Hizi mbio zote ni kuelekea wasikokujua

Rose Mayemba

Verified Member
May 7, 2012
720
500
Tazama,
Wote wamepigwa upofu, hakuna anayeona mbele,kina mmoja anakaza mwendo kuelekea kusikojulikana, si wakubwa wala wadogo wote wanahangaika.

Hawakuwahi kufikiri kama haya yoye yangetokea, walijisahau, wakafanya mambo mengi kwa hila wakiamini hakuna anayeona, walitumia neema iliyoshushwa na Mwenyezi Mungu kwa nufaa ya matumbo yao, wala hawakuwahi kuwakumbuka waliotembelea tumbo kutafuta riziki zao..

Mungu asingekaa kimya, pengine alihuzunishwa sana na mwenendo mbaya uliokithiri wa mabwana hawa, akakasirika, amemwamsha kila aliyekuwa katika usingizi mkali wenye mateso yasiyo simulika ili kuushuhudia uozo wao, naye aliyetoka usingizini amefurwa na hasira, anauchungu wa kuishi taabuni muda mrefu huku hazina yake wakigawana wachache, sasa amedhamiria kufanya mapinduzi...

masikini...
Hakuna hata mmoja kati yao anayeliona anguko lao, wengi wanatabiri tu, na wengine kujifariji kama bado neema i upande wao. Mambo yanaharibika kila kunavyokucha lakini wapi, MUNGU amekwisha kuwaondolea ufahamu wao, ili wasije wakafunguka , kisha wakaongoka...

HAKUNA MSHAHARA UNAOZIDI MATENDO, MALIPO HUFANYIKA KWA KADRI YA JUHUDI YA KAZI ULIYOPEWA.
 

ROBERT MICHAEL

JF-Expert Member
Oct 23, 2012
4,922
2,000
Ila sidhani kila mtu ameamka kuona hao mabwana wanavyofanya. Wengine huamini umasikini umeletwa kwa ajili yao kwa hiyo baragumu la ukombozi bado lahitajika ili wawepo wengi wajuawo hao mabwana wafanyavyo kuwafanya wao wawe duni na si Mungu aliyewafanya wawe duni.
 

REMSA

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
2,577
1,225
Ni heri waendelee kuwa na macho wasione,na waendelee kuwa na masikio wasisikie ili watakapokuja kufunguliwa
macho na masikio yao tayari watakuwa wamechelewa milango imeshafungwa.

Ni wajibu wa wenye macho na mzigo wa uchungu kuwafanya hawa waliofura kwa uchungu na hasira ya
mateso na manyanyaso waliyoyapata kwa kitambo kirefu,kufunguka zaidi na kujua ni nini wajibu wao na
jukumu lao kwa ajili ya kujitoa ktk kifungo cha hawa mahayawani wa mwituni'
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom