Hizi ndio tofauti kati ya malezi ya baba na mama

Mwanangu anapigwagwa na babake mpka huruma naishia kumkanda tu na kumchemshia mayai.
Na hivi si mwanangu wa kumzaa ukimtetea au ukiongea tu utasikia baadae rum ndo unataka kupendwa na mtoto wa kambo??haaaa

Dogo ana umri gani?

Anakuwa kweli amefanya makosa ya hovyo?
 
Mwanangu anapigwagwa na babake mpka huruma naishia kumkanda tu na kumchemshia mayai.
Na hivi si mwanangu wa kumzaa ukimtetea au ukiongea tu utasikia baadae rum ndo unataka kupendwa na mtoto wa kambo??haaaa
basi wewe una roho nzuri, kibongobongo wamama ndio wanaoongoza kupiga watoto hasa kama ni wa kambo
baba sio mlezi mzuri sio kwa sababu anapiga watoto, no...sababu ni don't care na muda mwingi anawaza ishu zake kuliko huyo mtoto
 
baba kakaa kwenye beseni
baba kamning'iniza mtoto ..

hivi kwanini wanaume wasingezaliwa na akina baba?
maaana kina mama wanawazaa lakini hawaigi mfano wao wa malezi
 
Umesema kweli kabisa,ndo maana Mungu hakuweka utaratibu
wa mtu au jinsia moja kuwa na uwezo wa kuzaa mtoto.
alijua malezi yanatofautiana.Mama akimfurahisha mtoto na kumfanya awe
mayai baba amchangamshe mtoto ili ajiandae kupambana na maisha
siku za mbeleni wakati hayuko na wazazi wake.

Kama ningepewa uchaguzi wa kulelewa na mmoja
ningechagua kulelewa na baba,maana hiyo mikiki mikiki ina mwisho
pale unapoyajua maisha na kuanza kuchangamka mwenyewe.
au fuatilia maisha ya watoto waliolelewa na mama wa kambo
utakuta wengi wanajua kujituma,na anaweza kuishi popote
na mtu yeyote.
 
wazee wengi wana show Tough love.........
Nimeipenda hiyo mzee patriotic wa kirusi...
 
Mimi nina uhakika wengi wetu hatujalelewa na baba kabisa lakini tupo vizuri, familia nyingi za ki afrika baba huwa halei mtoto na wengine unakuta hajui hata jina la ubatizo la mtoto wake, lakini wanakuwa wazuri tu na wa kujitegemea japokuwa wamelelewa na mama
 
Malezi ya Baba ni ya kukutengeneza kujitegemea,ila tatizo lake anayaharakisha mno. Wakati Mama ni full kudekezwa,athari zake zinaonekena baadae ukubwani unakuwa mzito kujiamulia mambo yako kwa muda muafaka.
 
Ahahahahhahaahah nimecheka sana...hasa hiyo ya dingi kuoanda baiskeli yeye af dogo anaukanyaga
 
Hapo wakiwa wote wawili...ila.unadhan ingekua single parennt baba na mama nani bora? Kila mtu ana umuhimu ila single parent kwa faza ni mziigo mitoto inaharibika sana kuliko kwa maza ambae atakulea akiwa peke yake...kwenye pita pita yangu nimegundua hakuna wazazi wapo serious kwa malezi kama wamama ambao wanalea peke yao
 
kweli mkuu, malezi ya baba ni hovyo kabisa
 
Ushuhuda wa kujishuhudia ni mara chache sana kukuta umezingatia
vigezo,ushuhuda halisi ni ule unaoshuhudiwa na wengine.
kama kila mtu angejijua madhaifu yake angejirekebisha siku hiyo hiyo.
Ndo maana ni muhimu kukubali kukosolewa maana si rahisi
ukayafahamu mapungufu yako

Wengi waliolelewa na mama peke yake ni walegevu.
na waliolelewa na baba peke yake ni wakakamavu
mpaka inakuwa kero,ndo maana Mungu akaweka
familia iwe na baba na mama,ukiachilia mbali bahati
mbaya zinazosababisha baadhi kukosa mzazi kwa kufiwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…