Hizi ndio fursa/kazi unazoweza kuzifanya katika maeneo ambayo yana migodi ya dhahabu

Think2

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2025
Posts
2,193
Reaction score
3,957
Maeneo;

Maeneo yote maarufu kwa uchimbaji wa madini ya DHAHABU katika kila mkoa kwa nchi nzima ya TANZANIA.

Kwa hapa tanzania mikoa/sehemu ambazo zina madini ya DHAHABU kwa wingi ni Geita ( nyarugusu, mgusu, nyaruyeye, buzibwa, iseni na lwamgasa n.k), shinyanga ( kahama, mwime, bulyanhulu, lunzewe n.k), tabora (nzega,), singida (Londoni, sekenke n.k), mbeya (chunya), tanga (handeni, kilindi, mjembe), mara (buhemba,nyamongo n.k), dodoma (nzuguni), pwani (kibindu, kwamduma), RUKWA (mpanda).

1. UCHIMBAJI/UTENDAKAZI KWENYE MIGODI YA WATU (WAPONCHAJI):
hiii haihitaji mtaji wowote wa wewe kwenye kufanya kazi kwenye migodi ya dhahabu zaid kinachohitajika ni ujasiri wako wa kuingia kwenye mashimo marefu na kufanya kazi. mara nyingi watu hawa huwa hawalipwi mishahara bali mkienda kufanya kazi chini ya mgodi mara nyingi mnagawana mifuko ya dhahabu mliotoa kwa siku husika kati ya nyie wafanya kazi na mwenye mgodi, mara nyingi mkitoa mifuko ya mawe 10 ya kilo 25 mgawanyo ni kuwa WAFANYAKAZI yenu 3 na mwenye mgodi yake 7.

2. KUNUNUA MADINI YA DHAHABU: hapa kwenye kununua madini haya kumegawanyika sehemu kuu mbili ambazo ni mnunuzi mdogo ambae huyu atakuwa anaenda migodini kwa wachimbaji kwenda kununua madini na kwenda kuuza mjini, na mnunuzi mkubwa huyu ni mtu/kampuni ambae anakuwa na ofisi mjini ya kununulia madini na yeye atasubiria wanunuzi wadogo yoka migodini waje kumuuzia yeye, mnunuzi mkuwa anaruhusiwa kusafirisha madini yake nje ya nchi ila mnunuzi mdogo haruhusiwi kutoa madini yake nje ya mipaka ya tanzania, wanunuzi wote wawili wanatakiwa kuwa na leseni ya kukunua madini ambapo mnunuzi mdogo broker licence (290,000/= kila mwaka garama ya leseni), na mnunuzi mkubwa master dealer licence (around 3 milion kwa mwaka garama ya leseni).

3.KUFUNGUA MRADI WA KUSAGA MAWE YENYE DHAHABU/MRADI WA MAKARASHA:
karasha ni mashine maalum inayotumika kuyasaga mawe yenye dhahabu hadi yanakuwa unga ili madini hayo yaweze chenjuliwa kutoka katika mawe hayo, mashine hizi ni maarufu sana hasa kwenye maeneo ambayo kuna migodi ya mwamba, ITAKUGARIMU MTAJI WA MILIONI ZIPATAZO 10 kukamilisha mradi wako wenye karasha 1 la kusaga mawe, kumbuka madini ya DHAHABU yakiwa kwenye jiwe huwezi yatoa mpaka yasagwe kwenye hili karasha hivyo huu ni mradi muhimu sana kwenye eneo lenye migodi ya mwamba, wenye migodi wakitoa mifuko yao ya mawe chini ya mgodi lazima watafute karasha lilipo ili wasage mifuko yao.

Na kwa kawaida kusaga mfuko 1 wa mawe ni shilingi elfu 3 kila mfuko, na itachukua muda wa dakika 30 mpaka 45 kwa karasha kusaga mfuko mmoja wa mawe, sasa kule migodini mtu anawekeza mpaka anamiliki karasha zaidi ya 10 na muda wote karasha yako bizee maana mifuko imesimama inahitajika isagwe.

