Hizi ni salamu zangu kwako..Najua nitakuudhi

MT255

JF-Expert Member
May 3, 2012
3,606
4,912
Watu wengi hawajui kwa nini wazungu huwa wanasema LIFE BEGINS AT 40. Yaani maisha yako ya kweli yataanza ukifika umri wa Miaka 40. Wakati ambapo unatakiwa uwe na elimu uliyoihitaji.. Uwe na familia yako tayari.. Uwe na kwako tayari siyo umepanga bado.. Uwe na usafiri binafsi.. Uwe na kitu chako cha kukuingizia pesa na si kutegemea ajira peke yake. At 40!!

At 40 inabidi uwe unaishi. Siyo ndo unaanza kujaribu hiki na kile. At 40 inabidi uwe unasomesha zaidi kuliko kusoma wewe japo kuongeza maarifa ni vizuri.
At 40 unatakiwa uwe umeshapata exposure kwa kusafiri huku na kule dunia hii kujua wengine walioendelea zaidi wanaishi vipi na wewe ufanyeje?

Sasa hivi vitu haviji ukiwa upoupo tu hutafuti fursa za kukusaidia kuwa na maisha tofauti upo tu una LIKE kila kitu facebook na Instagram unatuma tu picha za ajali za mabasi zikikosekana unatuma za migomo ya madereva mgomo ukiisha unatuma za mafuriko kama mvua zimeisha unatuma picha za Lowassa yaani umekuwa mtumwa wa simu. Ikikosa network unalalamikia kampuni ya simu utafikiri hiyo network unafanyia kitu cha maana. Gallery yako imejaa vitu vya ajabuajabu tu. Havikufikishi popote na umri unazidi kwenda unazidi kusogea miaka 40 hivi hivi. Maisha ya kweli yataanza ukiwa na miaka 40. Wakati ambapo watoto wako hawatakula LIKES zako za instagram bali wanahitaji chakula. Wanahitaji ada. Wanahitaji maisha bora. Wewe unasubiri maisha bora CCM ndo wakupe. Wasipokupa unataka UKAWA waje wakupe ukiwa umekaa Instagram unaLIKE picha za Wema Sepetu. Umeshajua wema akifika miaka 40 atakuwaje? Ulishajiuliza wanamuziki waliovuma miaka 15 iliyopita wakiwa na umri wa miaka 25 hivi au 30 wakati huo wana miaka mingapi na wako wapi sasa hivi. You see? Unayemfuatilia kila siku kavaaje kaamkaje katembea na nani hakusaidii kuwa na maisha mazuri. Maisha bora hayaji ukiwa unafatilia nyimbo gani zimetoka udownload. Maisha bora hayaji kwa KU-ENTERTAIN brain yako bali kwa kuifikirisha akili na kufanya mambo ambayo wachache tu ndo wanafanya.

Kwani wanasoka wangapi wako kama mbwana samata
Kwani Wanamuziki wangapi wako kama Diamond au Ali kiba
Wacheza ngumi wangapi wako kama Frances cheka? Unadhani wamepata mafanikio wakiwa wamekaa na TECNO chumbani wana comment kuhusu migomo? No. Walikuwa wana-hussle wakati wengine wanachat.

Seriously. Diamond unayemfollow anafanya kazi hivyo hivyo. Anatoka studio saa saba usiku wewe uko kwenye page yake unaLIKE. Huwezi kuona kuwa uko tofauti. Anaandaa maisha akifika miaka 40 awe na kila kitu wewe utakuwa unalalamikia network ya tigo tu na kutuma picha za sijui gari limegonga treni. Kwa hiyo wewe ndo NIPASHE kwa sasa au?

Anyway. Kuwa serious na maisha yako angalau basi kwa ajili ya watoto wako na wajukuu zako. Aise huyu mzazi wetu alifanya jambo la maana. Au unadhani watazikuta hizo comments na LIKES zako? No. Wanapaswa wakute nyumba, viwanja, account za benki zinazopumua. Siyo account inaingiaga mshahara tu halafu by tarehe 10 iko empty ushakomba kila kitu!!!! Wanatakiwa wakute assets za maana angalau.

mwaka huu 2016 umeeka mikakati gani kuweka msingi wa maisha tofauti sana na kuhakikisha ufikapo umri wa miaka 40?
Au bado unategemea mshahara wa laki 8 (tena hapo kabla ya makato) uje ubadili maisha yako).
Kwa waajiriwa, Microsoft ya Bill Gates inapunguza wafanyakazi 800. Kama ulikuwa hujui. Unadhani kampuni yako ndo utakaa hapo milele?
Be careful my friend.
" KUZALIWA MASIKINI SI KOSA BUT KUFA MASIKINI NI DHAMBI"
 
Haya mkuu, mshukuru Mungu wako kwa kukujalia, ukawa na akili nzuri, umbile lisilo na ulemavu, ukapewa elimu nzuri, ukapata fursa n.k.
 
Yaah ujumbe murua kujitambua bado msamiati ila lazima tupigane na sio excuses kibao ooh babaa yangu hakunisomesha mara kwetu sikukuta hata baiskeli ni lazima tuchangamkie furda sio wote walio soma wana mashabiki mazuri na sio wote ambao hawajasoma wana maisha mabovu.
 
Sisi ambao tuko above 40 hatuhusiki na huo mshushuo,hakyamungu umewananga kinoma.Meseji sent
 
Najuta kwanini 40 haijanikuta,maana hii sms inanihusu sana.Ila nashukuru mtoa mada,nimejifunza kitu hapo hasa kuwa na kitu cha historia kwa wajukuu na watoto wng hapo mbeleni.Ngoja niendelee kujipanga zaidi ili 40 inayokaribia inikute salama!!
 
Kulike picha/post Fb au humu Jf inachukua dakika ngapi... pambana na life ila usisahau unahitaji muda na familia yako, kupumzika na muda wa kufahamu kinachoendelea kitaifa na kimataifa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom