAUTI AU??

Smart-brain

Senior Member
Joined
Mar 17, 2014
Posts
101
Reaction score
62
Habari wakuu;
Nikizungumzia upande wa Tanganyika, tumebarikiwa kuwa na katiba, sheria, kanuni, taratibu, pamoja na miongozo (licha ya mapungufu) mbalimbali ili kutufanya tuishi kwa utaratibu na amani.
Lakini kwa upande mwingine hatuoni sheria hizi zikiwashughulikia wahusika kikamilifu au kupendelea kundi la watu kwa manufaa yao.
Mh. Dr Ndalichako(W.Elimu) amefanikisha kupeleka Mahakamani na kushtakiwa kwa Walimu walioonekana kukiuka maadili ya kazi, eg Mwl. aliyempiga Mwanafunzi kwa fimbo na kupelekea kufariki kwake. Hili alilofanya Mh. Waziri ni jema kuhakikisha Walimu wanakumbuka mipaka yao ya namna ya kutoa adhabu.

Wizara ya Mambo ya Ndani, nasikitika imefeli kabisa kuwashughulikia wavunjaji wa sheria kwa kuwapeleka Mahakamani (au kwa taratibu zingine) ili kuweka utendaji uliotukuka kwa Watumishi hawa wa Umma. Hapa ninalenga zaidi JESHI LA POLISI. Hili jeshi linautaratibu wake wa kushughulikia wavunjaji wa kanuni za kijeshi, haziendi kinyume na taratibu, huwa hata anayeshughulikiwa nazo, kweli hujiona ni mkosaji hasa.
Lakini, tunaona baadhi ya Polisi hawa(sijui ni kwa maagizo au la) jinsi wanavyokiuka Haki za Binadamu hata kupelekea kunakosemekana "Kuua Raia Wasio na Hatia au Kujeruhi kwa RISASI za Moto nk", (ref: Mbeya, Tabora, Dar Es Salaam). Kinachotia tashwishwi ni pale "tukio linapoonekana kutendwa na wao" lakini tunaona mambo yakifunikwa tu na kuacha MASWALI MENGI KULIKO MAJIBU. Kama Mh. Lugola na Mh. Insp. wa Jeshi la Polisi wangefuata "nyayo" za Mh. Ndalichako , jeshi letu lisingepakwa matope! Mh. Lugola, katika hili VAA MASK!!!!

"Mh. Lugola ebu pia kata ngebe za mgambo wanaojiona ni Mafarao sasa, bila hivyo ....!!!"
 
Wewe hii Tznia inachukulia waalimu kawaida sana, hawana watetezi mishahara midongo yani hiyo ni fani ya umasikini sana....unafikiri angekua dakitari au dereva wa wizari ndo amasababisha kifo hicho wangekua charged "murder" mkuu wa mkoa moja alipinga mtu risasi hadharani ila alichajiwa kuua bila kuhusudia.....hiyo kazi ya ualimu ni ya wanyonge tu mimi siwezi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
DAH walimu wakisoma hii watachukuliaje? pamoja na yote haya walimu lazima wawepo. unapoomba kwenda kusoma unaomba kukutana na walimu!
 
Wewe hii Tznia inachukulia waalimu kawaida sana, hawana watetezi mishahara midongo yani hiyo ni fani ya umasikini sana....unafikiri angekua dakitari au dereva wa wizari ndo amasababisha kifo hicho wangekua charged "murder" mkuu wa mkoa moja alipinga mtu risasi hadharani ila alichajiwa kuua bila kuhusudia.....hiyo kazi ya ualimu ni ya wanyonge tu mimi siwezi

Sent using Jamii Forums mobile app
Hawa Walimu si kwamba hawana mtetezi, la hasha! Ninamkumbuka kiongozi mmoja wa CWT (jina limenitoka kidogo ), huyu aliichachafya kidogo Awamu ya 4, ila Walimu dhambi yao kubwa inayowatafuna ni "kutumika kisiasa!" Viongozi wa juu wakipewa "vihela vya mboga" watasimamia haki za watu? Hapana!
 
Back
Top Bottom