NOTE: ukiwa na mradi wa makarasha fursa zinakuwa nyingi sana za kupiga pesa kirasi kwani kma ww unakarasha lako na watu wanakuja kusaga mawe yao ili waipate dhahabu mwisho vipi kama utakuwa na leseni yako ya kununulia madini ili kila anaekuja kusaga kwako awe anakuuzia dhahabu yake? maana ww utakuwa upo karibu nao sana czani kama asage kwako mawe halafu akatae kukuuzia madini labda uwe unanunua kwabei za kulalia ila ni rahisi sana ukiwa na makarasha kuwa mnunuzi wa madini maana wateja watakuwa wanakuja hapo hapo ulipo.

4.KUANZISHA MRADI WA LEACHING PLANT (MRADI WA KUCHENJUA MARUDIO):
kuwekeza katika mradi huu unahitaji mtaji ambao sio chini ya milioni 200 au zaid kwani kama utaanzisha mradi huuu kwa mwezi hukosi kuchenjua madini zaidi ya kilo 1.

karasha linaposaga mawe na kuwa unga, unga huu huwekwa kwenye karai na kuchanganywa na maji na kumwaga maji haya kwenye mteremko/slop ili kuinasa sahabu baada ya kutega gunia kwenye slop hiyo, sasa KITALAM hapa dhahabu inayokamatwa kweny hili gunia ni asilimia 33% tuu na iliyobaki inaenda kwenye lile tope na yale maji, hivyo basi hili tope ndio tunaita MARUDIO.

kwa kule migodini, wewe ukiwa na karasha lako na watu wanakuja kusaga mawe yao kwenye karasha lako, hili tope litabaki kuwa lakwako mwenye karasha na hili ndio litakalo kupa utajiri sio kusaga ile mifuko ya elfu tatu tatu, ww mwenye karasha ukiwa na tope hili jingi watu watakuja kulinunua Na ww utauza TIPA MOJA NIKATI YA MILIONI 70 MPAKA 150MILION utaliuza na hii ni baada ya mnunuzi kuchukua sampo ya tope lako na kupeleka maabara na kupima kuona kiasi cha dhahabu kilichomo ndani.

NOTE: Mradi wa karasha watu/wamiliki hutajirikia kwenye hili tope, ww fanya juu chini watu waje wengi kusaga mawe yao kwenye mashine yako ili tu WAKUACHIE HILI TOPE ndani ya mwaka 1 tuu hukosi tani kazaa za tope unapiga hela.

NARUDI KWENYE MAADA YANGU YA LEACHING PLANT:
hiii ni technolojia ya kuchukua tope/MARUDIO yenye dhahabu ndani yake yanayokusanywa toka kwa wachimbaji wadogo na tope hili kuwekwa ndani ya matank maalumu na tope hili kuwekewa maji na maji haya kuwekwa KEMIKALI MAALUMU INAYOITWA CYANIDE, kazi ya kemikali hiii ni kuyeyusha madini ya DHAHABU nakuwa katika mfumo wa kimiminika, baada ya mataki haya kuwekewa sumu hiii mirija maalumu kutoka katika matanki haya na kwenda katika kijumba maalum au CONTROL ROOM, maji haya kuwekewa kitu kinachoitwa KABONI na kazi ya kaboni ni kufonza madini ya DHAHABU kwenye hayo maji na kuyaacha maji yakiwa hayana dhahabu, kaboni hizi huchukuliwa na kwenda kuchomwa katika mashine inayoitwa ELUSION MASHINE hapo ndio dhahabu HUPATIKANA ikiwa uji uji na kugandishwa katika umbo maalum la tofali.

NOTE: KEmikali ya cyanide ni sumu hatari sana maji hayo yatokanayo na process hizi akinywa binadamu au mfugo lazima ufe hapo hapo kwani inakata utumbo.
 
"TIPA MOJA NIKATI YA MILIONI 70 MPAKA 150MILION"
Mkoa gani wanauza tipa moja kwa hiyo bei!? Ishu ya marudio umeizungumza kwa wepesi sana na haujasema ili uipate hiyo 70 ni average gani ya sampuli ya hilo rudio, na vipi gharama zake na mengineyo mengi.
 
H
Hapo amelukaluka kama amekanyaga tope la rudio.huwez sema tipa m70,bila kujua kiasi cha bpm inasomaje na gharama za uendeshaji zilifika ngapi,m70 sibora apeleke mwenyewe plant.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…